Ni Kama machozi ya samaki ndani ya maji.

Niliposikia majina ya ajira mpya za walimu yametangazwa leo nikajipa moyo labda na Mimi jina langu limo.Taratibu nikaanza kutazama kwenye simu sikuamini nikahisi ndoto,Jina langu sijaliona kabisa nikajipa moyo au orodha ya majina hi ni fake lakini ukweli ukabaki palepale ni majina original.Machozi yakanilenga nikalia kwa hisia nikahisi kukosa tumaini na nguvu kupungua nikaanza kutafakari maswali mengi Sana.
Nimejitolea kufundisha takribani miaka mitano Leo hii naachwa?!,Nimekuwa mzalendo kwa nchi yangu mtoto wa mnyonge Mimi!.Majina ya walimu wazalendo wanaojitolea shule za serikali ina maana hayakwenda TAMISEMI? mbona tulituma majina nahisi Kama utani je,nitaendelea kuwa volunteer Tena au nifanye Mambo yangu.Nimekuwa volunteer kwa muda mrefu nitaificha wapi aibu yangu.Tulitiwa moyo tuendelee Kujitolea tutakumbukwa daaaah kwa kweli nimechoshwa na mwendo.Wanafunzi niliowafundisha watanifikiriaje? Nilitamani kuwa mwalimu lakini bahati haikuwa yangu,msinicheke ndugu zangu Kujitolea nastafu kuanzia Leo nipokeeni mtaani nifundisheni plan B.Wote tuliokosa tusikate tamaa Wala Tusinung'unike tushukuru kwa yote maisha lazima yaendelee. Kama umeguswa unaweza kutoa pole na kutupa maneno ya kututia moyo kwa wale wote tuliokosa na ushauri jinsi gani tupambane mtaani ili kulisongesha gurudumu la maisha.Ni maombi yangu Tukumbukwe tuliokuwa tunajitolea tutaficha wapi sura zetu maana tayari tumeshaanza kutukunwa na kuonekana wajinga tulioenda kupoteza muda na mwisho wa siku tumetemwa Kama bigijii(Banzoka).
-Toa ushauri wenye mtazamo chanya wa kutujenga vijana sio kejeri,matusi na siasa Tunaitaji ushauri wako.
By Mr Volunteer mwenye huruma nisiye na bahati.nilitoka kwenye familia ya walalahoi,YAHWEH tutie nguvu vijana wote tuliokata tamaaaa kwa Kila mtu na mapito yake.Ameni
funzo: "HOPE BUT DON'T EXPECT" expectations kills

Ushauri:"don't give up" check plan B kulingana na mazingira uliyopo

Nb: "huruma na kukata tamaa ni dhambi"

Asante

Asante
 
daah pole mkuu fikria nje box
kweli ni kwenda kukusanya Kila kitu kilichokuwa kinanihusu ofisini na kumuhaga Mkuu wa shule na walimu.Kwenye kota za shule ni kufungasha vilago na kutokomea itakuwa ngumu kuendelea Kujitolea kufundisha wakati tayari maji yameshamwagika yaaan ikiwezekana na jina nibadili sio kwa kudhalilika huku miaka mitano ujitolee huku ukijipa matumaini one day yes,mwisho wa siku mchezo unabadilika.Inaumiza Sana hasa pale utakapokutana na wanafunzi wako wakakuamkia shikamoo mwalimu wakati huo upo kitaaa umejichanganya na misheni town.Neno ningejua hujaga mwisho wa safari aliimba Mrisho mpoto.Muda nilioupoteza hawawezi kufidia,gharama za maumivu hawawezi kufidia aliimba chid Benz ft Q chila.ni maombi yangu Wahusika wa TAMISEMI watufikilie maana Kama ni uzalendo tuliuonyesha Sana yanapotokea haya inakatisha tamaa.
 
Pole Sana mkuu, usikate tamaa , hujachelewa , endelea kupambana kwa njia nyingine utafanikiwa tuu , mungu yu pamoja nawe
 
Pole Sana mkuu, usikate tamaa , hujachelewa , endelea kupambana kwa njia nyingine utafanikiwa tuu , mungu yu pamoja nawe
Ameni,nashukuru kwa kunitia moyo.Ana heri mtu Yule ambaye kinywa chake huwabariki wenzie na kuwaombea.Ana heri mtu Yule ambaye mzigo wa mwenzie hubeba Kama wake hushauri na kutoa neno la faraja na kulejesha tumaini.Balikiwa Sana kamanda wangu,Asanteni nyote kwa ushauri wenu hata wale walionikejeri ninawashukuru pia.Mmepoteza muda wenu kunishauri na kunitia moyo Sina zaidi ya kusema Asanteni lengo letu ni Moja kujenga na si kubomoa.shukrani
 
Nimeumia saana kwa ujumbe huu maana na mile no mhanga kibaya zaidi shule ambayo najitolea kuna mwalimu kaletwa wa wasomo Yale Yale tena na watu mtaani wasema nilifeli chuo, Serikali tuhurumieni walimu wa kujitolea jamani.
 
Back
Top Bottom