Leo Wadau nawaletea majina manne ya Wanasiasa nguli kwenye siasa za Tanzania yaani January Makamba,Edward Lowassa,Dr Wilbrod Slaa na Zitto Kabwe.Haya ni majina ya Wanasiasa mchanganyiko yaani wakongwe na damu changa kwa pamoja waliojijengea heshima kubwa kwa Wananchi wa Tanzania kutokana na michango yao mbalimbali kwa Taifa hili.Wadau mnachotakiwa kufanya ni kujenga hoja zenye ushahidi usio na shaka (substantial arguments) juu ya mmojwapo wa Wanasiasa tajwa hapo juu unayemuunga mkono kugombea Urais na hatimaye aje kuwa Rais wa Tanzania 2015.Dadavua namna unavyomfahamu Mwanasiasa huyo kuanzia historia yake ya utendaji toka alipoanza kabla hajajulikana mpaka hapa alipofikia.Dadavua pia kuhusu misimamo,mawazo na maono yake juu ya aina ya Taifa analotaka kulijenga kisiasa,kiuchumi na kijamii ili na sisi wengine tusiomfahamu tuweze kumjua ili basi ikifika mwaka 2015 tufanye maamuzi sahihi (informed decisions) kwa kumchagua mtu sahihi (right leader) wa kuliongoza Taifa letu pendwa la Tanzania.Karibuni Wanajamvi!