Ni January Makamba,Edward Lowassa,Dr Wilbrod Slaa au Zitto Kabwe 2015?

TECH WIZ

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
1,675
553
Leo Wadau nawaletea majina manne ya Wanasiasa nguli kwenye siasa za Tanzania yaani January Makamba,Edward Lowassa,Dr Wilbrod Slaa na Zitto Kabwe.Haya ni majina ya Wanasiasa mchanganyiko yaani wakongwe na damu changa kwa pamoja waliojijengea heshima kubwa kwa Wananchi wa Tanzania kutokana na michango yao mbalimbali kwa Taifa hili.Wadau mnachotakiwa kufanya ni kujenga hoja zenye ushahidi usio na shaka (substantial arguments) juu ya mmojwapo wa Wanasiasa tajwa hapo juu unayemuunga mkono kugombea Urais na hatimaye aje kuwa Rais wa Tanzania 2015.Dadavua namna unavyomfahamu Mwanasiasa huyo kuanzia historia yake ya utendaji toka alipoanza kabla hajajulikana mpaka hapa alipofikia.Dadavua pia kuhusu misimamo,mawazo na maono yake juu ya aina ya Taifa analotaka kulijenga kisiasa,kiuchumi na kijamii ili na sisi wengine tusiomfahamu tuweze kumjua ili basi ikifika mwaka 2015 tufanye maamuzi sahihi (informed decisions) kwa kumchagua mtu sahihi (right leader) wa kuliongoza Taifa letu pendwa la Tanzania.Karibuni Wanajamvi!
 
I wish Lowassa asingekuwa CCM... Nampitisha Slaa kwa ajili ya mageuzi ... Zitto hafai kuwa kwenye list! muongeze JJM, Lisu na yule jamaa wa NHC...
 
Hapo ipo hv
2015 Edo lowasaa
2025 ZZK akati pm n Januar Makamba
2035 Kizaz kipya tena
Hapo Babu enu slaaa ashajifia zamaaani bila kupaonja magogoni
 
Drslaa.................born to be a leader

hao wengne stoi kura hata nikiwa ndoton

bora nipgie gogo,kuliko hao mafsad na wasaliti
 
Mbona kwenye list simuoni Nchemba? Make naskia naye anauwazia urais.
 
Dr.slaa na lowasa wameshajichokea hao. Inaweza ikatufanya tz tukafanya uchaguzi mdogo wa urais.watafia ikulu hao wagonjwa. January hajafanya chochote cha maana.
 
January naye ni mwanasiasa nguli!! Mnalishushia hadhi neno nguli!!
 
Back
Top Bottom