Ni janga na aibu kwa taifa kuwa na vijana aina ya Mdude Nyagali

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,356
9,786
Ndugu zangu Watanzania,

Nawasikitikia sana wanaompatia maiki Mdude nyagali kuzungumza, ni aibu kwa unayemsikiliza ,ni fedheha kwa unayefuatilia anachokizungumza. Alikuwa anazungumza mpaka Dr Slaa anatamani azibe masikio au ampokonye maiki. Ni aibu pia kwa mtu mwenye akili Timamu kukaa meza moja na Mdude na ukawa unasikiliza anachozungumza Mdude.

Mdude Ni mtu ambaye unaona wazi kuwa kichwani hana mpangilio mzuri wa mawazo na muunganiko mzuri na wenye mawasiliano mazuri kati ya akili na mdomo wake. Ndio maana unaona anaongea kwa kupayuka,kuropoka na mihemuko ya hali ya juu sanaa. Anaongea kinachotua na kutangulia kufika kinywani pake. Amekosa utulivu wa akili na mawazo. Anaongea pasipo kujiandaa wala kujuwa ataanza na nini,kufuatia na nini na katika hatua ipi atazungumzia nini na kugusa wapi na wapi.

Mdude siyo mtu sahihi wala mwenye kuweza kuwashawishi watanzania wenye akili Timamu na wanaojitambua kuingia barabarani na kufanya maandamano. Kwa kuwa mtu akimtizama na kumsikiliza kwa dakika chache tu anagundua na kupata jibu kuwa kuna vitu alivikosa na amevikosa katika makuzi na malezi yake.

Mdude anaonesha wazi hakupata malezi bora ya wazazi au walezi wake katika makuzi yake. Ni kama alijikulia tu pasipo uangalizi wa aina yoyote ile, alikuwa bila kuwa na mtu wa kumlea ,kumuongoza,kumchunga na kumkanya. Ndio maana unaona hata ongea yake haimshawishi mtu timamu kumsikiliza maana hana adabu wala hekima wala staha. Pia inaonyesha kuwa Mdude anaweza kuwa ni mhanga au mtumiaji wa vitu kama bangi ambayo amewahi kutumia siku za nyuma.

Mdude anapaswa kusaidiwa katika mambo yafuatayo.kwanza awe anaelekezwa juu ya nini akazungumze mbele ya hadhira au watu ,hapa aelekezwe hoja za kujikita na mahali pa kuishia tofauti na sasa anapozungumza kimizuka na kwa mihemuko mpaka anapoteza Dira na muelekeo.pili awe anaandika yale yote atakayozungumza tofauti na sasa inavyoonyesha akikosa muunganiko kwa yale anayozungumza na kuishia kuserereka tu bila breki ya mdomo .

Afundishwe namna ya kuwa mtulivu anapozungumza pamoja na kutumia lugha za staha ,heshima na busara ambazo zinaweza kusikilizwa na watu wa aina zote bila aibu iwe wachungaji, mapadri ,mashehe,vijana ,wazee,akina mama n.k. yaani atumie lugha inayolenga hadhira pana na siyo kuongea utafikiri anawahutubia au anadhamilia kufikisha ujumbe kwa walevi walioshindikana. Atumie lugha inayoweza kuwaunganisha watu bila kujali rika zao,umri wao,jinsia zao, vyeo vyao, vipato vyao na Dini zao.

Siku zote mtu unaweza kuungwa mkono au kutoungwa mkono kutokana na uwasilishaji wako wa hoja.hakuna anayeweza kumuunga mkono mtu anayeonekana kama mhuni mhuni na aliyezibuka kiakili. Ni ngumu sana kwa mdude kuweza kuwashawishi watanzania kwa jambo lolote lile na akaungwa mkono. Vijana aina yake wanakuwa wanatudhalilisha vijana wote na kuonekana sisi ni wahuni wahuni tu. Vijana aina yake hata wangekuwa enzi za uhuru wasingeungwa mkono na watanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Nawewe upo kwenye hilo kundi huna tofauti na yeye. Punguza uchawa huyo mama yako labda amfikie baba ako wananchi hawezi kuwafikia labda anawafikia kwa kuweka vilaza kwenye nishati ambao wanasababisha hata mafuta kuwa tabu japo yapo. Unateseka kwaajili ya ujinga mda mwingine nakupinga asee usiwe chawa wa kijinga
 
Tafuta opportunity kama Chawa wenzako ambao Wakiinua midomu tu Uwaziriiii..Paaaa ( Nadhani yule Professor wa Singida Unaona Kapewa ulaji Kanyamaza kimyaaa, Pia huyu Mbunge wa Jimbo la kitunda pia juzi Kalamba. So do you thing is your time .

Basi Pambana na wewe Upate , CHAWA weeeee... MKATABA NI MBOVU WALA HAUTAJI KUWA NA ELIMU YA FORM TWO ILI KUJUA HILO...
 
Tafuta opportunity kama Chawa wenzako ambao Wakiinua midomu tu Uwaziriiii..Paaaa ( Nadhani yule Professor wa Singida Unaona Kapewa ulaji Kanyama Pia huyu Mbunge wa Jimbo la kitunda pia Kalamba. Pambana na wewe Upate , CHAWA weeeee...
Mimi sitafuti uteuzi wala fadhila hapa jukwaani.
 
Niliona aibu sana kiukweli hadi nikawaza kuwa Mdude anavuta bangi au ameathirika bangi.
Huwezi kupendwa na wote na huwezi kuchukiwa na wote pia...
FB_IMG_1693917789656.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku mmoja niliona taarifa inatolewa kutaja watu waliokamatwa, miongoni mwao wakamtaja mdude huku wametanguliza kwa kumuita "muheshimiwa mdude" nilicheka sana
 
Back
Top Bottom