Ni Jaji yupi ambaye hukumu zake unapenda sana kuzisoma?

Wakuu,
Ni Japi yupi ambaye hukumu zake unapenda sana kuzisoma?
Haijalishi,awe ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Rufaa!
Mie binafsi nazikubali hukumu za Samata J,.!
Ana good command of English language na huwa sikosi lakujifunza kwake!
Na mwisho nazikubali za Jaji Lubuva pia!
Wewe je?
Wengi sana wako vizuri sana (>90%) orodha ni ndefu...ungetaka majaji wanaoboa/ukiona tu jina la Jaji una-close page kufungua nyingine ndo orodha iko fupi sana.

Coz kuna Jaji HCT (....) wa zamani kidogo sijawahi kuona hata hukumu yake iliyokatiwa rufaa CAT imekubarika zote ni... "the trial judge misdirected himself....."
 
sagaci waweza wataja hao majaji wanaobo,japo kwa ufupi?
Pia waweza mtaja huyo jaji ambaye hukumu zake haziwahi kukatiwa rufaa c.a.t?
 
Lameck mfalila, Justice mwesiumo, Mapigano, koroso, mwalusanya, lugakingira, MLAY, ORIYO, RUTAKANGWA, KATITI....
 
Ni Kweli Samatta alikuwa akitoa hukumu nzuri sana na zenye kueleweka. Napenda sana hukumu zake.

Jaji mwingine ni marehemu Mwalusanya. Huyu alikuwa anatoa kesi hukumu yake kama anafundisha vile. Usipoelewa hukumu za huyu jamaa bora uachane ma mambo ya sheria. Hata Mahakama ya rufaa walikuwa wanapata tabu kupindua hukumu za huyu jamaa. alikuwa akisimamia haki, tena hata kama ni against serikali. Aliipiga chini serikali mara nyingi sana. So sad mahakama na serikali kwa ujumla wakamtupa mkono, hawakumpromote na alipostaafu hadi kufa alitelekezwa. Atabaki legend kwenye mahakama ya tanzania na hadi leo hakuna jaji aliyemfikia. RIP.
Kuna huyu jamaaa Rutakangwa. Hukumu zake zimesimama na ni very authoritative. reasoning yake utaipenda, hababaiki na anakuwa imara kwenye msimamo wake.

Mjamaa mwingine ni Massati bwana. anaandika long judgments na anaweka ma authority ya kufa mtu, ni researcher mzuri.

Mwingine ninaevutiwa na hukumu zake japo kwa mbali ni Nsekela, anajitahidi kuandika. Kalegeya pia anajitahidi.
Umeongea mengi ila umeharibu uliposema hakuna atayemfikia....
Chipeta alikua ni Judge wa maJudge ...
 
Back
Top Bottom