Ni Jaji yupi ambaye hukumu zake unapenda sana kuzisoma?

Jaji Kahwa Rugakingira RIP
Mtikila vs State ktk kesi ya mgombea huru Mahakama kuu Dodoma 1992
Jaji Rugakingira alikuwa anajua sana kuandika decents za kesi
Itafute hukumu hiyo ipo online
 
Jaji christian Ronaldo ni jaji mzuri sana hivi punde alimaliza kesi vizuri kati ya R madrid na juventus amongst zingine vilevile messi ni jaji mzuri sana haijawahi kutokea
 
Nguli bora kwenye fani yenu nyinyi mangwini ni Living Legend Chenge jamaaa ni mastermind anapenya kwa hao majaji wenu wote
 
Kalegeya ana ngeli ya kutishaaaaaa
Hahaaa. Ni kweli. anapangilia kiingereza chake vizuri hadi unavutiwa kuendelea kusoma hukumu yake. Amekaa sana pale Commercial Division kabla ya kuwa promoted kwenda mahakama ya rufaa. Kule aliamua kustaafu kwa hiari kabla ya mda wake kufika baada ya kuona junior judge kapewa ujaji mkuu na kuwaacha wakongwe wakitazamana tu. Almanusra majaji wote wa rufaa waachie ngazi, bahati nzuri diplomasia ilifanya kazi yake, majaji wengine wakakubali kubaki, Dr. Bwana akakimbilia mahakama ya kimataifa, jamaa kalegeya kaamua kustaafu kwa hiari. Hatakagi mambo ya mchezomchezo.

Mwingine kwenye mambo ya lugha ni P. A. Rugazia. Huyu jamaa anapamba kiingereza hadi raha. ana vi terminology vyake hivyo ukiiona tu hukumu utajua huyu ni Mwamba Mwenyewe Rugazia, Mzee wa misimamo - haogopi mabosi zake. Jamaa kasota sana mahakama kuu ingawaje alikuwa ni kichwa, hakubahatika kuwa promoted kwenda mahakama ya rufaa. Wengi wanasema ni sababu ya kiburi na majigambo yake. Kastaafu hivi karibuni (mwaka jana kama sikosei).
 
Living Legend Chenge ata upambe hukumu kwa viterminology vya kilatino yeye lazima akufanyie ubaya tu....Havard akwenda kutalii yule mwamba.....yule mwamba ndio anafaa kuitwa wakili msomi sio awa wengine mbwembwe nyingi hakuna kitu
 
Living Legend Chenge ata upambe hukumu kwa viterminology vya kilatino yeye lazima akufanyie ubaya tu....Havard akwenda kutalii yule mwamba.....yule mwamba ndio anafaa kuitwa wakili msomi sio awa wengine mbwembwe nyingi hakuna kitu
Hv kwa nini mzee chenge hajapata ujaji mpk leo? ?
 
Back
Top Bottom