Ni ipi tofauti ya Victor Ambrose na Abdulrahaman Kinana?

Rufiji

Platinum Member
Jun 18, 2006
1,881
941
Victor Ambrose ni kijana aliyekamatwa na jeshi la polisi na kushtakiwa kulipua kanisa huko Arusha. Kijana huyu ambaye anafanya biashara ya kuwabeba watu na pikipiki, maarufu kama bodaboda, alikodishwa na mtu anayesadikiwa kufanya kitendo hiko cha kinyama. Kama walivyo vijana wengi wanaofanya hiyo kazi, wao kazi ya ni kutoa huduma ya usafiri tuu na wala hawaulizi wateja wao ni kitu gani au jambo gani wanalotegemea kulitenda.

Swali ambalo ninajiuliza, kama watu watu wengi wameweza kukubaliana na utetezi uliotolewa na Abdulrahaman Kinana kuwa yeye ni mmiliki wa meli na wala hajui kinachopakiwa kwenye meli (meno ya tembo). Kwa nini, tusitumie sheria hiyo hiyo tunapoangalia hii issue ya Ndugu Ambrose?
 
nafikiri ingekuwa bora zaidi ila wanaangalia wadhifa tofauti kati ya watu hao wawili sheria sio msumeno tena ule wa jk Nyerere
 
Back
Top Bottom