Ni ipi dawa nzuri 4 malaria?

Drphone hiyo dawa uliyopewa na huyo mzee ni ipi na inapatikana wapi,tafadhari mkuu tuelekezane, na dawa hiyo ya Zandu ya kihindi iko mtaa upi hapo kariakoo
 
Pole ndugu, dawa za malaria zipo nyingi sana ingawa nyingi zimesha develop resistance. Kwa sasa dawa za malaria kulingana na national guide line zipo nne tu. Kwa uncoplicated malaria zipo mbili mseto (ALU) na Duo-cortecxine na kwa complicated malaria zipo quinine na artemether injection. Kwa hiyo kama una malaria kwanza pima ukigundulika unamalaria dr atakushauri utumie dawa gani kulina na unavyopresent wakati huo. Ingawa bado kama unadawa ambayo huwa inakufaa inaweza pewa priority. Achen kunywa madawa ovyo yanamadhara ukitumia bila mpangilio maalum. Al the best
 
SOMA HAPA:-
Dawa za maleria zipo nyingi nzuri na mbaya,kinachotakiwa ni mtu kuwa makini na mdadisi.
Kwa sasa kutokana na usugu wa malaria,unashauriwa kutumia dawa ambazo ni mchanganyiko(mseto) ingawa kuna baadhi ya watu dawa ambazo si mseto bado zinawatibu. Dawa ambazo ni mseto zilizo sokoni tanzania na maelezo yake ni kama ifuatavyo
1-Coartem-huu ni mchanganyiko wa dawa mbili(Artemether+Lumefantrine 20/120mg) Dawa hii inapendekezwa na wizara ya afya na ni nzuri kwa kweli kwani watu wengi(si wote) wanapona bila matatizo au kwa matatizo yanayovumilika. Tatizo lake ni vidonge vingi kwa dozi(24) pia ni kwamba mwanzoni ilikuwa inatengenezwa Switzerland lakini mchina kaaingia na anatengeneza under licence,unajua mambo yake, pili serikali ilipandisha kodi kwa kampuni binafsi za dawa kwa hiyo pamoja na kutoka china bado garama zake si chini ya Tsh 15000 kwa dozi,lakini hata hivyo serikali inazipata kutoka swiz kwa bei nafuu lakini kwa paki tofauti na za mwanzo(sijui ubora wake) huu ndo mseto au Alu za serikali
Tatu ni kwamba wahindi nao wameingia baada ya kuona mseto unatumika,unapendwa na ni ghali,kwa hiyo wamekuja na zao za bei rahisi(ubora sina uhakika) zenye majina ya biashara..Artefan,lumaterm,lumerax tena zenye vidonge vichache mfano (dozi vidonge 6 badala ya 24)
Watu wananunua buku 1 mpaka 2000,zinawasaidia ila hazijatumika muda mrefu sijui madhara yake ya muda mrefu(long term effect)
2-Duocotecxin (dihydroartemesinin+piperaquine 40/320mg) inatoka china,ni nzuri zaidi ya 70% ya watu wanatumia bila shida ila kwa wale isiyowafaa ina madhara makubwa kama kushusha presha na hata kuua(rare) Tatizo lake ni kwamba ukitumia iliyokaa,tuseme zaidi ya miaka miwili hata kama tarehe ya expire haijafika haiponeshi na ndo maana wamebadili idadi ya vidonge(zamani vilikuwa 8 dozi 3/3/2 siku hizi 9 dozi 9/9/9 kwa wakubwa) vinginevyoo si mbaya lakini ni ghali >Tsh10000 brand
3-Artequine(artesunate+mefloquine 600/750 etc) ni nzuri kwa watu wasio na matatizo ya moyo,lakini inasumbua kwa watajwa tena inaweza kufanya hali ikawa mbaya sana. Bei ni ghali pia>Tsh11000 lakini kama utaweza kununua ni nzuri tu kama huwezi mseto(ya dozi vidonge 24)
4-Ntaendelea kesho pita pita,umeme umekatika na betri yangu chaji imeisha ntaendelea
 
nice info we gonna wait for other
 
Tuendelee kama nlivyo ahidi!!!
4:Artequick-bado inafanyiwa post marketing study(uchunguzi wa mwisho ikiwa sokoni)
-ni nzuri kwa dozi kwani ina vidonge 4 tu,unameza 2 kila siku kwa siku 2,ila ndo hivyo haijatumika muda mrefu kwa hiyo uzoefu bado ingawa
kwa wale walokwisha tumia hawajaripoti madhara yoyote
5:Arco
-ina fanana fanana na namba 4 hapo juu lakini tofauti yake ni idadi ya vidonge
Dozi yake ni vidonge 8 x 1 basi,lakin inatia shaka kwa ukimwambia mtu meza 8 x 1 anaweza fikiri unataka kumuua,hata hivyo bado watumiaji si wengi kwa hiyo sina data za kutosha
6:Arsumoon
-ni dawa nzuri yenye (artesunate+amodiaquine) lakini inawafaa watu wasiodhurika na amodiaquine kama wenye matatizo ya moyo
-dozi ni vidonge vingi kama mseto(alu) kwa hiyo si rafiki kwa waoga vidonge
-kuna wakati amodiaquine imewahi katazwa na WHO lakini naona bado tz inatumika

N:B kesho ntamalizia na dawa zisizo mseto kwa ajili ya maleria
FAHAMU KUWA DAWA KABLA HAZIJAANZA KUTUMIA ZINAPITIA HATUA MBALI MBALI ZA TAFITI KABLA YA KUUZWA KWA HIYO KILA DAWA ILIYOSAJILIWA NI HALALI KWA MATUMIZI
 
Zisizo mseto mkuu....
 
Back
Top Bottom