Ni hesabu tu.. Kuliko kutuma laki mbili kwa simu ndani ya Dar, mtume mwanao apeleke

Mna maoni gani masikini na wanyonge wenzangu?

Iparamasa,
Unaweza kuwa sawa kwa sehemu na siyo sawa.Kwanza inategemea unatumia mtandao gani lakini pili ujue kuna vibaka kila kona mpaka ndani ya Miendo kasi! Kwa kutaka kuokoa 5,000 unaweza jikuta hiyo 200,000/= ikaishia kwa vibaka! Tatu kuna kitu tunaita time management. Kuna maeneo hakuna mwendo kasi inabidi mtu apoteze muda mwingi ambao angeutumia kuzalisha 5,000 nyingine au hata hiyo 200,000/=!
Jambo la msingi hapa ni kupinga kwa nguvu zote hizi KODI za kijinga zinazo anzishwa na Serkali ya JPM kumnyonya Mtu wa chini huku Wawekezaji uchwara kwenye raslimali zetu wakiwa wamepewa TAXI HOLIDAYS ZA MIAKA 5/5 na ikiisha wanabadili jina la Kampuni kwa kisingizio kuwa hawapati Faida! Wanahamisha madini,wanyama hai na nyara zake kila siku na kukwepa kodi kila kukicha lakini Serikali ya CCM wanajifanya hawajui au hawaoni!!!
 
Hicho ulichoeleza una uhakika nacho? Jana nimetuma 260,000 sijaona hiki ulichoeleza
Mkuu kutuma Tsh.260000/=ada yake ni Tsh.850/= hiyo ni ada utakayokatwa wewe. Unayemtumia nae akitaka ku-withdraw(kutoa) atakatwa Tsh.42000/= hiyo ni tigo. Jumla itakuwa Tsh.5050/=.
 
Labda ufanye utafiti kwanza kabla ya kupost. Juzi nimetuma 505,000/- tigo-tigo ada 1,850. Leo nimetuma 850,000 tigo-voda ada 2,250. Kutuma gharama zake ni hizo sasa sijui hio 5000/- kutuma 200,000/- umeitoa wapi. Ninachoweza kukueleza kingine, kutoa pesa cash kwa wakala ziko juu kulikom kutuma.

Sasa kwa 1,850 ni afadhali nitume kwa njia hii kuliko kumpa mtu apande nayo daladala, labda hukuangalia risk ya kupanda daladala na kiasi kikubwa cha fedha.
Hujamuelewa mtoa mada..
Hiyo elfu 5 aliyoisema inajumlisha gharama za kutuma pamoja na kutoa yule ambaye unataka hela imfikie.
 
Ukiona matajiri wanakwepa kodi basi jua kuwa kodi ni adui wa utajiri na umaskini ni rafiki wa kodi that why Messi alivyokuwa maskini hakukwepa but aliyokuwa tajiri kaanza kukimbia kodi
 
Hujamuelewa mtoa mada..
Hiyo elfu 5 aliyoisema inajumlisha gharama za kutuma pamoja na kutoa yule ambaye unataka hela imfikie.
Sawa. Ila siwezi ku risk 500,000 kuokoa 3000/-. Na kama alivyosema hapa ni hesabu tu, nasikitika hesabu hio haileti maana. Huwezi kuhangaika na hela nyingi kwenye daladala kisa unaokoa 3000/-.
 
Nenda katume 505,000 tigo-tigo uje utuambie gharama za kutuma ni kiasi gani.

Anaweza akawa anamaanisha ile situation ambayo unatakiwa kumtumia mtu hela na makato yasimhusu

Mimi nimefanya hivyo 2 days ago, nimepeleka kodi ya mwaka kwa land lord wangu in cash badala ya kutuma kama ilivyozoeleka, baada ya kuona makato yatakuwa makubwa na nilikuwa na ishu zingine huko huko anakoishi.

Na faida nyingine nimepata namba ya binti yake mzuri balaa
 
Mimi nilikua nahifadhi ela zangu huko ila kwa sasa nalala nazo tu acha zipotelee kwangu sio kwa serikali isiyokua na msaada kwangu.
 
Anaweza akawa anamaanisha ile situation ambayo unatakiwa kumtumia mtu hela na makato yasimhusu

Mimi nimefanya hivyo 2 days ago, nimepeleka kodi ya mwaka kwa land lord wangu in cash badala ya kutuma kama ilivyozoeleka, baada ya kuona makato yatakuwa makubwa na nilikuwa na ishu zingine huko huko anakoishi.

Na faida nyingine nimepata namba ya binti yake mzuri balaa
Cash kama kodi ya mwaka nitaipeleka kwasababu makato yanalingana na bei ya mafuta! Ila siwezi kumtuma mtu apande nayo daladala ili nikokoe 5000/-.
 
Ni kweli gharama za kutuma fedha kwa njia ya simu zimekuwa ghali mno mnoo, na gharama zinapanda hovyo hovyo..!! TCRA wako wako tu..!!

Wizi wa wazi ni pale UNAPOULIZA SALIO, eti wanakata hela, hv mtu una hela yako tigopesa, mpesa, unaangalia salio, hela yako, wanakukata hela, HUU NI WIZI MKUBWA NA WAWAZI...!!
Huwa TCRA mm sijui kabisa kazi yao hapa nchini... wanalala sana.. haiwezekani mtu una kifedha chako ktk tigopesa, mpesa, kila ukicheki salio, wanakukata hela, HUU NI WIZI NA TCRA is part of it.. nailaumu sana sana TCRA, na kuwalaani kabisa..!!

Pili mfano TIGO, wahuni sana sana, wanakuunganisha na huduma wao, hata hujajiunga, ukiweka vocha wanakukata eti unatumia huduma fulani... Tigo ni wezi sana, wanakuunganisha na huduma hata hujui, kisha ukiweka vocha wana deduct daily, sometimes wanakuunganisha huduma hadi 2 na wakata hela ki wizi wizi tu.. TCRA wanajua na wako wako tu... Mm nawalaani sana TCRA..!! Tigo ndio wezi kabisa..!! utajitoa ktk huduma zao zote, weka vocha watakukata, watakwambia unatumia huduma fulani, na wanakuunganisha wao makusudi kabisa... TCRA nawapa laana kabisa..!!
HIVI KWANI HIYO MITANDAO MMEFUNGA NAYO NDOA? SI MHAMIE HATA TTCL JAMAN ALLAH!! TCRA WAPO KWA AJILI YA KUSIMAMIA WIZI LAKINI HAWAINGILI HUDUMA ZA KAMPUNI BINAFSI EBBOH, NYIE VIP! ANAEUMIA NA MAKATO AHAME TU! SOKO LIPO KIUSHINDANI ZAIDI
 
Huyu jamaa kapotosha sana,huwezi tuma laki mbili ukatwe alfu tano....huo ni urongo wa level ya juu.
 
Be serious ma friends sitetei haya makampuni ya simu nakubali kuwa ni expensive ki uhalisia lakini ukumbuke kama hiyo hela unataka kuituma mwanza, au nje ya wale ambao wapo Dar au Mbali na mkoa ulipo je utapanda daladala? Pia kumtuma m2 kuna mambo mawili anaweza kuja na stori kaibiwa, pia swala la muda atakaotumia naona hauhesabiki kabisa! Think out of the box,
 
Ikipotea hiyo hela njiani kwenye huo mwendokasii utamlaumu nani... Au ukiibiwa ...
 
Back
Top Bottom