Ni hatua zipi za kufuata ili kupata simu iliyoibiwa/kupotea?

chichiboy1

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
1,262
1,620
Habari za Jumamosi ya leo waungwana,

Tafadhali, kwa mwenye kufahamu hatua za kufuata ikiwa unataka kuipata simu iliyopotea kwa kutumia IMEI# naomba anifahamishe.

Hii ni baada ya kutoa taarifa Polisi.
 
Inatakiwa askari wenyewe waifuatilie tatizo itabidi utoboke mfuko. Nafikiri hii huduma ilitakiwa iwe wazi mno ili kuzuia uwezekano wa mtu kujikuta unatumia gharama kubwa mpaka kulingana na bei ya simu.

Baada ya kuwaachia imei wao huanza track ile imei kama kuna service provider anaihudumia ikatokea imeonekana hiyo imei kuna mtandao inautumia wao huwasiliana na mtandao husika watachukua namba ambayo inahusik na hiyo imei.

Hapa sasa wanaweza tumia mtego wa kumpigia mhusika na kuonyesha wanamjua na kutaka kukutana au la watajifunza pattern ya hiyo namba kwa kuangalia mahali anapokua mara nyingi na muda anaotumia.

Hivyo wataenda hilo eneo na kuipiga namba, atakayepokea atakamatwa. Hii ishu ya usajili wa alama ya vidole inazidi kurahisisha ukamataji.

Niliuliza inakuaje imei ikabadilishwa nikajibiwa hata imei ikibadilishwa polisi wakiamua kuipata simu ni inawezekana labda uitupe.
 
Back
Top Bottom