Hatua za kufuata unapofanya uhakiki wa Picha kwa kutumia TinEye

maxresdefault.jpg


TinEye ni nyenzo nzuri ya kutafuta picha kwenye wavuti ambayo inaweza kutumiwa kufanya uhakiki wa Picha.

JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha.

1. Fungua Kivinjari Chako
Anza kwa kufungua kivinjari chako kwenye kifaa chako cha mkononi au kompyuta.

2. Tembelea Tovuti ya TinEye
Ingiza 'TinEye' kwenye sanduku la utaftaji la kivinjari chako na bonyeza kwenye matokeo yanayofanana na tovuti rasmi ya TinEye.

3. Pakia Picha
Kuna njia mbili za kupakia picha kwenye tovuti ya TinEye
  • Bofya kwenye kitufe cha 'Pakia Picha' au "Upload' kisha pakia picha unayotaka kufanya uhakiki.
  • Ikiwa picha tayari iko kwenye wavuti, unaweza kunakili URL (Link) ya picha hiyo na kuibandika moja kwa moja kwenye sanduku la utaftaji la TinEye lililoandikwa 'Paste or Enter Image URL'
4. Bofya Kitufe cha Utafutaji
Baada ya kupakia picha husika, bonyeza kitufe cha 'Tafuta' au 'Start Searching' ili TinEye ianze kutafuta picha kama hiyo kwenye wavuti.

5. Angalia Matokeo
TinEye itakuonesha matokeo ya picha inayofanana kidogo au inayofanana kabisa na picha uliyopakia. Utaweza kuona tovuti ambazo zina picha hiyo na maelezo zaidi kuhusu picha hiyo.

6. Kagua Chanzo cha Asili
Kagua matokeo kwa makini ili kubaini chanzo cha asili cha picha au taarifa zaidi kuhusu picha hiyo. TinEye itakuonyesha tovuti ambazo zina picha husika, na unaweza kuchunguza zaidi ili kujua maelezo zaidi kuhusu picha hiyo.

7. Thibitisha na Tathmini
Baada ya kupata matokeo, tathmini taarifa ulizopata ili kubaini ikiwa picha ni ya kweli au la. Kulinganisha maelezo kutoka TinEye na vyanzo vingine itakusaidia kujenga uhakika.

Hitimisho
Baada ya kufuata hatua hizi, utakuwa umepata ufahamu zaidi kuhusu asili au maelezo ya picha hiyo. Kwa hiyo, utaweza kufanya tathmini inayofaa ya picha hiyo na kuamua ikiwa ni sahihi au la.

Kumbuka, TinEye ni chombo kingine muhimu kwa uhakiki wa picha, lakini pia ni muhimu kutumia vyanzo vingine na mbinu za uhakiki wa ziada kuthibitisha habari zaidi.

Pia soma
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom