Lyamber
JF-Expert Member
- Jul 24, 2012
- 11,716
- 18,753
Vitu ksma hivyo ilibidi ukodi magari yenye friji yaleDah! Imenihuzunisha aisee, pole mkuu.
Kwaupande wangu nilipoteza 1mil kwenye biashara ya mbogamboga(brucol, cauliflower, letuce). Nilikuwa na mshkaj wangu aliyekuwa napiga nae hizi mishe za kufungasha hizo mboga halafu tunatuma Dar kwa mama mmoja ambae alikuwa anatupa oda yaan anawatumia idadi ya kg za hizo mboga mnakata mnafunga mnatuma halafu mnatumiwa hela akiupokea mzigo.
Nashukuru biashara ilianza vizuri sana nakumbuka nilianza na mtaji wa laki 4 hiyo pesa nilitoa mimi huyo jamaa yangu alikuwa anafanya kazi ya kutafuta mboga kwa wakulima na kufunga kwakuwa mimi ni Mwl. na kazi yenyewe ilikuwa inafanyika siku za kazi . Basi tukapiga kazi kama miez 2 nilikuwa napata faida kuanzia elfu 35 mpk 50 kwa wiki kwakweli niliona hii kitu inalipa sana basi nikajichanga nikaongeza mtaji ukafika mil 1.
Nakumbuka tukafunga mzigo usafirishwe kwenda mjini dah ilikuwa kipindi cha mvua barabara ya kutoka Soni kwenda Mombo ikazingua kuna kifusi na mawe makubwa yakashuka aisee njia zikawa hazipitiki gari zikalala pale siku 2 na mboga zinatakiwa zifike mjini usiku au mapema sana sokoni, mboga zilioza pale na ndio ukawa mwisho wangu kwenye biashara, aisee niliumia sana kwasababu hela yenyewe ya kuongezea mtaji nilikopa kama laki 4 tena kwa riba.
Sent using Jamii Forums mobile app