Konda wa daladala aliniokoa kipindi nachapika na maisha

mkarimani feki

JF-Expert Member
Nov 8, 2023
302
1,136
Based on true story:

Nakumbuka graduation yangu na washkaji zangu ilikua na mvuto sana pale mlimani city hall mwaka 2017 ,niliona baada ya muda mfupi tu basi ningepata mchongo mzuri na ningevuta usafiri unaosomeka crowm new model within the year(s)

JK alitoa hamasa kwa vijana wakapambane na mtaa either kwa kujiajiri ama kuajiriwa.

Muda kidogo badae hakuna rangi niliacha kuona baada ya kuhitimu chuo demu wangu alisepa. ndugu na wajomba walioniahidi kazi wengi niliishia kuramba blueticks whatsapp na kejeli juu baada ya kuwasambazia CV.

Nilichapika na maisha balaa nusra kudata, maumivu makubwa ambayo yalikuwa yakinitesa moyoni mwangu ni kuwa ni lini nitawabeba wazazi wangu kutoka kwenye lindi la umasikini uliokithiri atleast milo miwili homu isiwe tabu tena.

Kuna siku nimetoka kutafuta kazi Vingunguti viwandani nikakuta foremeni anahitaji umtoe chochote kitu ili akuunganishe kazi! nikatoa 9k lakini bado nilikosa kazi siku ile, changamoto ikaja muda wa kurudi mageto kwa mshikaji nilikokua najiegesha nauli sina.

Oya wanangu, nikasogea sogea kwa mguu mpaka Buguruni kwa Bakhresa kituo cha daladala huku njaa ikinichapa kweli kweli nikamwita konda pembeni (konda nisaidie mwanetu japo buku ama uni link na daladala za mawasiliano sina nauli na ubao unapiga sana) jamaa ile kunitazama tu mwana akazama mfukoni na kuniachia buku mbili .

Nafika gheto sijakaa sawa napokea simu toka kwa mdogo angu aliyeko shule kuwa bro naumwa nimeletwa hospitalini na wanafunzi wenzangu malaria imenibana sana kama unasomeka nitumie 12k ambayo wenzangu wamenilipia kwani homu wazazi nao hawapatikani hewani licha ya jitihada kadhaa, aiseeh moyo wangu ulipoteza tumaini siku ile niliona kama kuna mkosi unanisaka mimi na familia yetu .

Nisiseme mengi wadau nikaja kupata ajira utawala huu wa Mama Samia kamwe siwezi sahau changamoto wanazopitia jobless
 
Pole sana mkuu, ndiyo maana tunaambiwa tuheshimu kila mtu na anachokifanya halali maana huwezi jua nani atakuja kukusaidia na wakati gani katika maisha...


Screenshot_20240303-151941.png
 
mtu akisema nanjaa naelewa pasipo ufafanunuzi wowote ,wakuu amini nawambieni watafutaji ambao hawana wakuwa shika mikono wanateseka sana huku mtaani
Niliwahi pia saidiwa na Konda 2015 Goms to Chanika Saa 2.00 usku. Sina hata mia. Nilimueleza shida yangu, jamaa akaniruhusu nipande akaniachia na siti kabisa. Tulifika nikamuomba Na. ya simu akasema haina haja!
 
Back
Top Bottom