Ushawahi kutana na mtu mnafahamiana, Ukajifanya Sio wewe(hamjuani)?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Juzi Nipo k.koo, nimebeba loba langu la mzigo wa kwenye kaofisi kangu, nikiwa napeleka sehemu flani hivi kwa ajili ya kufungasha nirudi, nikiwa napita maeneo ya Uhuru road kama unatokea china plaza, maeneo yale wanajaza ma fridge nje.

Ghafla Bin Vuu mbele kulee naona Pisi Flani nilikua nayo Chuo, mpaka mwaka na nusu baada ya kumaliza mawasiliano yaliendelea, imewaka balaaaa, Hakukua na njia nyingne zaidi ya Kuula wa Mbuzi...

Sikutikisikaa, Nikahisi hatanifahamu Ukizingatia watembeaji ni wengi, Lakini nikiamini nimebadilika, Sio ile smartness aliyokua akiniona nayo Chuo, Udevu umeota Haswa, pia nimeinama kdg sababu ya mzigo begani, Lakini waaapi, Kumcheki Ashaanza kama kunipa attention, mara anapunguza mwendo, Na ishara zote za kutaka kuni alert kwa kutambuana,

Sikuzubaa wala kuleta utofati hata kdg, Nikaunga, ile namkaribia nasikia "Heyyy" namkuta nasikia "Heloo", kuna jamaa akanishtua "Oya Pisi inakuita hio Mwana", nikamwambia sio mimi, Mwingne Akasema "Oya kageuka, daahhh.... we jamaa.....!!" ??

Kiufupi nilikua nimechafuka sana, Jasho kuanzia Asubuhi ni (kutafta mzigo, kununua, kubeba x 9)
Pili ule muda nimeshachoka mno, kusimama dk mbili na ule mzigo ni keroooo..
Tatu Nilitanguliza Teja na Guta wako resi Mnajua wale ukiacha Gap la mita 4 tuu ni manyoya..
Nne, sehemu niliyokua nafungashia walisha ni alert kua wanafunga hivyo ni wahi,

Kwahio ninge simama, achilia mbali tuu na nilivyokua, ila ningekua na haraka mno kitu ambacho nikahisi angeona ni kutojiamini, nimtoke kumbe nina mengine....

Baada ya kama lijisaa na nusu, napakia mzigo naona msg namba mpya "Heloo ......"
Nikajua ni mteja flani hivi, kucheki kwenye history naona ni namba ishawahi nicheki mda kdg mara 2 ila sikuwahi kuijibu, Hivyo nikajua sio huyo mteja..

Nikamjibu......, tukachati kdg hata sikuuliza nani...., aka mute, jioni akanitext tena mimi ........

Nikajisemea Eheeeeeeeeeeee...... Jini limekula mganga...

Nikajishangaza pale kinafiki, Sijamaliza kutuma ya Pili, akaenda hewani...

Upo wapi....?
Kwa ufupi nilimchomolea kama sio mimi...

Basi, nikamwambia Nikija Town weekend kama utakua huru nitakucheki..., Akasema "Anytime"

Maisha yanabadilika Sanaa, mda mwingine Life linakufanya ujiweke pembeni mwenyewe, hata kabla hujawekwa...., Ujitafute, halafu Urudi kwenye Square.
 
Juzi Nipo zangu k.koo, nimebeba loba langu la mzigo wa kwenye kaofisi kangu, nikiwa napeleka sehemu flani hivi kwa ajili ya kuunganisha Ili nichomoke, nikiwa napita maeneo ya Uhuru road kama unatokea china plaza, maeneo yale wajaza ma fridge nje.

Ghafla Bin Vuu mbele kulee naona Pisi Flani nilikua nayo Chuo, mpka mwaka na nusu baada ya kumaliza mawasiliano yaliendelea, imewaka balaaaa, Hakukua na njia nyingne zaidi ya Kuula wa Mbuzi...

Sikutikisikaa, ila nikahisi hatani note Ukizingatia watembeaji ni wengi, Lakini nikiamini nimebadilika, Sio ile smartness aliyokua akiniona nayo Chuo, Udevu umeota Haswa, nimeinama kdg sababu ya mzigo begani, Lakini waaapi, Kumcheki Ashaanza kama kunipa attention, mara anapunguza mwendo, Na ishara zote za kutaka kuni alert kwa kutambuana,

Sikutikisika wala kuleta utofati hata kdg, Nikaunga, ile namkaribia nasikia "Heyyy" namkuta nasikia "Heloo" kuna jamaa akanishtua "Oya Pisi inakuita hio Mwana", nikamwambia sio mimi, Mwingne Akasema "Oya kageuka, daahhh.... we jamaa.....!!" ??

Kiufupi nilikua nimechafuka sana, Jasho kuanzia Asubuhi ni (kutafta mzigo, nunua, beba x 9)
Pili ule muda nimeshachoka mno, kusimama dk mbili na ule mzigo ni keroooo..
Tatu Nilitanguliza Teja na Guta wako resi Mnajua wale ukiacha Gap la mita 4 tuu ni manyoya..
Nne, sehemu niliyokua nafungashia walisha ni alert kua wanafunga hivyo ni wahi,

Kwahio ninge simama, achilia mbali tuu na nilivyokua, ila ningekua na haraka mno kitu ambacho nikahisi angeona ni kutojiamini, nimtoke kumbe nina mengine....

Baada ya kama lijisaa na nusu, napakia mzigo naona msg namba mpya "Heloo ......"
Nikajua ni mteja flani hivi, kucheki kwenye history naona ni namba ishawahi nicheki mda kdg mara 2, ila sikuijibu Hivyo nikajua sio huyo mteja..

Nikamjibu......, tukachati kdg hata sikuuliza nani...., aka mute, jioni akanitext tena mimi ........

Nikajisemea Eheeeeeeeeeeee...... Jini limekula mganga...

Nikajishangaza pale kinafiki, Sijamaliza kutuma ya Pili, akaenda hewani...

Upo wapi....?
Kwa ufupi nilimchomolea kama sio mimi...

Basi, nikamwambia Nikija Town weekend kama utakua huru nitakucheki..., Akasema "Anytime"

Maisha yanabadilika Sanaa, mda mwingine Life linakufanya ujiweke pembeni mwenyewe, hata kabla hujawekwa...., Ujitafute, halafu Urudi kwenye Square.
nimekuelewa kabisa mkuu

Maisha yetu ndio yanatubadirisha roho zetu

Nimekuelewa sana tu
 
Brother flani hivi rafiki yangu, alisoma na dada flani hivi chuo, kuna siku tukaenda naye msibani, Kufika Akamuona Dada mmoja hivi simple sana anazongwa zongwa na mijama kila anapoenda, hata hakulipa hilo attention, yeye akawa tu anajiulizaa hii sura mbona sio ngenii?, baada ya kung'amua kwa mda mrefu, akakumbuka alisoma naye..

Akamuita "We dada Njoo hapa" akaenda mbele kidogo kusalimiana na mtu halafu akarudi...,

Akamuuliza unanikumbuka? Dada akasema hapana, Jamaa akamtajia watu kama watano waliokua maarufu darasani, mwisho akataja jina lake yeye mwenyewe sasa, Dada kwa sekunde kadhaa akamuangali vzr alishangaa sana kwa furaha, akasema haaaaa......(akataja jina la utani) walikua ma best sanaa, wakapiga stori sana, baadae wakabadilishana namba,

Jamaa kidogo akaanza kutupia kamba, Sista akawa hasomeki, hakuna Yes wala No, mda mwingi anadai amebanwa na majukumu...

Baada ya kama Week 2 hivi Jamaa anakuja kuambiwa kumbe Dada ni Mkuu wa Wilaya flani hivi kubwa..

Akafuta mpka namba kwa woga, Akawa yeye ndio anatafutwa, mwisho kuna inshu kubwa alimsaidia..

Kuna mda ukijiridhisha upo chini katika level flani, kua mpole Acha uchawa, Hujui Mhusika atakuchukuliaje, Ni wachache Sana wanavalue urafiki wanyuma regardless na Gap lenu la maisha mapya, na sio wote wanapenda Machawa, Jipange mwenyewe.
 
Uoga wake tu. Hasa aliogopa nini hapo. Uboya ndio huuu
 
Back
Top Bottom