Ni hasara gani kubwa ulishawahi kuipata ikakurudisha nyuma?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Ni wazi Katika harakati za maisha kuna pingamizi nyingi sana, kuna muda unapambana sana kutafuta kile unachokihitaji, unabahatika unakipata lakini kinapotea na kubakiza kama ambaye hajafanya chochote,

Yaweza iwe kwa kuibiwa, kutapeliwa, kudhulumiwa, kupoteza, kuharibika n.k n.k

Kwa kweli huwa inauma sana, tena sanaaa,
Sizungumzii kitu kikubwa, hapana nazungumzia kitu chochote ambacho ulikipambania kukipata lakini kikatoweka haraka/kirahisi.

Binafsi Wakati nipo chuo mwaka wa kwanza nilikuwa nahifadhi pesa yangu kwa kujibana sana, zaidi ya nusu ya hela yangu ya Boom(nilikua napata 100%) nilikuwa naitunza inisaidie nikishamaliza au popote nitakapo pata nafasi ya kuianzishia biashara,

Hela yangu yote ya kujikimu, field, special faculty na za vikazi kazi kipindi cha likizo nikawa nimefikisha 2.6M mpaka namaliza,

Wazo kubwa nililokuwa nalo baada ya kumaliza ni kufungua stationary Morogoro, kulikuwa na uhaba sana wa stationary, nikaona hii ni fursa na bahati nzuri nikapata eneo zuri kabisaa.

Basi ile nimehitimu tuu sikutaka kukaa kabisa nyumbani, nilienda tuu kuwasalimia wazee nikawaomba kuondoka baada ya week moja nikatafute maisha,

Kiukweli hawakukubali mwanzo, waliomba hata wakae na mimi kidogo maana kiukweli sijawahi kukaa nao kwa muda mrefu tangu nianze darasa la kwanza, ila baadae wakalazimika sababu ya kuwashawishi, sikuwaambia chochote kuhusu ile pesa na mpango mzima.

Nikiwa nimeandika mahitaji yangu yote, nikaenda mjini kwenye duka flani hivi pale mtaa wa uhuru, nikanunua kila kitu kihusianacho na stationary(niliuza simu yangu nikajazia na kwingne ile hela ikafika 3.0M) na baadhi ya accessories za simu nikafungasha mzigo wangu ile jioni nikaupeleka Kwenye haya malori ya Mizigo yanayoleta mizigo Dar na kurudi mikoani Usiku, mimi nikarudi zangu home.

Lengo mzigo usafiri ule usiku, kuna rafiki yangu aupokee asubuhi mimi niukute huko mchana, ile ndio ikawa kwa heri 3.0M yangu.

Kiufupi mpaka leo hii sijajua ule mzigo ulipotelea wapi, Dereva na konda wanadai waliufikisha kwa mpokeaji na akapokea, Mpokeaji(rafiki yangu) nikimuuliza anadai amesubiri ila hakupata mzigo.

Mpaka dakika za mwisho naongea na konda anasema mpokeaji huyu hapa ongea naye, nikaongea na Mshkaji kweli akasema anashushiwa mzigo, Baadae nampigia sasa yeye kwa simu yake akasema hajapokea mzigo wala hajaongea na mimi kupitia simu ile...

Hiyo ilikuwa asubuhi niko pale Ubungo na mimi ndio nataka nitoke,

Sitosahau ile siku....nilikaa chini bila kujijua,
Maumivu yale sitokuja kuyasahau, nilikaa pale chini kama nusu saa hivi,

Mdada mmoja msafiri aliona ile hali yangu ndio akaja kunisaidia,

Yule dada Alichelewesha safari yake kwa kunisaidia kunivusha barabara na kuhakikisha mpaka napanda daladala akaniomba namba, akamwambia konda huyu anashukia sehemu flani ni mgeni hapajui, ndio akaondoka, sidhani kama ile siku ningepita salama pale mataa,

Network ilipotea kabisa, kufika kituoni ndio konda akanishtua "shuka dogo ndio hapa" pasipo kujua nimekulia hapo ila pamegeuka pageni kwangu, narudi nyumbani wanashangaa, kila wanachouliza nipo kimya, sio kama sitaki kujibu ila hata kinywa hakifunguki, macho yanaonesha kbsa nazuia machozi, walielewa ile hali, wakaniambia nenda kalale,

Nilianza kwa kuwaomba sana msamaha wazee, nikawaelezea kisa changu, nikawaonesha risiti za manunuzi na za kusafirishia mzigo, waliumia sana Mwishowe wakanipa support...

Hasara zipo nyingi, lakini je ni ipi ilikuumiza zaidi na kuona kama imekurudisha sana nyuma na ni ngumu kurudi kwenye Hali ya kawaida.

Sio lazima iwe pesa,
Yaweza kuwa ulipoteza mda kwa kitu flani, Nguvu, Matuaini/Mtarajio makubwa yakabuma n.k n.k
SHARE
 
Dili langu la kwanza kupiga hela nyingi ilikuwa 3.6M taslimu, hapo sina akaunti benki nikaomba mshkaji wangu nipokelee kwake.... pesa imeingia nilichoambulia ni 600k kodi ya nyumba.

Ile 3M nilipanga itulie kwanza iive [mature], huku nikiweka sawa mipango kazi... kilichofuata hapo ni maumivu tu.

Hadi leo bado nadai na mchizi akituma laki kwa mwezi amejitahidi sana, mwaka wa 3 huu.

Japo mchizi anaelekea kumaliza deni, ila sikumbuki nilichoifanyia 3M yangu zaidi ya kulipia vifurushi tu na luku.
 
Mimi nilijibana hela ya boom nilipomaliza chuo nikawa na vihela bahati nzuri nilivyomaliza tu nikapata sehemu ya kujitolea nalipwa kidogo, basi bwana nikaanza tubiashara cha nguo za ndani za wadada nilianza na mtaji wa elfu 70 sikutaka kuwekeza hela zaidi mtaji hadi ukafika laki 3.

Mara paap sister angu alikopa mkopo bank akashindwa kurudisha kwa wakati nyumba yake ikataka kuuzwa na bank ikabidi tukae kikao kama familia tumuokoe ndugu yetu nikatoa pesa yoote baasi na biashara ikaishia hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilimo cha kitunguu kwa simu nilikubaliana na mtu wa shamba i can pay each and everthing then mwisho mapato 50/50 lengo lilikuwa kumuwezesha hakujali kenge yule yeye shamba anaagiza watu kama navyomwagiza hela za matunzo ya shamba anapiga gambe siku nafika kukagua doh mwisho mtaji wangu wa kwanza wote ulipotelea huko sikupata kitu kabisa
 
Dili langu la kwanza kupiga hela nyingi ilikuwa 3.6M taslimu, hapo sina akaunti benki nikaomba mshkaji wangu nipokelee kwake.... pesa imeingia nilichoambulia ni 600k kodi ya nyumba.

Ile 3M nilipanga utulie kwanza iive [mature], huku nikiweka sawa mipango kazi... kilichofuata hapo ni maumivu tu.

Hadi leo bado nadai na mchizi akituma laki kwa mwezi amejitahidi sana, mwaka wa 3 huu.

Japo mchizi anaelekea kumaliza deni, ila sikumbuki nilichoifanyia 3M yangu zaidi ya kulipia vifurushi tu luku.
Kufungua akaunti mbona fasta tu, ulifeli wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom