OllaChuga Oc
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 21,125
- 24,060
Una umri gani mkuu ..ili nikupe namba ya kufanya usipoteze tena.Mimi nadhani nimeshakuwa sugu,nimepoteza mno kiasi kwamba imeshakuwa naona ni kawaida,siumii wala sishtuki ila wanaonizunguja wanaumia Hadi nawaonea huruma,,,mwezi wa tano pekee nimepoteza Mali ya zaidi ya million Saba,mwaka Jana sio chini ya million 70,komesha ni 2016...Duka la zaidi ya million 120 lilitafunwa na dogo niliyemuokota na kumfanya mdog o wangu,niliingizwa mjini na mtu was karibu million 70,nilipata hasara ya mifugo kufa zaidi ya 56m, nilibaki na madeni ambayo Hadi leo yananinyima Raha,2000 nilitapeliwa na mtu wa karibu 8m...mikasa ni mingi mno,ila namshukuru Mungu bado napigana,leo hii Niko naanza upya naamini sijachelewa bado....
Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app