Ni halali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni halali kwa mbunge kuongea na simu bungeni huku kikao kikiendelea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ptz, Jun 18, 2012.

 1. P

  Ptz JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana vikao vya bunge letu la Tanzania live kwa kupitia tv.

  Nimeshuhudia baadhi ya wabunge na mawaziri wakiongea na simu bungeni huku kikao cha bunge likiendelea, ni mara kadhaa nimemshuhudia Mkuchika akiongea na simu na gazeti la mwanachi lilishamtoa kwenye front page picha yake huku akiongea na simu.

  Leo hii pia, nimemshudia David Kafulia (mbunge Kigoma Kusini) akiongea na simu huku mzee Cheyo akitoa mchango wake, zaidi ya yote punde baada ya mzee Cheyo (Mbunge wa Bariadi) kumalizia mchango wake, kuna Mbunge wa Mbalali, Mh Kilufi akichangia kuna mbunge mmoja alikuwa kaketi kushoto kwake ghafla msg iliingia kwenye simu yake, niliisikia msg kwa ringtone ya Nokia, mbunge huyo alichukua simu na kuisoma msg na mara tu baada ya kusoma alionesha tabasamu zito (Source TBC leo saa 11 hadi moja jioni).

  Kwangu mimi nauita upumbavu. Nimekuwa pia nikifuatilia bunge la Kenya na Uganda, sijawahiona upumbavu huu.

  Ni bunge hili hili kuna mbunge mmoja alishathubutu kughushi hati na saini ya waziri mkuu Mizengo Pinda na kuachwa bila hatua yoyote ile.

  Je, ni halali kwa tabia kufanywa na hawa watu tunawaita waheshimiwa kuzitumia simu zao wakati wa kikao kikiendelea katika jengo tunaloliita tukufu kwani hata huku uraiani kuna vikao tumekuwa tukivifanya ni kulazimika kuzizima au kutoingia na simu kabisa?

  Kkwa mifano ya mabunge ya wenzetu niliyoitaja mfano bunge la Kenya naona kwa Yule spika "sir Kenneth Marende", naibu wake "sir Farah Macalin" upumbavu ninaouona huu kwa bunge letu Tanzania si rahisi kuuvumilia kwa bunge la Kenya, nilishashudia waziri akitolewa nje na kupigwa Ban ya vikao vitatu kwa kutojibu swali ipasavyo kwa ushahidi nilionao Bunge la Kenya ni Bunge la Kenya kweli "It's a really Kenyans Parliament" ni vigumu kumjua hata mpinzani au mtawala ni ninani!

  Nawasilisha.
   
 2. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Hata kusinzia kwenye bunge inatokea tz tu,makinda bunge limemshinda na utashudia vioja vingi
   
 3. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,601
  Likes Received: 16,559
  Trophy Points: 280
  Wako kwa ajili ya POSHO zaidi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:thinking:
   
 4. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni afadhali kusikiliza simu bungeni kuliko kulala (kusinzia) mjengoni.
   
 5. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,637
  Likes Received: 2,064
  Trophy Points: 280
  Ndio maana bunge letu linaongoza kwa kupitisha matumizi makubwa ya fedha bila kuangalia namna ya kuongeza vyanzo vya fedha, mfano mzuri budget ni sawa na Rwanda (sasa hapa tulinganishe idadi yetu na Rwanda jibu hapo unadhani ni nani ataendelea?). Angalia budget yetu na ya Kenya, wao budget kubwa zaidi yetu kwa trioni 10. Sasa angalia seating arrangement ya Bunge ilivyo wenye budget kubwa ukumbi wao wa bunge ni simple ukija kwetu ukumbi full kujiachia kwa mtu anaeangalia TV anaweza sema Tanzania na nchi jirani sie ndio tunaongoza kumbe wapi
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo inaonyesha udhaifu wa SPIKA; Niliongelea Juu ya Jinsi Chief Adam Sapi Mkwawa alivyokuwa Mkali na Mgumu

  Na Mfuataji wa Kanunu za Bunge, baadhi ya wana Jamii wakasema sababu ilikuwa ni Chama Kimoja...
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sio tu bungeni bali sehemu yoyote ya kazi sio vizuri kuongea kwenye simu sehemu ya kazi unless hiyo simu inahusiana na mambo ya kazi..sehemu nyingi tu hapa mjini ukiingia sehemu za kazi unakuta mfanya kazi anaongea na simu huku wateja wamepanga foleni wanasubiri huduma...bt ndio hivyo ndio bongo yenyewe inabidi tukubaliane nayo
   
 8. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Hakuna nafuu, uzembe ni uzembe tu!
   
 9. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii ni zamu ya bibi kiroboto kwa hiyo mambo mengi yamemshinda
   
 10. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  nidhamu inatuangusha
   
 11. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  hakuna tabia nisiyopenda kama mtu kupokea simu wakati anafanya shughuli nyingine,bunge ni chombo cha kutunga sheria,ni muhimili muhimu wa nchi,ndipo watz wote wanawakilishiwa mawazo yao,bunge letu halina nidhamu,wabunge wetu ni kama genge au mkusanyiko wa wacheza bao,hawajali pesa yetu inayopotea kuwalisha wao.mtu anapata wapi courage kuzungumza kwa simu bungeni ni ulimbukeni,ni ulevi wa madaraka,ni ufinyo wa kutotambua wajibu,tuna wabunge wa ajabu sana tz.bt nadhani wakati utafika tutapata uongozi usiotaka masihara kwakuwa nasi wananchi twaona na twajifunza sehem mbalimbali pia.ila ni tabia mbaya sana kwa wabunge kufanya mawasiliano binafsi bungeni.
   
 12. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamuulize Makinda atakupa kifungu cha sheria kinachoruhusu maana hakosagi vifungu vyakutetea.
   
 13. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,396
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Unashangaa kusikiliza simu? Mbona kuna wengine huwa wanaonekana wakitafuna jojo kama kocha wa Manchester United?
   
 14. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,087
  Trophy Points: 280

  Hakuna cha afadhali hapo, yote ni kinyume na maadili.
   
 15. U

  Udaa JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 727
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bora ya kupokea sim mjengoni na kulala,kuliko kupitisha sheria za kikoloni,na kupigia debe bajeti ya kukandamiza wanchi.
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Kwa bunge la Silly Season;
  • Kupiga simu ruksa wakati bunge linaendelea
  • Kulala bungeni ruksa wakati bunge linaendelea
  • Kutukana ruksa wakati bunge linaendelea
  • Kuzomea ruksa wakati linaendelea
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
 18. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Arabianfalcon na Wana JF,
  Kosa ni kosa, hakuna kubwa wala dogo, Dhambi ni Dhambi.
  Usiwafariji, hata kwa kusikiliza msg wakati Mbunge anatoa au kuchangia Mada etc ni Kosa, hata kwenye Maadili ya Bunge hakuna kitu kama hicho, kuruhusiwa kusoma msg kwenye simu au kuongea kwenye simu.
  Kibaya tunaambiwa alitabasamu, hatujui msg ilimfurahishije.
  Nawakilisha

   
 19. M

  Mta pter Member

  #19
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sa kama mbunge anaamua kupiga usingz,atashindwaje kupokea simu? Kwanza wabunge wengi,esp.wa Ccm,hawanaga time ya kusikiliza michango,labda tu kama unausu Posho! Apo wanak uwa active ile mbaya! Then uyu mama hawaoni? Au kawekwa pale kuwaona akina mnyika tu?
   
 20. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni mbunge dhaifu.
   
Loading...