Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Ni Tanzania pekee duniani fedha za walipa kodi hazilengi kumsaidia
mlipa kodi bali wachache. Vivyo hivyo walipa kodi wa Tanzania ndio
walipa kodi pekee duniani hawahoji hela zao zimetumika vipi kwa maslahi yao.

Tupe source na tafiti ipi ilifanyika kuthibitisha hayo usemayo ???? isije kuwa ni kauli za uchochezi
 
Wana Jf,
Ninaomba mnisaidie ufafanuzi. Nimesoma kwenye magazeti leo mwananchi.co.tz nikaona kuwa CCM inafanya mchujo wa wagombea umeya katika kikao kitakachofanyika DSM leo.

Nanukuu..... "Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba, jana aliliambia gazeti hili kwamba CC itakutana Ikulu chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kwa ajili ya kupitisha majina yasiyopungua matatu kupeleka kikao cha chama cha madiwani"

Kwa vile mimi najua iKULU ni mali ya serekali(wananchi walipakodi), je ni sahihi kikao cha chama kufanyika humo na kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya matakwa ya chama chao?"

nawakilisha!

Hiyo mbona haina shida kabisa ni haki yao kabisa kuitumia ikulu
 
Ni kinyume cha utawala bora kutumia rasilimali za nchi kwa maswala binafsi. Chama kinapewa ruzuku ambazo zinatokana na kodi za wananchi. Hivyo masuala ya chama yanapaswa kugharamiwa na chama husika kwa kutumia rasilimali za chama hicho. Kabla ya uchaguzi kamati kuu ya ccm ilikutana ikulu, na mara kadhaa wamekuwa wakifanya hivyo. Kama ikulu ipo kibiashara basi walipie gharama za kukodi ukumbi na za kuendesha vikao vyao. Kinyume cha hapo, kuendesha vikao vya chama ikulu ni uporaji wa rasilimali za nchi.
 
Binafsi naona ni bora mkutano huo ufanyike hapo Ikulu kwa sababu ya gharama ya muda na fedha za walipa kodi.

Mosi, jamani wengi wetu tunafahamu miundombinu ya DSM ilivyo, Rais JK akitoka Ikulu kwenda kwenye mkutano say Kempinsk ama Movenpick au hata pale Lumumba kwenye ofisi za CCM basi City center kutakuwa na foleni ya ajabu. Tukumbuke Mkuu kabla hata hajaenda 'kuoga' tayari traffic police wetu wanakuwa wameanza kuzuia magari. Hapo hujaongelea msafara wa Waziri Mkuu ambaye naye ni mjumbe kwenye kikao hicho.

Pili, Misafara ya Rais na WM inaambatana na magari yasiyopungua 14 kiujumla bila kuhesabu Ambulance (Paramedic Van) inayofuatana na mkuu popote atakapoenda. Hii yote ni gharama kama vile mafuta ya magari, posho za madereva n.k.

Kwa hiyo naona ni bora wafanyie mkutano wao wa CCM Ikulu kuliko kuanza kurandaranda mtaani.

By the way mbona hata Birthday parties za 'miungu watu' waliokaribu na Mkuu wanafanyia pale Ikulu!!
 
Kwa CCM kitu kinaitwa maadili kilikufa na mwanzilishi wake Kambarage!
Siku hizi tutachora chini!

Siku hizi katibu wa chama ni kiongozi wa serikali! CDM walisema wako tayari kuzungumza na serikali; Makamba akajibu CCM hawana muda kukaa na CDM. so Serikali=CCM. Unaona hata rais anaweza kufanya ziara ya kiserikali ndani ya Sare za CCM.

Nasikia Chenge ni mwenyekiti wa maadili, wakati yeye mwenyewe ni mtuhumiwa!

Usishangae hata watendaji wakuu wa Idara, Mikoa, n.k wanateuliwa kwa vile ni wana CCM. This is not fair. It must be distinguished: kazi za serikali na watumishi wake wajulikane! Sio kuwa na Waziri mbunge! Katiba yetu imepitwa na wakati! Tunataka katiba mpya
 
Wana Jf,
Ninaomba mnisaidie ufafanuzi. Nimesoma kwenye magazeti leo mwananchi.co.tz nikaona kuwa CCM inafanya mchujo wa wagombea umeya katika kikao kitakachofanyika DSM leo.

Nanukuu..... "Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba, jana aliliambia gazeti hili kwamba CC itakutana Ikulu chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kwa ajili ya kupitisha majina yasiyopungua matatu kupeleka kikao cha chama cha madiwani"

Kwa vile mimi najua iKULU ni mali ya serekali(wananchi walipakodi), je ni sahihi kikao cha chama kufanyika humo na kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya matakwa ya chama chao?"

nawakilisha!

Jibu sahihi: SIYO SAWA KUITUMIA IKULU KUFANYA VIKAO VYA CHAMA.

KWANINI: Kwasababu rasilimali za nchi zinatumika isivyo, hapa tunaongelea kulipa bill za umeme kwenye kumbi, kulipa wahudu na wafanyakazi wote wa umma watakao fanikisha mkutano huo, kuchakaza fanicha za ikulu n.k. Najua hapa watu watatwambia yale yale ya kulipia ndege za serikali lakini maelezo mazuri juu ya hayo malipo hayatolewi! Kwa wale wanodhani ni sawa basi wafikirie itakuwaje kama kesho kutwa Lipumba akiitisha mkutano wa CUF na kusema ufanyikie ikulu. Matumizi mabaya ya madaraka ni mapana sana!

 
Ili kupata jibu sahihi la uhalali wa vikao vya chama kufanyika Ikulu inabidi kuangalia sheria zetu. Kama sheria iko kimya kuhusu jambo hili basi jibu ni jepesi kwamba ni sawa kwa vikao kufanyika Ikulu na kama kuna hoja mpya inayoona jambo hili sio la kimaadili ni jambo lingine tofauti.

Mjadala hapa utakuwa tutunge sheria vikao vya chama visifanyike Ikulu
 
hili halinishangazi,kama waendesha bike wanaodai kutoka geita wanakaribishwa ikulu kirahisi bila story zao kuhakikiwa vizuri na wahusika why not fanya vikao vyao binafsi hapo....kweli utakatifu wa ikulu aliouongelea nyerere na kwa walio waroho wa madaraka kupaona kama paa haupo tena bali now nahisi wanajua inside and outside yake...du hamkawii kusikia jk anasema ikulu ni pake na kuanza muvuzisha mali kama watoto wake(masha,monica)walivyofanya
 
QUOTE=Brooklyn:magari yasiyopungua 14 kiujumla bila kuhesabu Ambulance (Paramedic Van)

Bila kusahau defender 2 za FFU. Moja mbele nyingine nyuma.
 
Brooklyn,mbona akili yako ni mavi namna hiyo?mada hapa si gharama,tunaangalia kanuni na sheria(utawala bora)!!je ni halali ikulu ifanye kikao cha wana-ccm?wakati JK yuko pale si wa CCM tu bali ni wa wote!!?!!
 
Tatizo la viongozi wanajifanya kutofahamu tofauti baina ya rasilimali za chama, dola na serikali (party, state and government).

Ndio maana utaona wanatumia mali za dola kwenye shughuli za chama. Au mali za serikali kwenye shughuli za chama. Na baya zaidi hata sisi raia hatujui tofauti ya vyombo hivyo 3.

Ndo maana wakati wa kampeni kuna watu walikua wakisema CHADEMA wataendeshaje dola wakati hata chama hakina pesa za kuwa na matawi nchi nzima? Hawaelewi tofauti ya mali za dola na chama. Sasa hali hiyo inatoa mwanya kwa CCM kutumia mali za dola na serikali kwa manufaa ya chama.

Elimu ya uraia ndio suluhisho.
 
Jibu la wazi ni kwamba siyo sahihi vikao vya chama kufanyika Ikulu. Hivyo vyama vya upinzani havina budi vilalamikie jambo hilo kwa Msajiri wa vyama.
 
ni kweli....

wakati mwingine huwa najiuliza hivi huyu mkwere ni chaguo la mungu yupi kutuletea mtu mzembe namna hii????????????

Mungu yupi? labda wa mnajimu shk Yahya.Ila Mungu wa Ibrahim/Allah hawezi kutuletea kituko cha namna hii hata kidogo
 
Serikali iliyopo inaongozwa na sera za CCM. Rais ni ametoka CCM ambapo Rais huyo wa CCM ndiyo kamteua Jaji mkuu. Spika ni wa CCM. Rejea ile mihiili ile mitatu utajua nafasi ya CCM. Katiba yako iliyopo haimuwekei mipaka ya rais aliyepo amwarike nani akiwa Ikulu!, awe ni mchezaji mpira, miss Tz, msanii au mpanda baiskeli Ruksa! Msimbanie
 
ccccm.JPG


ccccm1.JPG

JK Aongoza Kamati Kuu Ikulu Leo February 27, 2012
 
Back
Top Bottom