Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kitia, May 4, 2009.

 1. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Naomba kufahamishwa na wale wenye kufahamu zaidi, hivi ni sawa vikao vya CCM kufanyika Ikulu? Ninavyotambua Ikulu huwasikilisha serikali ikiwa ni pamoja na jamii nzima ya Tanzania.

  Hivi CUF, TLP au Chadema wanaweza kufanyia mikutano yao Ikulu au katika sehemu zingine kama hizo?
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Duh labda walikodisha ukumbi, si unajua tena mambo siku hizi mwendo wa mabusiness, si unaukumbuka ukumbi wa Bunge wa zamani Dar, twala pilau, twacheza muziki na kufanyia mazishi na send off mpaka harusi.
   
 3. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hii sio sahihi kabisa. Lakini hainishangazi kwa huyu mkulu 'JK' chochote kinaweza fanyikia ikulu
   
 4. C

  Chief JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani hamna tatizo vikao kufanyika Ikulu. Kwani Ikuku si makazi binafsi vile vile ya JK? sasa kuna kosa gani kuwaalika watu nyumbani kwake wakafanya mkutano kwenye sitting room yake?
   
 5. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sio mzima wewe...ikulu sio nyumbani kwa kikwete..Ikulu ni nyumbani kwa raisi wa Tanzania.
  Mada ya mwakyembe watu kama nyie ndo mlidandia conflict of interest bila kuelewa na hii ya kutenganisha serikali na ccm inawatoa jasho!!
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, kwa ridhaa yenu wana/wenye nchi imeiweka madarakani kwa zaidi ya miaka 45 huku mkiipa mamlaka ya kutumia rasilimali zenu bila usimamizi wenu. Hili la ikulu sidhani kama ni la msingi sana labda mwenzetu una personal issue hapo ila wizi unaofanywa na CCM ni mkubwa mara million sabini ya kufanyaia kikao ikulu...nimejaribu kuwa mkali kidogo ilkujibu uhalali wa swali lako?
   
 7. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu, naomba nikiwa nikufahamishe kuwa sina personal issue na mtu yeyote, na uandishi wangu hautawaliwi na hizo. Kama umesoma vizuri nimeuliza swali la kimsingi kuhusu kufanyia vikao vya chama tawala ikulu. Nakumbuka kuanzia enzi za TANU (ndiyo, nakumbuka vizuri sana) vikao vya chama vilifanyika katika ofisi za chama, hata wakati wa Chama kiliposhika hatamu, ndio kwanza makao makuu ya CCM Lumumba street, yakapata hadhi zaidi. Je kumekuwa na mabadiliko rasmi mapya yaliyotokea ambapo chama tawala kimeshika hatamu tena
   
 8. Sufa

  Sufa Member

  #8
  May 4, 2009
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Pamoja na mabadiliko ya katiba ya mwaka 1992 na kuruhusu vyama vingi, inaonekana ni kwenye karatasi kwani CCM hawaoni tofauti kati ya chama na serikali hata kidogo.
   
 9. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Sawa mkuu nimekusoma, ila tafadhari ni fahamishe je kuna madhara yeyote au ni athari zipi anaweza kuzipata mwananchi wa kawaida kwa vikao vya CCM kufanyika ikulu? na je ni wakati gani rais wa jamhuri ya muungano anakuwa ni mwenyekiti wa CCM taifa na kama inawezekana kuvitofautisha hivi vyeo hasa unapokuwa na serikali iliyo chini ya CCM?
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ah nilioona ile picha kuwa mkutano ikulu nilistaajab ila kilichonipigisha butwaa ni kwamba kuna memba mmoja wa CC nilimuona mule ndani ilhali ktk kikao cha kabinet hakuhudhuria..... dah duh!
   
 11. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  CCM ndio chama tawala, sasa kufanyia vikao vya chama IKULU sioni kama kunatatizo. kwani kuna matatizo gani kwa wadanganyika kwa kufanyia vikao hapo IKULU??

  Kinachotakiwa ni kuing'oa CCM madarakani ili mambo yawekwe sawa.
   
 12. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #12
  May 4, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hata mimi sioni tatizo, Wao ndio chama twawala bwana, nimemuona kama Ben yupo vile baada ya msekwa kushoto kuna mwenye mvi then anafuata mtu kama BEN.
   
 13. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Labda mkulu anaogopa kuongeza foleni zisizo za lazima jijini Dar kutoka ikulu kwenda lumumba. Experience zinaonyesha kuwa kila mara msafara wa raisi huchelewesha shughuli za watu kwa takriban masaa matatu.
  Je watu wa jijini mnge furahi rais awasababishie msongamano wa magari barabarani kisa ana vikao vya chama visivyokwisha lumumba?
   
 14. tHe NapSTer of Tz

  tHe NapSTer of Tz Member

  #14
  May 4, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanini asifanye vikao ikulu?.... 2memchagua raisi na chama chake!... na ikulu ni ofisi ya Raisi! hataki kwenda mbali na ofisi yake jamani!...
   
 15. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Unadhani????? Hivi ndugu zangu tutaishi kwenye zama za kudhani hadi lini? Je hatuna kanuni zinazotuongoza katika hili na masuala mengine kati ya vyama vya siasa na serikali....?

  Hawa Jamaa wa Deep Green walishajimiulikisha kabisa hii nchi kama vile walivyoamua kujimilikisha Viwanja vya mipira huko mikoani
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ikulu ni makazi binafsi ya JK? Tangu lini?

  Akiamua kuiuza anaweza? Akiamua kuivunja tu anaweza?

  Acha mambo haya bwana. Sio tu ni vibaya Kikwete kuendesha vikao vya CCM Ikulu, rais hatakiwi kuwa mwenyekiti wa chama, there arises a conflict of interest hapo, kuna information nyingine ambazo rais anakuwa privy nazo ambazo hazina best interest ya CCM, katika situation hiyo rais atafanya kazi katika capacity gani, kama rais au mwenyekiti wa CCM?
   
 17. C

  Chief JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Binafsi in the sense kwamba anaishi pale rasmi kama makazi yake. Si kwamba ana ownership kwamba anaweza kubomoa. Ni sawa na wewe kama unapewa nyumba ya kuishi na mwajiri wako. Unaweza kuitumia kwa matumizi yako binafsi. Naye anaweza kuitumia, kama kumtoa mwali, vikao vya arusi ya mtoto wake, na hivyo vya CCM, n.k. Si anaishi hapo kama makazi yake? Sasa akipata wageni wake binafsi kama wakwe anawapeleka wapi?? Labda issue ingekuwa mkutano huo unafanyika ofisini hapo Ikulu au kwenye Living room yake? Sijui Ikulu imetenganishwa vipi kati ya Office wing and residence wing.

  Suala la yeye kuwa M'kiti wa CCM na Raisi vile vile nadhani ni issue tofauti na hii tunayoongelea
   
 18. Ayayoru

  Ayayoru Senior Member

  #18
  May 5, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hilo ni tatizo
   
 19. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Liseme ni tatizo gani? mnaweza kuwa na point ila mnavyo jizungusha ndio mnapo haribu. Ni hatari zipi au athari zipi tunaweza kuzipata sisi wananchi wa kawaida kwa vikao vya CCM kufanyika ikulu? Hata harusi ya ridhiwan ilifanyika kwenye viwanja vya ikulu mzee.
   
 20. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ikulu niya serikali na Chama ni cha watz wachache hivyo kufanya vikao ikulu si sawa. Kwani pale ni pa watz wote hivyo mambo ya chama si pahala pake.

  That's why even TBC wanatumia kutangaza shughuli za chama as if ni ya CCM. Hivyo lazima kuwe na mipaka na kama itakuwa ngumu then itabidi sheria za nchi zibadilishwe ili kuondoa migongano maana hapo kuna mgongano wa maslahi.

  Unadhani rais atakichukulia hataua chama anachokiongoza wakati yeye ni mwenyekiti wake? Lazima hivi vitu vitenganishwe.
   
Loading...