Ni haki wanachuo wa ualimu kulipwa sh.500/= kwa siku?

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,445
Inauma sana na kusikitisha tr.20 March 2008. Wanachuo wa chuo cha Ualimu Morogoro [MOTCO] maarufu kama Kigurunyembe walitaka kufanya mgomo wakigomea fedha za mafunzo ya vitendo {BTP} kuwa ni kiduchu serikali hutoa sh.15000/= kwa mwezi kwa mchanganuo huo kila siku mwanachuo analipwa sh.500/= haijalishi umepangiwa Dar es salaam au Mbeya au Iringa pesa ndo hiyo hiyo. Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kalembo alienda kuokoa jahazi lakini swala la kulipwa 500 kwa siku alishindwa kulitatua zaidi ya ahadi hewa kibao.
Je hii ni haki?Kweli kwa hali hii unamjengea mazingira gani mwalimu mtarajiwa?Kwa vile ni mwalimu basi hana haki ya kupewa fedha za BTP?Serikali yetu imelifumbia macho kabisa swala hili kwani ni la muda mrefu na vyuo vyote nchini vinalipwa fedha hiyo.
Kwa mtindo huu tunasafari ndefu sana tusipo badilisha safu za kuongozi katika safu za juu basi tutaendelea kudumaa na nidhamu za woga.
Naomba msaada wadau wa elimu.Serikali inatenda haki hapo?

Mayombo.jpg
Huyu ni Mkuu wa Chuo cha Ualimu Morogoro bwana Ngonyani maarufu kama Mayombo.

wanafunzi wakipeleka  viti kusikiliza kikao cha dharula.jpg
Wanachuo wakiingiza viti kwenye ukumbi baada ya kuitishwa kikao cha dharura na mkuu wa Mkoa Said Kelembo.

choka mbaya.jpg
Wanachuo wakiwa wamechoka na kukata tamaa na hii fani.
 
500 kwa siku ni pesa ndogo sana! mtu utanunulie nini hii pesa??

Mie nilidhani ni 5,000

Waalimu Tz basi wanapata shida sana tangu wakati wa mafunzo hadi wanapoajiriwa na kupata mshahara kidogo!
 
hiyo imetulia 500..halafu tunataka kuendeleza elimu tanzania na wakati wakufunzi tunawapa 500.wakufunzi ni watu muhimu sana katika jamii yetu na wanatakiwa kuheshimiwa sana na serikali na jamii kwa ujumla na kama tusipowajali basi hatujali future ya taifa letu.wanatakiwa kupewa kipaumbele kifedha na kila kitu for the better future of our kids!!!!!!!!!
 
Hapa serikali inafanya mauaji kabisa,huyu mtu anahitaji kulipa nyumba,kusafiri na kula ,na hapo cjaweka matumizi ya kila clu. Huu ni uwaji wa hadharani kwa waalimu wetu. Unajua mimi huwa c elewi maana kila kiongozi nchi hii kaanzia msingi ,lakn hamna wanachokifanya kwa kuwajali waalimu hawa.
 
wanachuo wa U-ALIMU wanalipwa 500 per day....! je wanachuo wengine hulipwaje?
JE SI MARA KUMI ZAIDI....!?
 
....ualimu ni wito sote tumeitikiaaaaaa.!
ni baadhi ya maneno yaliyopo katika wimbo wa chuo kimojawapo cha ualimu hapa nchini....!
 
Inauma sana na kusikitisha tr.20 March 2008. Wanachuo wa chuo cha Ualimu Morogoro [MOTCO] maarufu kama Kigurunyembe walitaka kufanya mgomo wakigomea fedha za mafunzo ya vitendo {BTP} kuwa ni kiduchu serikali hutoa sh.15000/= kwa mwezi kwa mchanganuo huo kila siku mwanachuo analipwa sh.500/= haijalishi umepangiwa Dar es salaam au Mbeya au Iringa pesa ndo hiyo hiyo. Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kalembo alienda kuokoa jahazi lakini swala la kulipwa 500 kwa siku alishindwa kulitatua zaidi ya ahadi hewa kibao.
Je hii ni haki?Kweli kwa hali hii unamjengea mazingira gani mwalimu mtarajiwa?Kwa vile ni mwalimu basi hana haki ya kupewa fedha za BTP?Serikali yetu imelifumbia macho kabisa swala hili kwani ni la muda mrefu na vyuo vyote nchini vinalipwa fedha hiyo.
Kwa mtindo huu tunasafari ndefu sana tusipo badilisha safu za kuongozi katika safu za juu basi tutaendelea kudumaa na nidhamu za woga.
Naomba msaada wadau wa elimu.Serikali inatenda haki hapo?
Hii ni March 20 ya 2008 au 2009? Kama ni 2008, je mwaka huu iko hivyo hivyo au kuna mabadiliko. Huo ni unyanyasaji usio na kifani.
 
Huko wizarani kumejaa watu ambao sio wabunifu bali ni wa kufanya mambo yaleyale kila kukicha. Mimi nilimaliza chuo cha uwalimu hapo hapo Kigurunyembe mwaka 2002 nililipwa sh. 500 kwa siku. Kwa kweli siwezi kuelezea jinsi gani gharama za maisha zilivyopanda. Kwa ujumla watu walioko wizarani hawafai kuendelea kuendesha wizara hiyo. Wanazidi kutuandalia nchi ya watu waliojaa masononeko, hasira, chuki na visasi kitu ambacho ni hatari kwa usitawi wa jamii. Nafurahi kuwa MOTCO wameamua kutukisa kiberiti na kama watu wa wizara wataendelea na mwenendo sijui watawapooza kwa kutumia nini.
 
Duh, pole kumbe ulipitia machungu hayo. Vipi bado uko kwenye ualimu? Mambo yakoje sasa kazini ukilinganisha na chuoni?
 
Back
Top Bottom