Ni gazeti lipi linasema ukweli Tanzania?

Ni gazeti lipi linasema ukweli Tanzania?

Nimekuwa nikipata tabu kuhusu ni gazeti lipi linasema ukweli na inafaa tuliamini hapa Tanzania. UHURU ndilo gazeti kongwe lakini linaegemea mno CCM na serikali yake na hasa wakati wa uchaguzi.

CCM linamilikiwa na CCM. DAILY NEWS nalo ni la serikali na habari zake nyingi ni za kuifagilia serikali na CCM.

NIPASHE ni la Mengi lakini habari zake ni kwa manufaa ya mfanyabiashara huyu.

MAJIRA linamilikiwa na watu walio karibu na serikali, linaandika habari kwa kuuma na kupuliza.

MTANZANIA siku hizi ni la ROSTAM AZIZ na hivyo habari zake zimelenga kuwafafagilia baadhi ya watu ndani ya serikali na CCM.

MWANANCHI lenyewe ambalo ndilo linalosambaza nakala nyingi kwa siku ambazo ni kati ya 25,000 na 38,000 linamilikiwa na kampuni za Kenya. Kazi ya MWANANCHI ni kuisema Tanzania na hasa uongozi wake pamoja na CCM hii ikiwa ni kwa maslahi ya Kenya.

TANZANIA ni la wanaCHADEMA kwa hiyo siku zote gazeti hili ni kuisema CCM na serikali yake na hakuna kizuri ambacho kinafanywa na CCM wala serikali.

TANZANIA DAIMA ni kufagilia CHADEMA na upinzani kwa ujumla mwanzo mwisho.

Sasa 'Objectivity" na 'Journalistic Professionalism' kwa magazeti yetu iko wapi? Mimi nazungumzia magazeti tu na wala sitaki kuingilia Radio au televisheni. Uchaguzi Mkuu unakuja, kwa hiyo tutalishwa uongo mwingi.

Hebu mnieleze ni gazeti lipi tuliamini?

Soma ya Udaku
 
Magaziti mengi yananukuu habari za viongozi,habari mhimu za vijijini km kilimo, manyanyaso wanachi, huko magerezani vyakula .zaidi wanaandika habari za mjini
 
jf nayo ni pro-chadema
Umefanya research kulitamka hilo?

Kwa tathnini yangu, kwa kiasi kikubwa JF inajitahidi kubalance habari zake.

Unless wewe ni gamba ambaye ulitegemea JF ifanane na kile chombo chetu cha habari, kinachoendeshwa na kodi zetu wananchi wote, ambayo ni TB- Sisiem, ambayo yenyewe iko biased waziwazi kabisa, ikiwa imeegemea kwa magamba by 100%
 
Mwenyewe umetoa jibu majira linauma na kupuliza
 
Wewe Unaonekana Ni Pro Magamba Kabisa,ni Kipi Usichoelewa? Uhuru Linaandika Ujinga Wa Serikali,hata Ikila Mavi Linaandika Haijala,which Means Halifai,magazeti Yote Ya Serikali Yanapotosha,nipashe Na Tanzania Daima Yanaandika Ukweli Halisi Wa Mambo Ulivyo Nchini,magazeti Yote Yanajulikana Hukuwa Na Sababu Ya Kutaka Kujua Eti Ni Gazeti Lipi Linaandika Ukweli,wewe Ni Mtanzania Upo Hapa Tanzania,hali Ya Nchi Ilivyo Unaiona,sasa Unauliza Nini Kama Siyo Ujinga Kukutawala Ktk Akili Yako? Kusoma Hujui,hata Picha Huoni?
 
Magazeti Tanzania ni shida. Gazeti linaandika eti "KIKWETE AFICHUA SIRI YA KUPIGWA LIPUMBA: ASEMA SHERIA ZA NCHI LAZIMA ZIFUATWE". Siri ni ipi hapo? Soma na uyaache yaliyoandikwa humo humo gazetini usiyabebe kichwani.
 
Back
Top Bottom