Ni gazeti lipi linasema ukweli Tanzania?

Ni gazeti lipi linasema ukweli Tanzania?

1954

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Posts
11,274
Reaction score
13,788
Nimekuwa nikipata tabu kuhusu ni gazeti lipi linasema ukweli na inafaa tuliamini hapa Tanzania. UHURU ndilo gazeti kongwe lakini linaegemea mno CCM na serikali yake na hasa wakati wa uchaguzi.

CCM linamilikiwa na CCM. DAILY NEWS nalo ni la serikali na habari zake nyingi ni za kuifagilia serikali na CCM.

NIPASHE ni la Mengi lakini habari zake ni kwa manufaa ya mfanyabiashara huyu.

MAJIRA linamilikiwa na watu walio karibu na serikali, linaandika habari kwa kuuma na kupuliza.

MTANZANIA siku hizi ni la ROSTAM AZIZ na hivyo habari zake zimelenga kuwafafagilia baadhi ya watu ndani ya serikali na CCM.

MWANANCHI lenyewe ambalo ndilo linalosambaza nakala nyingi kwa siku ambazo ni kati ya 25,000 na 38,000 linamilikiwa na kampuni za Kenya. Kazi ya MWANANCHI ni kuisema Tanzania na hasa uongozi wake pamoja na CCM hii ikiwa ni kwa maslahi ya Kenya.

TANZANIA ni la wanaCHADEMA kwa hiyo siku zote gazeti hili ni kuisema CCM na serikali yake na hakuna kizuri ambacho kinafanywa na CCM wala serikali.

TANZANIA DAIMA ni kufagilia CHADEMA na upinzani kwa ujumla mwanzo mwisho.

Sasa 'Objectivity" na 'Journalistic Professionalism' kwa magazeti yetu iko wapi? Mimi nazungumzia magazeti tu na wala sitaki kuingilia Radio au televisheni. Uchaguzi Mkuu unakuja, kwa hiyo tutalishwa uongo mwingi.

Hebu mnieleze ni gazeti lipi tuliamini?
 
Tanzania kuna vipeperushi magazeti hakuna, usipate shida kutafuta.waandishi wananunulika kaz yao ni kupotosha jamii tu.
 
nilikuwa na nunua gazeti moja tu la mwananchi ila kwa sasa imani imeshuka ... sina hamu tena na gazeti lolote, consistency ya kununua magazeti imeisha ,ninanunua very occasionally.
 
Mwananchi nilili heshimu sana zamani lakin tokea huu muungano wa CoW uanze limekuwa Puppet ya Kenya na vibaraka wake!
 
Raia mwema, guradian na citizen
 
Lile walilolifungia mwana halisi lilikuwa linazungumza ukweli juu ya uozo uliopo kwa viongozi serikalin
 
CHUKI TU BINAFSI:Inaonekana Hata GAZETI Hujawahi Kununua.Anyway ANZISHA LAKO LIWE LINAKUFAGILIA NA WEWE,ULIAMINI 100%
 
Magazeti material ni haya utake au usitake: mawio, jamhuri, raia mwema ,majira na mwananchi communication gazetes. Usiposoma kati ya hayo usome lipi sasa, japo yanawekewa mipaka, isingekuwa hivyo yangekuwa mazuri zaidi. Mengine magazeti dada yako online yatembelee ujionee.
 
Back
Top Bottom