Toxic Concotion
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 5,785
- 21,025
Itakuwaje siku ikatokea maisha yako yote yakaonyeshwa mbele ya hadhara ya watu, kila ulilofanya la siri na dhahiri? Mangapi usingetaka yaonekane?
Itakuwaje siku ukaweza kusoma fikra za watu juu yako, kila kile wanachokiwaza kwako, unadhani wangapi watabaki karibu yako?
Itakuwaje siku ukigundua una kauli moja tu ya mwisho na yapaswa kuitumia ipaswavyo, ni nani utaitumia kwake na nini utamwambia?
Itakuwaje siku kila dua inayoombwa juu yako ikajibiwa unadhani wangapi wamekuombea mema?
Nafsi ya mtu inaficha mengi, ishi maisha yako kwa njia ambayo huna siri ya kukudhalilisha. Huwezi ridhisha wote ila haimaanishi uudhi watu pale inapoepukika.
They are my thoughts u don't have to believe in em as we all entitled to our personal opinions................