Janga la ukatili unaokithiri ni kutokana na fikra dumavu zinazopandikizwa kwa watoto wadogo

MwanaWA Ebrania

JF-Expert Member
Oct 6, 2017
940
1,138
Amani iwe nawe Mtu wa MUNGU

Rafiki yangu wa Thamani
Leo Nakuomba nikukumbushe kuhusu Madhara ya FIKRA za Matendo ya Ukatili Kwa Jamii.

Naamini Unajua Kuwa Ukatili ni matokeo ya Udumavu wa FIKRA 🧏.

Wahusika wakuu wa Matendo ya Ukatili ni wale manusura waliojeruhiwa na watu wenye FIKRA Katili 🥲

Nikushirikishe simulizi fupi iliyonitokea wakati nikiwa mtoto wa miaka 9, huwa sipendi kuikumbuka hii simulizi Kwa sababu inanitoa machozi Kila ninapoitafakari🧏

Natamani niizoee na kuchukulia kama vipande vingine vilivyomo kwenye mapito ya maisha yangu lakini Kwa kipande hicho ni nashindwa zaidi najikuta nalia🥲

_1st _Ilikuwa katikati ya mwaka 1999 wakati huo nikiwa mtoto wa miaka 8-9.
Nikiwa na Rafiki yangu Bruno, kwa sasa ni marehemu (RIP).

Tukiwa safarini tumedandia Treni tumetoka Mbeya tunarudi Dar Es Salaam.

_Tulisafiri salama tangu tulipodandia kutoka Mbeya, shida ilianza mara Baada ya kutoka station ya Morogoro

Kwenye Treni kunawalinda Usalama wanaitwa Matii-tii (Askari wa usalama)
Kuna Askari anaitwa sajent Michael,
Alitukamata akawaita na wenzie wakatufunga Kamba na kutufungia kwenye chumba kidogo🥲

Sasa huyo Afande Michael baada ya muda alirudi akaanza kutupanga Kwa maneno ya vitisho kuwa yeye ndiye kiboko ya watoto watukutu na walioshindikana Kwa family zao, hivyo kama tunahitaji kuishi, tujiandae kumpa anachokitaka ili afurahi moyo wake, tofauti na hapo ataturusha nje ya Treni ili tufe 🥲 wakati hayo yanaendelea Treni iko speed kubwa.

Mara alitoka na kutufungia tena lango, me na Bruno tukaendelea kuangahika kujifungua zile Kamba walizotufunga Kwa kuwa walitufunga Kwa kutuunganisha mikono huku tukipeana migongo tulishindwa kujifungua🥲

Mara Afande Michael alirudi tena, Safari hii kidogo alionekana kama amelewa, ndipo akaanza kuvua magwanda yake na kubaki uchi, kisha akasema "sasa nifuraisheni"
Baada ya kusema hayo, akafungua mlango mdogo wa emergency

Ambao ulikuwa Jirani na tuliposimama sisi, ambapo mtu akikusukuma tu kidogo lazima uanguke na kufa moja kwa moja kutokana na upepo mkali uliochangiwa na speed kubwa ya Treni, Nguvu ya upepo ulimfanya mpaka Afande Katili apepesuke asingeshika chuma basi tungedondoka na kufa sote 🥲.

Mara upepo ulitulia kidogo, hofu kuu ililipuka moyoni mwetu na kuona kuwa yule Afande amedhamilia kufanya anachotaka kutufanya, hivyo Tulianza kumshambulia Kwa maneno ya kumuomba msamaha Kwa unyenyekevu Mkubwa 🥲

"Kama hamuwezi kunipa..... Leo mnakufa na mizoga yenu inasangwa na Treni "
Afande Michael aliongea kama Shetani aliyevurugwa na damu

Mara alitu-push kutumia mguu wake wa kulia, kwa kuwa hatukuwahi na balance tukajikuta tupo ewani tunaelea nje ya Treni upepo ukituzonga, ndio Kwa mara ya Kwanza niliona Nguvu ya uvutano kati ya ARDHI hewa/Anga, nilijiona tumeganda juu kama sekunde kadhaa hivi, ndipo Ardhi yenye unyevu-nyevu wa maji ikatuvuta.

Nilijikuta tunadondoka kama kifurushi katikati ya Shamba ya mpunga (Jaruba) nikiwa nimemlalia Bruno 🥲

Nikajikuta na piga kelele mfulizo wakati wote napiga kelele simsikii ndudu yangu Bruno akikohoa wala kupumua🥲 hofu ilizidi kunishika Kwa kuwa pale Kwenye Jaruba kulikuwa na maji afu kichwa cha Bruno kilikuwa chini hivyo nikaanza kuangahika ili kumfanya naye apate hewa🥲

Mara wakatokea wasamaria Wema waliokuwa wanarudi kutoka mashambani kwao.
Walipotufikia tu' nilipoteza fahamu🥲

Nilikuja kuzinduka siku ya pili tuko hospital ya Mzenga Pwani, Bruno akiwa anakunywa uji kwenye kitanga kingine kilichokuwa Jirani nami🥲.

Leo tuishie hapa.
Kwa nini nimeamua kukushirikisha simulizi hii fupi ambayo katika vipande vingi vinavyoumiza kwenye maisha yangu, hiki akiumizi sana.

Lakini ni kipande ambacho kinaniliza sana kila wakati napokikumbuka.

Kipande hiki Kinaumiza kwa sababu,
1-Mtu anayeshiriki kufanya Ukatili huu ni mtu aliyeaminiwa na Mamlaka kuu ya Serikali kuwa Mlinzi Kwa ajili ya Usalama na msimamizi wa Amani Kwa Jamii na Taifa.

2_Ni mtu ambaye jamii inaona iko salama akiwa katikati yao.

3_Ni mtu ambaye Kila siku anahesabu no Kwa Rais.

_Lakini huko siri ni mtu ambaye hatari sana🥲 mtu mwenye Fikra Dumavu, Hasi, Mtu mwenye kupanda na kuchipusha UKATILI

Watu kama hawa wapo wengi Kwa Taifa letu,
Kila saa wanapandikiza Fikra Katili Kwa mtu mmoja, piga hesabu Kwa week anapandikiza watu wangapi!?
Mbaya zaidi tusiombee wapandikize fikra katili Kwa watoto wetu, maana mpaka watakapokuwa watakuwa wamepandikiza sehemu kubwa sana Kwa Taifa na dunia

Matokeo ya Ukatili tunaoona Leo duniani ni kutokana na Matendo waliyotendewa watu wakiwa wadogo

Baada ya miaka 10 kupita - Siku moja majira ya saa 6 usiku, nikiwa kijana nimeyazoea maisha ya mtaani nikiwa na kundi la Mabraza Akina Abubakar Katwila Maarufu kama Q-Chief, kaka mkubwa John Mjema (mwanamusiki wa zamani) Emmanuel (Ney wa Mitego)

Pamoja na Mabraza wengine,
Nilikutana na macho Kwa macho na Afande Michael akiwa anakabwa na kundi la Vijana waporaji,
Nilimjua baada ya kusikia sauti yake

Tukae kumpa msaada kwa kuwa wale vijana pia tulikuwa tunawajua.
Baada ya kumsaidia alitushukuru, kisha nikamkumbusha kitu alichotufanyia kwenye Treni Tukiwa wadogo na Ndugu yangu Bruno 🥲

Kundi lile la Mabraza waliposikia Habari zile walipanic sana na kutaka kumpiga yule Afande Michael, Vijana hao wakiongozwa na Q-Chief na Baraka Paul.

Unajua nini kilitokea! Yule Afande alikuwa anatetemeka na kuanza kujikojolea, aliomba msamaha wa Kila Rangi.
Lakini Mwisho alijifunza kitu kikubwa sana alituahidi hatorudia tena na atakuwa Mwalimu mzuri Kwa watu wengine

Nachotaka kusema ni kwamba, UKATILI ni Janga kubwa sana Kwa jamii yetu.
Ili kuushinda inatakiwa Elimu kubwa ya mabadiliko ya FIKRA ifanywe Kwa watoto wetu.

Tuseme na watoto wetu Kila siku kuhusu Ukatili, tuwaonyeshe Matendo Mema kwao, Ili kuzikuza fikra zao katika kutafakari yaliyo mema zaidi.

Kwa maana Imeandikwa "MLEE MTOTO KATIKA NJIA IPASAYO NAYE HATAIACHA HATA ATAKAPOKUWA MZEE".

TUTAUSHINDA UKATILI KWA KUBADILI FIKRA ZA KIZAZI CHETU🧏

Imeandikwa na James Yustar
0657579300
jamesfoundation2@gmail.com
20221117_193403.jpg
 
Mwanzo ulisema ni kipande kinachokuumiza sana, mwisho unasema hicho kipande hakikuumizi sana kati ya vipande vyote vya simulizi ya maisha yako.

Ni unatangaza hicho kitabu pichani, umeshare ili tujifunze tu au kupi ni kipi mkuu. Ungekua specific ingependeza zaidi!!
 
Mwanzo ulisema ni kipande kinachokuumiza sana, mwisho unasema hicho kipande hakikuumizi sana kati ya vipande vyote vya simulizi ya maisha yako.

Ni unatangaza hicho kitabu pichani, umeshare ili tujifunze tu au kupi ni kipi mkuu. Ungekua specific ingependeza zaidi!!
Kwani maelezo yanasemaje mkuu!?
Hujaelewa nini!?
Unataka kujua kipi!?
Maelezo niliyoyatoa yanajitosheleza hayo mengine jazia wewe
 
Andiko halihusuani na biashara
Ama ulipo soma umeona nimetangaza biashara
Kwani Akili imewekwa kichwani Kwa ajili ya nini🧏‍
Picha yako uliyoweka inadhihirisha hilo, sio lazima useme unafanya biashara ndgu. Ni tangazo hilo.

Sasa ningeng'amua vipi kua wafanya biashara(kitu ambacho umekubali pia).
 
Habari za Leo Ndugu wajumbe
Nawakaribisha woote kwenye Dua na Sala
Kuombea Amani Taifa letu Nzuri
IMG-20221202-WA0034.jpg
 
Back
Top Bottom