Ndio maana nasema labda hujui kiswahili.
Kikao au mkutano kuwa wa hadhara sio lazima mkutano ufanyike uwanjani au nje ya jengo.Mkutano unaweza ukafanyika ata chumbani lakini ukawa ni mkutano wa hadhara.Mfano, mkutano ukafanyika ukumbuni, watu wamejaa ndani ya ukumbi na hakuna mtu anazuiliwa kuingia,huo ni mkutano wa hadhara.Mjadala wa Bunge ni mjadala ulio hadharani japo unafanyika ndani ya ukumbuni ndio maana umeona wakigombana mle ndani kwa sababu ipo hadharani.Lakini utakuwa mkutano wa ndani tu kama ujumbe wake unasikilizwa tu na watu wachache maalum na wengine hawaruhusiwi,mfano Bunge lisipoonyeshwa kwenye TV na waandishi wa habari wakaondolewaa basi unageuka kuwa mkutano wa ndani(kwa wabunge tu).
Hivyo unaweza ukawepo chumbani kwako lakini ukarushwa live kwenye TV ni mkutano wa hadhara,maana hufichi lolote,kila mtu anashuhudia unachosema.Mikutano ya ndani ya CCM haiwezi kurushwa kwenye TV, mkutano wa ndani ni maalum tu kwa watu walioko ndani, haupaswi kusikika kwa walio nje, mkutano wa kamati kuu wa kuchunja wagombea kuwa watano na wa halmashauri kuu kuchuja wagombea kuwa watatu itakuwa mikutano ya ndani(siri).Haitaonyeshwa kwenye TV.Ni mkutano mkuu peke yake ndio utakakuwa wa hadharani,utarushwa Live kwenye TV.Elewa hivi vitu.
Ile ya Marekani inaitwa town hall meetings, mikutano ya kwenye hall,ambayo sio ya kusikiliza tu hotuba lakini zaidi kuhojiana na mgombea/maswali na majibu ya papo kwa papo,ni mikutano ya hadhara.Usichanganye hivi vitu.Uzuri wa mikutano ya namna hii mgombea hana nafasi ya kudesa au kuulizia,inabidi awe fiti na anajua anachosema maana hawezi kujua ataulizwa nin.Wanasiasa wa kwetu mikutano ya namna hii ni wachache sana watakubali.