Edson Carrington
JF-Expert Member
- Oct 30, 2022
- 216
- 634
Habari wakuu,
Serikali ya awamu ya sita imezidiwa. Tena imezidiwa haswaa.
Hakuna upande hata mmoja uliotekelezwa na kwenda kama inavyotakiwa kwa maana nyingine, sera za serikali hii kwa kiasi kikubwa zinaonekana kuikandamiza nchi zaidi ya kufanya maendeleo.
Hakuna namna, hata wenye mamlaka wanaona jinsi nchi inavyokwenda mrama, lakini kiukweli hawawezi sema TUMESHINDWA. Klichobaki ni kuangalia maslahi yao wao wenyewe.
Hebu niambie sekta gani imeenda sawia, toka uongozi huu uanze!?
ELIMU
Malalamiko yamekuwa ni mengi, wanafunzi wanashindwa kuendelea na elimu ya juu kwa kukosa mikopo inayokidhi. Hali ya walimu bado ni hoi taabani.
UCHUMI
WB wamekuja na takwimu zao baada ya serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani, "Tanzania imeshuka kutoka uchumi wa kati na kurudi kuwa nchi ya uchumi wa chini", hiki ni kiashiria kikuu cha uchumi wa nchi kuzorota. Pia mfumuko wa bei za bidhaa unadhihirisha kuwa uchumi wetu bado uko chini kwa mara nyingine.
MADENI KUONGEZEKA MARADUFU
Serikali ya awamu ya sita imejikita zaidi kwenye kukopa, na kwa bahati mbaya hatuwekwi wazi juu ya vigezo vya mikopo hiyo. Hakuna mradi unaoweza kuendeshwa kwa pesa za ndani ya nchi, miradi yote inategemea kwenda kupiga magoti kwa mabeberu.
KODI NA TOZO
Serikali imekosa mpaka namna ya kutafuta mbinu mbadala za ukusanyaji wa kodi, zaidi ya kuwakamua raia wake kiasi kwamba mpaka wanakiuka haki za kibadamu. Serikali kila siku inafikiria wapi watatupata vizuri watukamue kodi ya kutosha, baada ya kutukomesha kwenye vifurushi.
KILIMO
Huku ndio kuna hali mbaya, tunaaminishwa kuna maboresho lakini mwisho wa siku hakuna matokeo ya maana, wakulima bado wana hali ngumu na bado vyakula vinazidi kupanda gharama.
VILIO KWA MASIKINI
Masikini wanalia, lakini hakuna wa kuwasikiliza. Sera nyingi zinazoundwa zinaonekana kutowagusa kabisa. Wamachinga wamepigwa marufuku bila mbinu mbadala ya kuwawezesha, wengine kuvunjiwa vibanda vya biashara na kubaki wakitaabika.
UMEME WA MGAO
Hii inadhihirisha bado kuna kitu hakiko sawa, mfano mdogo tu! Tulisahau tatizo la umeme kwenye serikali ya awamu ya tano. Ila kwa mara nyingine hili tatizo limerudi kwa kasi bila ya viongozi kuwa na ufumbuzi.
TATIZO LA MAJI
Tatizo hili lilianza kutafutiwa ufumbuzi, ila kwa sasa ghafla limesimama na linajirudia tena. Maeneo mengi bado maji ni kitendawili, maji yamekuwa tatizo kwa kiasi kikubwa.
Bado kuna mengi mengi mengi siwezi yote kuorodhesha,
Muwe na siku njema.