Ni dhahiri serikali ya awamu ya sita imechemsha

Edson Carrington

JF-Expert Member
Oct 30, 2022
216
634
Habari wakuu,

Serikali ya awamu ya sita imezidiwa. Tena imezidiwa haswaa.
Hakuna upande hata mmoja uliotekelezwa na kwenda kama inavyotakiwa kwa maana nyingine, sera za serikali hii kwa kiasi kikubwa zinaonekana kuikandamiza nchi zaidi ya kufanya maendeleo.

Hakuna namna, hata wenye mamlaka wanaona jinsi nchi inavyokwenda mrama, lakini kiukweli hawawezi sema TUMESHINDWA. Klichobaki ni kuangalia maslahi yao wao wenyewe.

Hebu niambie sekta gani imeenda sawia, toka uongozi huu uanze!?

ELIMU
Malalamiko yamekuwa ni mengi, wanafunzi wanashindwa kuendelea na elimu ya juu kwa kukosa mikopo inayokidhi. Hali ya walimu bado ni hoi taabani.

UCHUMI
WB wamekuja na takwimu zao baada ya serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani, "Tanzania imeshuka kutoka uchumi wa kati na kurudi kuwa nchi ya uchumi wa chini", hiki ni kiashiria kikuu cha uchumi wa nchi kuzorota. Pia mfumuko wa bei za bidhaa unadhihirisha kuwa uchumi wetu bado uko chini kwa mara nyingine.

MADENI KUONGEZEKA MARADUFU
Serikali ya awamu ya sita imejikita zaidi kwenye kukopa, na kwa bahati mbaya hatuwekwi wazi juu ya vigezo vya mikopo hiyo. Hakuna mradi unaoweza kuendeshwa kwa pesa za ndani ya nchi, miradi yote inategemea kwenda kupiga magoti kwa mabeberu.

KODI NA TOZO
Serikali imekosa mpaka namna ya kutafuta mbinu mbadala za ukusanyaji wa kodi, zaidi ya kuwakamua raia wake kiasi kwamba mpaka wanakiuka haki za kibadamu. Serikali kila siku inafikiria wapi watatupata vizuri watukamue kodi ya kutosha, baada ya kutukomesha kwenye vifurushi.

KILIMO
Huku ndio kuna hali mbaya, tunaaminishwa kuna maboresho lakini mwisho wa siku hakuna matokeo ya maana, wakulima bado wana hali ngumu na bado vyakula vinazidi kupanda gharama.

VILIO KWA MASIKINI
Masikini wanalia, lakini hakuna wa kuwasikiliza. Sera nyingi zinazoundwa zinaonekana kutowagusa kabisa. Wamachinga wamepigwa marufuku bila mbinu mbadala ya kuwawezesha, wengine kuvunjiwa vibanda vya biashara na kubaki wakitaabika.

UMEME WA MGAO
Hii inadhihirisha bado kuna kitu hakiko sawa, mfano mdogo tu! Tulisahau tatizo la umeme kwenye serikali ya awamu ya tano. Ila kwa mara nyingine hili tatizo limerudi kwa kasi bila ya viongozi kuwa na ufumbuzi.

TATIZO LA MAJI
Tatizo hili lilianza kutafutiwa ufumbuzi, ila kwa sasa ghafla limesimama na linajirudia tena. Maeneo mengi bado maji ni kitendawili, maji yamekuwa tatizo kwa kiasi kikubwa.

Bado kuna mengi mengi mengi siwezi yote kuorodhesha,

Muwe na siku njema.
 
Amka usingizini maana Tanzania kumekucha Sasa chini ya uongozi shupavu wa mama Samia. Katika kilimo kwa Sasa Hali Ni njema Sana Tangia tupate Uhuru Tumeona bajeti ikiongezeka Hadi kufikia billioni Mia Tisa na point huku serikali ikitoa mabillioni ya Ruzuku katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni, huku soko likiwa Ni la uhakika kabisa kwa mazao ya mkulima kuanzia wakati wa mavuno,wakulima huwaambii kitu juu ya mama Samia maana wanamuona Kama mkombozi wao katika kilimo aliyekuja kwa wakati muafaka.

Ukija katika Elimu nako Ni mafanikio na matumaini matupu kwa watanzania,mfano mh Rais amefuta Ada zote kuanzia shule za msingi Hadi kidato Cha sita ambapo Sasa watoto wanaotoka familia za kipato Cha chini wanamatumaini ya kupata Elimu bila kikwazo Cha aina yoyote Ile,lakini pia katika Elimu ya juu wanafunzi wengi wamepata mikopo ya Elimu ya juu na hivyo kupat fursa za kutimiza Ndoto zao

Ukija kwa vijana nako mh Rais amewasha taa ya Matumaini katika mioyo ya Vijana kwa kutoa ajira karibu secta zote zinazofikia elfu 42 zikiongozwa na secta ya Elimu na Afya,huku pia vijaa wengine wengi wakipata mikopo kupitia halmashauri zao na kuwawezesha kupata mitaji kwa ajili ya kufungua biashara mbalimbali za kuwaingizia vipato

Ukija katika uchumi unakuta nako mambo Ni mazuri kabisa ndani ya muda mfupi wa utawala wa Rais wetu,kwa kuwa Ni kipindi hiki ambako Tanzania imeshuhudia mafuriko ya watalii na wawekezaji kuingia nchini mwetu.kunakotokana na Sera na kuimarika kwa diplomasia yetu ya uchumi kulikoimarishwa na mh Rais wetu mpendwa hasa baada ya wazo lake la kibunifu la royal Tour lililotangaza vivutio vyetu vya utalii pamoja na kuitangaza nchi yetu

Ukija katika huduma za kijamii nako unakuta mapinduzi makubwa Sana yamefanyika ,ambapo karibu kila Kona ya nchi unakuta miradi mbalimbali imejengwa ikiwepo vituo vya Afya Kam tulivyoshuhudia hapa majuzi vituo vya Afya takribani 234 vikijengwa na madarasa zaidi ya elfu nane yamejengwa yaliyotokana na tozo zetu

Upande wa biashara nako Ni imara Sana,kwa kuwa kwa Sasa Biashara zinaongezeka kila Siku badala ya kufungwa hii Ni kutokana na kuimarika kwa mazingira ya kibiashara,ambapo kwa Sasa wafanyabiashara wanafanya biashara bila hofu Wala bughuza,wanakadiliwa mapato kwa haki bila maonezi
 
Simple, apunguze kuzurura nje ya nchi, aendepo huko watendaji wake wanapiga hela
Safari za mh Rais nje ya nchi Zimekuwa Ni za faida kubwa Sana kwa Taifa letu,tumeshuhudia kupitia safari hizo Diplomasia yetu ikiimarika na kuwavutia wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa ambao Sasa wanakimbilia kuja kuwekeza Tanzania na hivyo kutoa fursa za ajira kwa vijana na kuongeza wigo wa Kodi,lakini pia Ni safari hizo Tumeona China ikitusamehe Deni la Billion 31 pesa ambayo tutaitumia kuwekeza katika shughuli nyingine za kiuchumi
 
Amka usingizini maana Tanzania kumekucha Sasa chini ya uongozi shupavu wa mama Samia. Katika kilimo kwa Sasa Hali Ni njema Sana Tangia tupate Uhuru Tumeona bajeti ikiongezeka Hadi kufikia billioni Mia Tisa na point huku serikali ikitoa mabillioni ya Ruzuku katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni, huku soko likiwa Ni la uhakika kabisa kwa mazao ya mkulima kuanzia wakati wa mavuno,wakulima huwaambii kitu juu ya mama Samia maana wanamuona Kama mkombozi wao katika kilimo aliyekuja kwa wakati muafaka.

Ukija katika Elimu nako Ni mafanikio na matumaini matupu kwa watanzania,mfano mh Rais amefuta Ada zote kuanzia shule za msingi Hadi kidato Cha sita ambapo Sasa watoto wanaotoka familia za kipato Cha chini wanamatumaini ya kupata Elimu bila kikwazo Cha aina yoyote Ile,lakini pia katika Elimu ya juu wanafunzi wengi wamepata mikopo ya Elimu ya juu na hivyo kupat fursa za kutimiza Ndoto zao

Ukija kwa vijana nako mh Rais amewasha taa ya Matumaini katika mioyo ya Vijana kwa kutoa ajira karibu secta zote zinazofikia elfu 42 zikiongozwa na secta ya Elimu na Afya,huku pia vijaa wengine wengi wakipata mikopo kupitia halmashauri zao na kuwawezesha kupata mitaji kwa ajili ya kufungua biashara mbalimbali za kuwaingizia vipato

Ukija katika uchumi unakuta nako mambo Ni mazuri kabisa ndani ya muda mfupi wa utawala wa Rais wetu,kwa kuwa Ni kipindi hiki ambako Tanzania imeshuhudia mafuriko ya watalii na wawekezaji kuingia nchini mwetu.kunakotokana na Sera na kuimarika kwa diplomasia yetu ya uchumi kulikoimarishwa na mh Rais wetu mpendwa hasa baada ya wazo lake la kibunifu la royal Tour lililotangaza vivutio vyetu vya utalii pamoja na kuitangaza nchi yetu

Ukija katika huduma za kijamii nako unakuta mapinduzi makubwa Sana yamefanyika ,ambapo karibu kila Kona ya nchi unakuta miradi mbalimbali imejengwa ikiwepo vituo vya Afya Kam tulivyoshuhudia hapa majuzi vituo vya Afya takribani 234 vikijengwa na madarasa zaidi ya elfu nane yamejengwa yaliyotokana na tozo zetu

Upande wa biashara nako Ni imara Sana,kwa kuwa kwa Sasa Biashara zinaongezeka kila Siku badala ya kufungwa hii Ni kutokana na kuimarika kwa mazingira ya kibiashara,ambapo kwa Sasa wafanyabiashara wanafanya biashara bila hofu Wala bughuza,wanakadiliwa mapato kwa haki bila maonezi
Mkuu Unalipwagwa sh ngapi kusifia namna hii
 
Silipwi hata Senti Wala sipo hapa kwa ajili ya kulipwa Bali nimeridhishwa na utendaji kazi wa mh Rais na ndio maana naandika kwa ushahidi kwa Yale niyaonayo kwa macho yangu,maana mambo makubwa anayoyafanya Rais wetu yanaonekana kwa macho ya kila mwenye macho na ambaye hajafungwa kifikira
 
Binafsi siwezi kutoa sifa nyingi kama hizi tena nyingi nikijua kabisa nasema uongo. Bora nikae kimya kuliko kuiongopea nafsi yangu
 
Haya yote yanaeletwa na uroho wa madaraka yule mtoto wa mkuu wa mkoa mstaafu wa dar es salaam na katibu mkuu wa chama sijui kwenye uwaziri mkuu kuna nini kijana ana figidu za ajabu sana umeme tatizo maji tatizo yani anamtafutia timing mtu wa Mtwara uko kwa mbali sana lengo ajae tu

Hatujasahau mambo ya filikunjombe kilichomtokea kisa uwaziri mkuu na ndio sasa sinema za umeme tunaziona
 
Silipwi hata Senti Wala sipo hapa kwa ajili ya kulipwa Bali nimeridhishwa na utendaji kazi wa mh Rais na ndio maana naandika kwa ushahidi kwa Yale niyaonayo kwa macho yangu,maana mambo makubwa anayoyafanya Rais wetu yanaonekana kwa macho ya kila mwenye macho na ambaye hajafungwa kifikira
Vipi kuhusu mgao wa umeme, maji, ugumu wa maisha maswala ya mamikopo selikali ichukuayo kila uchwao pia waliona hilo?
 
Hakuna serikali isiyokopa,kinachoangaliwa unakopa ili ufanyie Nini? Je Kuna tija inayopatikana na kuonekana baada ya kukopa? Ni aina gani ya mkopo? Mashariti ya mkopo yapoje? Utarudishwa baada ya muda gani? Unakwenda kufanya shughuli gani? Mikopo yote iliyokopwa na serikali yetu Ni mikopo yenye mashariti nafuu na Tumeona kazi zilizofanyika kutokana na mikopo hiyo,Ni mikopo isiyo na mashariti magumu ya kuhatarisha usalama wa Taifa letu na kuweka rehani nchi yetu
 
Back
Top Bottom