Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,607
- 729,505
Hapo nyuma ilikuwa (inaonekana) ni kwa ajili ya kuwaandama wapinzani na kuwalinda wapigaji pesa ndefu, usalama wa Taifa kikawa ni kitengo kilichokosa heshima yake katika jamii, kukawa na mpaka watu wenye vitambulisho vya usalama na kila mwenye bastola alijifanya kuwa usalama hata kama ni bandia, watu waliringa na kujinasibu na usalama, ilikuwa kama fasheni, hata humu jamvini kuna baadhi walijiita usalama special branch.
Leo hii mambo ni tofauti kabisa. Hawa usalama wa kweli wana faili la kila mmoja huko serikalini na pengine hata huku mitaani, hii kamata kamata si ya kukurupuka wala bahati mbaya, ikifikia hatua ya kupandishwa kizimbani mengi yameshafanyika.
Kinachofanyika sasa hivi ni hiki, nitatoa mfano wa mtuhumiwa X.
Huyu tuseme alikuwa Mkurugenzi kwenye idara fulani kwa miaka kadhaa, akafanya kazi kwa mazoea na vimemo kutokana na mwenendo wa utawala uliopo, akapiga kwa msaada wa mtandao wa wizi uliokuwepo, akafanya mengi bila hofu.
Lakini katika kufanya haya yote TISS walifahamu kila kitu ila hawakuwa na uwezo wa kufanya lolote kulingana na mazingira yaliyokuwepo.
Kwahiyo sasa TISS wanaombwa faili la Mkurugenzi X kisha linafanyiwa kazi, linafuatiliwa kila kitu chake; bank accounts, mali, jumbe mbalimbali za simu, miito, ndugu jamaa na hata marafiki ikiwemo wageni waliofanya naye mawasiliano yoyote yale.
Hili likishakamilika ni hatua ya kwanza... Hii inafanywa kimyakimya na kwa siri kubwa, kinachofuata ni kutembelewa ofisini kwako kuulizwa maswali ya kizushi na mwisho kupumzishwa, au wakati mwingine kupumzishwa tu au kubadilishwa nafasi au kusimamishwa.
Baada ya hapo unarudi nyumbani lakini ndani ya siku zisizozidi tano jamaa wanakuja nyumbani kwako na official search warrant! Wanakupekua mpaka chooni kisha wanaondoka na baadhi ya vitu vyako kama simu, laptop, diaries nk.
Huko wataenda kumonitor kila ujumbe na na kila muito, kisha utaitwa rasmi kuja kutoa passwords na locks zote kwenye simu na laptop. haya yote yanafanyika kwa kusaini mwenyewe.
Baada ya hapo wataendelea na kazi yao huku ukiruhusiwa kurudi nyumbani.
Huko mitaani wakati huo hawajui kinachoendelea zaidi ya habari za redio mbao. Mwishowe wakishajiridhisha na uchunguzi wao na ushahidi walioupata na kuukusanya, defender inakufuata na kupelekwa kizimbani moja kwa moja kusomewa mashtaka na kupelekwa lupango.
Hii ni hatua ambayo sasa hujulikana na wote TISS wa sasa wamejipanga kuepuka kupigwa mweleka mahakamani na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni kwa kulipa fidia.
Jiulize, mbona Makamba jr yuko kimya sana?
Time will tell!