Ni Demokrasia huzaa maendeleo!! au maendeleo ya nchi ndio huchagiza kupanuka na kukua kwa demokrasia!!?

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
2,829
3,824
Wana jamvi, hivi vitu viwili mimi huwa vinanitatiza kuvielewa, kwamba kipi huwa ndo kichagizo Cha kingine kustawi na kuimarika.

Nimejaribu kufikiria kwenye level za kifamilia na level za ki nchi, lakini pia hata level za kiroho( Muumba na devil).

Kwenye level za kifamilia naweza nikawa na majibu kulingana na mm nataka familia yangu iweje, mfano kwangu Mimi Demokrasia huwa naipa asilimia 25%-45%,the rest percent 55%-75% ni dictatorial (au niseme kwa lugha nzuri nakaza).

kwa upande wa Imani,hapa pananivuruga pia, Ila concern yangu kubwa ni nchi, na ndo hasa nataka mnifungue ,nimejaribu kuyafikilia mataifa makubwa Kama USA ,RUSSIA , GERMANY,UK,CHINA,nk. haya mataifa kweli kwa Sasa yameendelea na kustaarabika kiuchumi n.k lakini swali langu haya mataifa ambayo kwa Sasa tunayaita super power au mataifa yaliyoendelea ,huko nyuma yaani kabla hayajafika hapo yalipo,ilikuwaje !? Je walianza kuwekeza kwenye Demokrasia ! mpaka wakafika hapo walipo!!! au kuendelea kwa mataifa Yao ndiko kumeifanya Demokrasia ya nchi zao iwe Bora na kukua !!?

nadhani Kuna haja Kama ,binadamu wenye utashi ,tuelimishane hapa,ili tujue tusimamie wapi,kwa kulenga kipi!! maana wanasiasa wanatuvuruga ,kwenye haya Mambo mawili , Demokrasia na maendeleo!!!

karibuni !!
 
Demokrasia ndio inayoleta maendeleo ya kweli, demokrasia inaleta taasisi huru ambazo husaidia mno kusukuma maendeleo,

Mfano Bunge letu lingekua huru, definitely lingeiweka serikali yetu at its toes,kila cent ingewajibika kuelewa imetumika vipi,

Bunge huru lingetunga sheria huru na Judiciary huru ingekua ndio inatafsiri hizi sheria kiuhuru,na yote haya yakifanyika kiuhuru watanzania wangesonga mbele kimaendeleo, politicians wangewajibika kutekeleza wajibu wao kisheria,

Ona sasa ni vurugu tupu, matamko mengi ni ya kisiasa, nguvu,udikiteta etc etc,tunahitaji demokrasia ili kusukuma mbele maendeleo!
 
Sasa mimi nitakusaidia,kuanza utafiti wako,,kama u-mvivu wa kupitia maandishi,kutazama/kusikiliza "documentary" basi hii habari mbaya kwako!!


Mtafute mchumi kutokea korea kusini HA JOON CHANG,Anza na kitabu cha KICKING AWAY THE LADDER,
kisha soma soma vitabu vyake vyote!!utafiti na kusaka maarifa ni gharama na muda pia(kuchukua).

Safari njema bwana Mkubwa.
 
Sasa mimi nitakusaidia,kuanza utafiti wako,,kama u-mvivu wa kupitia maandishi,kutazama/kusikiliza "documentary" basi hii habari mbaya kwako!!


Mtafute mchumi kutokea korea kusini HA JOON CHANG,Anza na kitabu cha KICKING AWAY THE LADDER,
kisha soma soma vitabu vyake vyote!!utafiti na kusaka maarifa ni gharama na muda pia(kuchukua).

Safari njema bwana Mkubwa.
asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom