G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Nimefanikiwa kusikiliza "audio clip" ya mtu anayedaiwa kuwa ni Gloria Michael ambaye bila shaka ni mtangazaji wa TBC. Katika hiyo sauti iliyorekodiwa inaonekana dada huyu anakiri wazi kuwa amejiridhisha kuwa ana kila dalili inayoonyesha anaugua COVID 19 na kwa sasa yanaendelea vyema.
Dada anaelezea kuwa alipitia zahanati kadhaa kabla hajalazimika kukimbilia taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete baada ya kuwa anahisi maumivu makali sana kwenye moyo na upande wa mgongoni achili mbali kikohozi kikavu. Anaelezea kuwa ni kweli pale Taasisi ya JK walimpima na kugundua kuwa mishipa ya karibu na moyo imetanuka kwa sababu blood pressure ilikuwa juu. Wakampa dawa akaruhusiwa.
Dawa ambazo yeye mwenyewe anaelezea kuwa hazikumsaidia kitu. Lakini vilevile hapo kabla anakiri kuwa alienda hospitali ndogo ambapo walipompima walimueleza kuwa ana maambukizi mengi kwenye damu bila kuambiwa hasa ni maambukizi ya aina gani.
Kwa maelezo ya dada yetu ni wazi kuwa kote huko hakuna aliyewaza kuhusu COVID kwani achilia mbali kumpima hakuna aliyeweza hata kuongelea jambo hili. Hata taasisi ya JK? Hawana kipimo?
Dada yetu anadai kuwa kilichomfanya akagutuka na kuanza kuwaza kuhusu Corona ni vifo vya wenzao wawili wa kazini na anasema kuwa baada ya kusikia habari ile ya vifo ndipo akagundua kuwa mmoja wa marehemu walifanya kazi kwa ukaribu sana kwa wiki nzima ikiwa ni kuchapisha nyaraka mbalimbali ikiwemo barua ya kupeleka Ubalozi wa Korea kuhusu swala zima la ARIDHIO.
Anasema alipata mshituko na presha kuzidi kuwa juu kutokana na habari hizi. Lakini baada ya hapo ndipo akaanza kuomba ushauri kwa wenzake (Anawataja) ni nini cha kufanya. Akaelekezwa atumie malimao, tangawizi mbichi pamoja na vingine ili kujinusuru. Anadai baada ya kufanya hivyo walau kwa sasa ana nafuu.
Audio hiyo aliitoa siku ya Jumapili ya Pasaka.
Anadai siku ya mwisho kuwa kazini walikuwa na kikao cha menejimenti, alikuwa akilalamikia ugonjwa ila kila mmoja kwenye kile kikao akaona ni jambo tu la kawaida.
Kilichonishtua ni kuwa anadai ameji "lockdown" yeye pamoja na familia yake. Yani serikali haijahusika na yeye pamoja na hii familia! Kweli?
Kiukweli jambo hili linaacha maswali mengi sana yasiyo na majibu.
1. Taasisi ya Jakaya Kikwete haina uwezo wa kupima COVID 19 mpaka mwezi huu wa nne? Au ni kutokuchukulia jambo hili kwa upekee?
2. Serikali inafanya nini kuhakikisha usalama wa jamii kama mgonjwa anadai kuwa ameamua kuji lock down yeye na familia yake? Nini hatima ya hili?
3. Inasubiri hadi lini kusambaza vifaa vya kupimia ugonjwa huu kwenye hospitali zake mbalimbali pamoja na incubators ili sampuli nyingi zipate majibu kwa haraka? Katika hili dada yetu aliambukiza watu wangapi huko alikopita?
Yapo madai mengi mitaani kuwa serikali inasubiri hadi mtu aumwe, ajipeleke mwenyewe hospitali ndipo waitwe kuja kumchukua wakampime ili kugundua kama ana maambukizi ya huu ugonjwa, madai haya yanathibitishwa pia na kisa cha kifo cha kwanza kutokea hapa nchini na sasa haya yaliyotokea TBC.
Hizo fedha za kutoka kwa wafadhili, zile za sherehe zilizoelekezwa huko na ambazo zinatengwa kwenye mfuko wa waziri mkuu wa kukabiliana na majanga kwenye kila bajeti ya mwaka zimefanya mini? Mbona hatuji na mikakati mipya ya kupambana na huu ugonjwa zaidi tu ya kusikia ipo tume imeundwa ambayo nayo haijawahi kujieleza ina au imekusudia kufanya nini la ziada kukabiliana na hili janga?
Chonde chonde Watanzania, narudia tena chonde chonde! Kwa hili tunacheza waziwazi!