Ni busara tu ndio itaokoa CHADEMA

Ni busara tu ndio itaokoa CHADEMA

Mzee Uchwara

Senior Member
Joined
Oct 28, 2013
Posts
119
Reaction score
35
Ndungu zangu wanachama na wapenzi wa Chadema,kuna mgogoro mzito unaoendelea ndani ya chama cha Chadema. Ingawa viongozi wanakanusha, hii inatokana na CC kumvua madaraka yote Mh. Zito na wenzake. Ni lazima tukubali kuwa zito bado ana wafuasi wanaomuunga mkono ndani ya Chadema. Ili binadamu uendelee ni lazima ukubali kukabiliana na changamoto mbali mbali na Chadema ili kistawi vizuri ni lazima kipitie katika changamoto mbali mbali na pia kikubali mgongano wa mawazo. Ndugu zako ili Chadema iepuke huu mtego wa kusambaratika ni lazima busara itumike na si jazba wala kuoneshana ustadi wa kujibizana kwenye vyombo vya habari. Hali hii haijenga, zito kama kijana anae jijenga katika siasa ana mazuri na mabaya,kama tumeona ana mapungufu ni vema tukamwita na kumwambia mapungufu yake na hivyo hivyo kwa uongozi kama una mapungufu ni lazima ukubali kukosolea hii ndio DEMOKRASIA. Ili tutoke hapa salama ni vema suluhu ikapatikana kati ya zito na uongozi wa Chadema. Ebu tujikumbushe kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba uliopitishwa na wabunge wengi wa CCM lakini Raisi kikwete alitumia busara kwa kukaa meza moja na wapinzani na yakaisha. Na hivyo hivyo ndani ya Chadema suluhisho la mgogoro huu si kuwa fukuza kina zito bali ni kukaa meza moja ili Chadema iwe kitu kimoja, na sio maamuzi magumu kama tunavojidanganya. Naomba sana Mh. Mbowe na Dr.slaa mtafakari kwa makini sakata ili na mtumie busara kulimaliza na ubabe. Ni vema mkakaa na zito na wenzake katika meza moja na kutatua mgogoro huu. Kwani mkikaa pamoja mtakosoana na kupata suluhu. Wahenga wanasema vita ya panzi ni furaha ya kunguru. Ili kuwaziba mdomo CCM ni vema tukawa wamoja kwa kutafuta suluhu na kuendelea kukijenga Chama na kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa hapo mwakani. Mungu ibarike CHADEMA.
 
Hekima na busara huwa ni TUNU, si kila mmoja amejaaliwa na Muumba.
 
Hiyo busara yenu mbaki nayo. Busara yetu tunamfuta uanachama akaudai mahakamani. Tumechoka anatumia CDM kupaisha Magamba
 
Tumechoswa na up-pu wenu mnazidi kushusha hadhi ya JF ukilinganisha na miaka michache iliyopita. Hivi kule kwa MACCM kulikojaa wauza unga, mafisadi, majangili kuna busara ya aina yoyote? Busara kwenye issue zipi? Acheni upumbavu wenu wa kuandika uzushi kila kukicha.
 
Tatizo la Zito anataka uenyekiti kwa kutumia machiavellian principle. Kwa nini asikubali kubaki kwenye chama kama mwanachama wa kawaida? Kimsingi Zito hana madhara kwa CDM akiondoka kinyume chaka CDM itabaki imara zaidi baada ya cleansing inayofanyika kwa kuondoa mapandikizi. Kwa nini usitoe mawazo yako ndani ya vikao, unaogopa nini kama sio sabotage? Coward? opportunist/barakala? arrogance?
 
Waacheni wafu wazikane.

Ulaghai wa CHADEMA ulipofikia ni kwenye point of no return. Hakuna mawazo au angalizo litakalokinusuru kwenye maangamizo yanayochochewa na natural dearth to natural death.
 
Chadema walianza na shetani watamaliza na shetani chama cha mzee kinakufa mchana jua linawaka.
 
Busara ni bidha adimu sana Chadema!. Zitto ni kijana mdogo not expected kuwa na Busara ila its very unfortunately wale ambao ndio expected wawe na Busara ndio kwanza wanamtunishia msuli kushindana nani zaidi!.
Nilisema Zitto alipofikia ni zaidi ya Chadema!, kubalini kataeni mfukuzeni muushuhudie muziki wake!.
Pasco
 
Kuna mahali unaweza kuamua kufanya suluhu na mahali hiyo suluhu haiwezekani bali kuchukua hatua sahihi. Kilichofanyika kwa aklna Zito ni sahihi. Ndumila kuwili unaweza kufanya naye suluhisho? Ukigeuka kakunasa!
Na hawa CCM wanaoleta domo lao hapa hapahusu. Malengo yao ya kumtumia yamesambaratishwa. Wasiojua undani wa jambo msiidandie.
 
Back
Top Bottom