happiness win
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 2,461
- 1,384
Naombeni ushauri ili niweze kumshauri rafiki aliyeniuliza kama anaweza kumhoji mumewe kuhusu mali na vitu vingine alivyonavyo maana huyo mumewe amepata ajali mbaya sana na hali yake hairidhishi kama ataendelea kuishi.
Mwanamume huyo ni mfanyabiashara na inaonekana ana mali nyingi tu ambazo mkewe hazitambui vizuri. Baadhi ya ndugu wamemshauri amhoji mumewe kabla hajafa ili mali na vitu vingine visipotee vije wasaidia watoto baadaye.
Mke anasita akijiuliza mumewe atajisikiaje? Jamii itamuelewa? Mke ni mama wa nyumbani na alizoea kufanyiwa kila kitu, sasa nahisi ndugu wanawasiwasi kuwa endapo mume atakufa mali nyingi zitapotea.
Naomba ushauri wenu, huyu mama afanyeje? je ni busara kuhoji? ataeleweka kwa jamii?