Ni busara kuhoji mali za mwenza wako akiwa hoi kitandani?

happiness win

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
2,461
1,383
Naombeni ushauri ili niweze kumshauri rafiki aliyeniuliza kama anaweza kumhoji mumewe kuhusu mali na vitu vingine alivyonavyo maana huyo mumewe amepata ajali mbaya sana na hali yake hairidhishi kama ataendelea kuishi.

Mwanamume huyo ni mfanyabiashara na inaonekana ana mali nyingi tu ambazo mkewe hazitambui vizuri. Baadhi ya ndugu wamemshauri amhoji mumewe kabla hajafa ili mali na vitu vingine visipotee vije wasaidia watoto baadaye.

Mke anasita akijiuliza mumewe atajisikiaje? Jamii itamuelewa? Mke ni mama wa nyumbani na alizoea kufanyiwa kila kitu, sasa nahisi ndugu wanawasiwasi kuwa endapo mume atakufa mali nyingi zitapotea.

Naomba ushauri wenu, huyu mama afanyeje? je ni busara kuhoji? ataeleweka kwa jamii?
 
Kama ataona umuhimu huyo marehemu mtarajiwa ataanza kusema mwenyewe tena kwa mtu anaemtaka.Mambo ya kuuliza mtu hajafa yanapicha mbaya sana kwa mgonjwa kwa kuwa ataona namna gani huyo mke anavyotanguliza maslahi kuliko uhai wa mumewe.
 
Hapo pagumu... Amuulize ila atumie ujanja, amwambie kwa kuwa utachukua muda hapa hospital basi niambie wadeni wako na biashara zako ili nisimamie au nimuulezeke mtu wa kusimamia maana la sivyo atamkatisha tamaa mgonjwa, huwezi jua Mungu mkubwa, anaweza kupona huyo so awe very carefully kwenye kuongea.
 
wanaume sasa msipowaamini wake zenu kiasi cha wao kujua asset zenu mnawaamini kina nani jamani!

ona sasa mambo ya kuanza kuulizana vitandani ICU ''eti beby niliwahi kusikia kuwa una kampuni ya uwindaji ngorongoro file lake liko wapi?''uuuuwih hamad kabla hujamjibu vizuri unazidiwa anakutingishaje mabega sio ili upone hapana ili uendelee kumwelekeza zilipo mali zingine!
cha kutufanya tuonekane wachawi kwa mama zenu au dada zenu ni nini jamani!
kwa walio na hii tabia hebu jirekebisheni!
mke wako ni wewe ndani yake!hebu badilikeni jamani!
 
it's a tough call indeed....ila nafikiria kuwa mwanaume anaweza kuulizwa ila kuna baadhi ya maneno yatapaswa kuepukika.
Busara ya hali ya juu itahitajika kwenye kupangilia matamshi...
 
wanaume sasa msipowaamini wake zenu kiasi cha wao kujua asset zenu mnawaamini kina nani jamani!

ona sasa mambo ya kuanza kuulizana vitandani ICU ''eti beby niliwahi kusikia kuwa una kampuni ya uwindaji ngorongoro file lake liko wapi?''uuuuwih hamad kabla hujamjibu vizuri unazidiwa anakutingishaje mabega sio ili upone hapana ili uendelee kumwelekeza zilipo mali zingine!
cha kutufanya tuonekane wachawi kwa mama zenu au dada zenu ni nini jamani!
kwa walio na hii tabia hebu jirekebisheni!
mke wako ni wewe ndani yake!hebu badilikeni jamani!

Kwa kweli kutokuwa wazi kuhusu mali zetu kwa wenza wetu ni mbaya sana. Hali imekuwa ngumu sana upande wa huyu mama, ndugu wanalijua hili na wanamshawishi yeye aanze kumhojo mumewe, hajui hata aanze vipi.
 
Fuata ushauri wa Dero, muulize kwa kutumia ujanja; waweza mtaja rafiki yake kuwa amekuja kudai, mwambie unashindwa kujua kuwa ni kweli au la.

Nilipata shida nusu kuwa chizi ndugu yangu wa karibu alivyofariki; unaambiwa alitakiwa kusupply hiki na malipo alishachukua. Madeni yake hata ya uongo wanakuletea ila wadaiwa wake huwaoni.

Una dhamana kwa familia hivyo bora umuulize anyway.
 
Last edited by a moderator:
Huwezi muliza mtu akiwa kwenye hali hiyo,kwani alikua wapi alipokua mzima wa afya huyo mumewe?
na asisahau kua ya mungu anaweza akamuinua akaonekana mwanga wake,chamsingi amuachie mungu na amuombe afya njema.....
 
Mazoea yanatusumbua sana na tunayafanya maisha yetu kuwa magumu sana
"
Hapo kwenye hiyo ndoa kuna tatizo la kwanza ambalo watu wanatakiwa wajifunze.
"
Tatizo hilo ni kutokuaminiana.Unapokua unamuamini mwenzako ina maana kuwa utakua wazi kwake nae pia.Unapomficha mwenzako mambo yako huyo utakua unamchukulia kama mpita njia tu.Inakuaje mpaka mnaoana mnakua hamuaminiani?Mnafichana mambo?Haipendezi kabisa.
"
Kuhusu kumhoji,ni vyema huyo rafiki yako akajiuliza sababu iliyomfanya mumewe amfiche yote hayo.
"
Asipopata jibu,ajiulize kama kuna umuhimu wa yeye kujua mali hizo.
"
Ninavyosema haya ninamaanisha kuwa,huenda kukawa na tatizo kati ya wanandoa hao na kitendo cha kumuuliza kikazua mtafaruku.
"
Hebu fikiri kama mumewe alikua anadhani huyo mkewe amekubali kuolewa nae kwa sababu ya mali,unadhani atakapomuuliza si patachimbika?
"
Ndo maana nikasema ni bora akatafuta sababu ya yeye kufichwa mali hizo kwanza!
 
Hapo pagumu... Amuulize ila atumie ujanja, amwambie kwa kuwa utachukua muda hapa hospital basi niambie wadeni wako na biashara zako ili nisimamie au nimuulezeke mtu wa kusimamia maana la sivyo atamkatisha tamaa mgonjwa, huwezi jua Mungu mkubwa, anaweza kupona huyo so awe very carefully kwenye kuongea.

kaa humu.....
 
mkuu umetoa ushauri wa ukweli,naukubali,asante hope bibie apo ataufikisha
 
Huwezi muliza mtu akiwa kwenye hali hiyo,kwani alikua wapi alipokua mzima wa afya huyo mumewe?
na asisahau kua ya mungu anaweza akamuinua akaonekana mwanga wake,chamsingi amuachie mungu na amuombe afya njema.....

Imefika mahali tuache mazoea.Tujue kuwa kuna kifo na maisha.Kumuuliza mtu haimaanishi wewe ni mwanga wake na unataka afe,bali unachukua tahadhari kama jambo hilo litatokea.Na linaweza kutokea au lisitokee!Huo ni ukweli usiopingika!
 
Aisee, kumuuliza mswahili afu akipona hata waliokushauri watakuruka. Acha zipotelee mbali. Muangalie, mtunze. Mali kama umepangiwa utapata tu. Wacha hizo habari!
 
Aisee, kumuuliza mswahili afu akipona hata waliokushauri watakuruka. Acha zipotelee mbali. Muangalie, mtunze. Mali kama umepangiwa utapata tu. Wacha hizo habari!

Hivi dada,ni nani anapanga mtu kuwa na mali vile?
 
duh,hapo pagumu.wakimwuliza nduguzake atahisi wanatamani malizake,akimwuliza mkewe atahisi anampango wa kuchukua mali zote na anamtakia kifo.Mwambie atumie rafiki kipenzi wa mmewe amwambie kama story hivi,au viongozi wa dini kama yuko close nao waje kumsalimia then wamshauri(si mumlazimisha) kuandika husia.Kwa jamii za kibongo nyingi zimekutwa na matatizo ya mirathi,ajipigishe story ya watu fulani(ambao mume anawafahamu) amabao walipata shida(walikosana) kutokana na mali za marehemu kutokuwa zimeeandikiwa mirathi.Kwa mfano,unajua mamaXYZ sasa hivi anauza genge,ingawa mumewe alikuwa na mali nyingi ila hakuandika mirathi matokeo yake watoto wake wanapata shida.Fikiria but I hope kuna kitu umenielewa,onyo evaluate ushauri wangu na ufanyie marekebisho kama utaone unafaa.
 
wanaume sasa msipowaamini wake zenu kiasi cha wao kujua asset zenu mnawaamini kina nani jamani!

ona sasa mambo ya kuanza kuulizana vitandani ICU ''eti beby niliwahi kusikia kuwa una kampuni ya uwindaji ngorongoro file lake liko wapi?''uuuuwih hamad kabla hujamjibu vizuri unazidiwa anakutingishaje mabega sio ili upone hapana ili uendelee kumwelekeza zilipo mali zingine!
cha kutufanya tuonekane wachawi kwa mama zenu au dada zenu ni nini jamani!
kwa walio na hii tabia hebu jirekebisheni!
mke wako ni wewe ndani yake!hebu badilikeni jamani!

nishaona familia 2 zikipoteza mali na kurandaranda kwa tabia hii ya wanaume......
 
wanaume sasa msipowaamini wake zenu kiasi cha wao kujua asset zenu mnawaamini kina nani jamani!

ona sasa mambo ya kuanza kuulizana vitandani ICU ''eti beby niliwahi kusikia kuwa una kampuni ya uwindaji ngorongoro file lake liko wapi?''uuuuwih hamad kabla hujamjibu vizuri unazidiwa anakutingishaje mabega sio ili upone hapana ili uendelee kumwelekeza zilipo mali zingine!
cha kutufanya tuonekane wachawi kwa mama zenu au dada zenu ni nini jamani!
kwa walio na hii tabia hebu jirekebisheni!
mke wako ni wewe ndani yake!hebu badilikeni jamani!

Hapo nyumba ndogo huwa zinaambiwa ajenge ushosti na kimada cha mme wake waokoe mali.
 
Hivi snowhite na BADILI TABIA ,ni wanaume tu ndo wana tabia hii ya kutowaamini wanandoa wao?
"
Kwenye jambo hili,unaweza kukuta mwanamke mwenyewe ndo chanzo
"
Hata kama mwanamke sio chanzo,hiki sio kipimo cha kuwajumlisha wanaume wote.
"
Kufanya hivi ni kutokututendea haki!
 
nimeliexperience zaidi kwa wanaume.....
Hebu niambie jinsi gani mwanamke anaweza kuwa chanzo?

Maana nimeshuhudia wanaume wakishauriana seriously kuwa mwanamke asijue mali zao......

Nimeshuhudia familia ikipoteza mali zote za baba yao na kuponea kwenye kibanda cha mama yao.....

Nimeshuhudia familia ikidhulumiwa maana mume alimkabidhi rafikie mali akamficha mkewe........ Hata baada ya watoto kujua ukweli miaka kumi baadae its too late

familia ambazo baba na mama wako bega kwa bega ndo hufanikiwz.....hata kama hutaki mwenza wako ajiingize kwenye biashara au mali zako ni vyema ukampeleka ajue zilipo na hifadhi docs kwenye safe ubakie na password angalau likitokea la kutokea watachakachua na kufungua.....

Kuna baba akiwa mahututi alimwelekeza mkewe kwenye nyumba yao wahamie (walikuwa wamepanga uzunguni hali ya ugonjwa ilipozidi ikabidi wahame ili wasave wapate na fedha za kumuuguza) kwenye nyumba alojenga, alikuwa amemuweka nduguye, amini usiamini walifukuzwa kwa mapanga......ikabidi waende kwenye chumba na sebule alojenga mke, na mume alifia humo......... Mke na watoto hawakuabulia hata ndururu za mume/baba yao..... Marafiki wa mke ndo walimsaidia kumpa mtaji, baadae wakamtaftia kibarua aweze kusomesha watoto 7 alozaa na mumewe......
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom