"Ni bora kupata ukimwi kuliko mimba"

"Ni bora kupata ukimwi kuliko mimba"

HoneyBee

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
912
Reaction score
864
Nimesoma hii article mara 3, nimeishiwa nguvu:

Majivu yatumika kupanga uzazi na utoaji mimba Mbeya « JamiiForums|TMF Blogs

Tutafika kweli? Some other worrying quotes:

-Baadhi ya wanawake katika wilaya ya Mbeya Vijijini na Jiji la Mbeya wamekuwa wakitumia majivu kama njia ya kupanga uzazi na kutoa mimba zisizotarajiwa.

-Baadhi ya wanaume huwa hawapendi kutumia mipira (Condom) wakati wa kujamiiana hivyo baada ya tendo la ndoa wanalazimika kutumia njia hiyo kama moja ya njia rahisi ya kuzuia mimba kutotunga.

-Katika sayansi ya akili watu wanaojamiiana huwa wanatumia kinga mara ya kwanza na ya pili baada ya kuanza mahusiano na huwa hawatumii tena kinga baada ya kukutana mara ya tatu na nne na kuendelea.
(Warning kwa wanaopenda kavukavu)

-Ili kuepukana na kupata madhara ya kansa yanayoweza kutokana na majivu, huwa mtu akinywa basi siku hiyo anatakiwa kunywa maji kwa wingi ili kupunguza kemikali zitokanazo na majivu. (Hii ni sayansi ya wapi? Ukinywa sumu ukashushia maji mengi ina maana sumu inaisha makali??)

-Imebainika kuwa wauguzi wengi huwa hawatumii njia za kisasa za uzazi wa mpango licha ya kuendelea kuwashawishi wananchi wengine kutumia njia hizo kwa madai kuwa vidonge hivyo huwa wakimeza haviyeyuki.
(Ni dhahiri kuwa wauguzi hawana elimu ya kutosha kuelewa hivi vidonge vinavyofanya kazi. Huenda hii ni sababu kubwa wanawake wanasumbuliwa na matatizo mengi baada ya kutumia vidonge vya majira, au sindano.)
 
What!!!!!!!!!! Unautan na janga la taifa
 
elimu wanayo sana ila wanajua madhara yake ndo maana hawapendi ku2mia
 
Unashangaa majivu?hua wanatumia mpaka jiki ile ya kuondolea madoa kwenye nguo!

naongezea majani ya chai,mti wa kisamvu,dox,pamoja spoku ya baiskeli kwa bahati mbaya wote waliotumia njia hizi ninaowajua waliaga dunia kwa mtoto kufia tumboni ama kuoza kizazi,MUNGU ATUNUSURU KWA HAYA.kwa mimi heri mimba ukimwi unaua!
 
Kuna mdada mmoja anafanya kazi duka la dawa, akaniambia wanunuzi wakuu wa vidonge vya majira, ni wanafunzi wa shule haswa za sekondari, wao wanachoogopo ni "mimba" na sio kingine chochote, kwa sababu akishika mimba, itajulikana, atafukuzwa shule na maisha yataharibikia hapo!, lakini akipata "ukimwi", hawezi kujijua ameupata lini, kwa nani, hauna dalili yoyote wala haujulikani, hivyo ataendelea tuu na masomo yake, na mpaka ukimwi ujulikane, sio leo, sio kesho!, hivyo kwao kitu kinachoogopesha zaidi ni mimba na sio ukimwi!.

Masikini watoto wetu, dada zetu na mama zetu, na chanzo cha yote haya ni sisi wanaume!.

Pasco.
 
ah bora ngoma kuliko mtoto anakuja hapa duniani hapati malezi anaishia kuteseka tuu...huo ni ubinafsi. kwa nini mtoto ataabike nakuona dunia chungu? starehe yako weye iwe machungu kwa mtoto.
pata wewe mwenyewe ngoma ili utaabike mwenyewe na sio mtoto.
 
Imani ni kitu cha ajabu sana,

Hiyo ni imani waliyojiwekea kutumia majivu kama kinga ya mimba na dawa ya kutolea mimba.

Utashangaa hata hayo madhara wanayosema yanatokona na majivu, hayatawapata wanawake hao kutokana na imani waliyojiweka, kwamba wakinywa na maji basi itakuwa wamejikinga na madhara ya majivu.

SIKU ZOTE IMANI INAPONYA
.
 
Nimeogopa sana kusikia haya yanafanyika katika jamii yetu.
 
I get your point, Mzabzab. Lakini mbona ngoma na mimba zinaepukika (is this a word? lol)
 
Unaweza ukasema ni imani, lakini vilevile inawezekana ni bahati yao. Mwanamke anaweza kushika mimba pale tu yai linapopevuka. Inawezekana kila wakijamiiana ni siku salama na ni hilo linalowaokoa, lakini si kusema kwamba ni imani. Kuna vitu vingi sana vinavyosababisha kansa, kama kemikali kwenye chakula, kuvuta sigara n.k. Ukiwa na bahati utaepuka kansa lakini kitu kingine kikachukua uhai wako (ajali, kisukari), lakini bado kuna possibility utaugua kansa.

Kwanini watu watumie "imani" kuzuia mimba wakati kuna vidonge na njia salama kama kufata kalenda? Sijui ni uvivu au kutokuwa na elimu.

Imani ni kitu cha ajabu sana,

Hiyo ni imani waliyojiwekea kutumia majivu kama kinga ya mimba na dawa ya kutolea mimba.

Utashangaa hata hayo madhara wanayosema yanatokona na majivu, hayatawapata wanawake hao kutokana na imani waliyojiweka, kwamba wakinywa na maji basi itakuwa wamejikinga na madhara ya majivu.

SIKU ZOTE IMANI INAPONYA
.
 
Kwanini watu watumie "imani" kuzuia mimba wakati kuna vidonge na njia salama kama kufata kalenda? Sijui ni uvivu au kutokuwa na elimu.

Si kweli kwamba kila aliyekunywa kikombe cha Babu Loliondo hakupona maradhi yake!
Ile dawa ya babu ilikuwa ikiwatibu na kuwaponya kabisa wale tu waliyoiamini.
Hivyo waliopona ni IMANI YAO ILIWAPONYA.

Kama ulisoma vizuri utakumbuka kwamba hata Wauguzi wa hospitalini hawatumii njia hizi za kisasa ktk kupanga uzazi wakisema kwamba zina madhara ila ni hodari wa kuashauri wengine kutumia njia ya kisasa kama ya vidonge.

Njia bora na salama zaidi ni ya kalenda ila asilimia kubwa ya wananchi hawajui kuhesabu kalenda, kwahiyo tatizo hapa ni elimu.
Mimi binafsi natumia kalenda kupanga uzazi na mwenzi wangu na sijawahi kubugi meen.
 
Unashangaa majivu?hua wanatumia mpaka jiki ile ya kuondolea madoa kwenye nguo!

Kumbe na wewe ni mtumiaji mzure eeeh..........................................!:confused2:
 
Hongera kwetu cc waTz kwa uvumbuzi mwingi tulionao ya madawa ya kienyeji... Tunakipaji kikubwa sana!
 
Ohh Yeah, kimtaani taani
Tunaogopa sana mimba kuliko hata miwaya, tena sie fomu wani B?
Nikipata mimba mzee anifukuze home, na-deal na mimba kwanza ukimwi ARV nitatafuta baadae

Inahuzunisha lakini ndio ukweli wenyewe
 
Back
Top Bottom