Habarini wakuu.
Katika harakati za kujikomboa kiuchumi ninawaomba tujaribu kujuzana matumizi ya ndizi hasa zile za kupikwa.
Mbali na matumizi ya kawaida kama vile
1. Kupika
2. Kutengeneza mbege
3. Kutengeneza pombe n.k
Ninaomba tujuzane bidhaa zingine mbali na hizo katika harakati za kujiongezea kipato.
Waghana na Wanigeria wanachemsha green plantains kasha wanaponda kwenye kinu, inatokea ugali unavutika kama ugali wa mhogo, huliwa na mchuzi wa aina yeyote.