Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Ualimu wa watoto wa international schools tu (sio NECTA). Mtaji ilikuwa 400,000 kwa ajili ya matangazo ya awali. Tulifanya mauzo ya kama mil 20 katika kipindi kile.

Magroup ya Whatsapp. Mtaji simu na matangazo ya FB. Tulitumia kama 50k (niligundua njia ya kupata matangazo ya FB kwa almost free mwaka 2015). Tulianza mauzo 2016 June na tuna zaidi ya mil 150 mpaka sasa.
Duh ungefunguka mkuu
 
Watu wengi wanaamini wakiwa na pesa nyingi mtaji ndo watafanikiwa kibiashara, kitu ambacho Ni tofauti, unatakiwa upate wazo la biashara ambalo ndo utajiri wengi wasiojua, mfano unatakiwa kuwaza ni biashara ipi mfano naweza nikawekeza mtaji wa 200000 na kwenye hii laki 2, kila siku faida yangu ianzie 30000 tu kwa siku Kama starting point, ukiwa hujawahi au si mbobezi wa biashara usijaribu weka fedha nyingi kwenye trial never.

Kitu cha kwanza katika biashara kabla ya vitu vyote ni pesa.

Anza kuwaza pesa, pesa ndo itaamua ni biashara hipi unatakiwa huwe na hayo, baada ya pesa kuamua linakuja wazo, wazo kitatokana na uwezo wa kifedha uliyonao, wazo litakupa aina ya biashara yaani bidhaa ambayo unaona hii watu watakuelewa mwisho ni masoko.

Business secret
1.Finacial support
2.Great products
3 market

Kumbuka wazo la biashara liendane na uchumi wako, kwaiyo pesa kwanza.
 
Mchawi ni ku Brainstorm tu anza General kuangalia Sector(Industries) zote chambua moja baada ya nyengine mpaka utapata kitu kimoja then kakifanyie Field Study.

Hakuna kitendawili hapo mtaji wa 250K mkubwa sana kukupa 1M kwa mwezi na ikawa 3M ndani ya miezi mitatu.

Kuna jamaa kariakoo ukiangalia mtaji wao hauzidi 100K wanfikisha hiyo 1M+ kwamwezi...katika field observation nilizofanya ndani ya dakika 20 nilizokuwa napata huduma hapo wameingiza mauzo ya 5000 na bidhaa 50+ zipo prepared kuuzwa, bidhaa wanayouza ina Profit margin ya ½ kwa ½ na mtaji.

Mimi kwasasa nimeamua kukaa kimya nitapaza sauti nitapojenga misuri yangu zaidi.
Biashara gani hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeuza viazi vya mafungu na kwenye sado pale Temeke sterio sokoni hapo nipo chuo UDSM mwaka wa pili dah halafu najishangaa hata nilikuwa sioni haibu.. lakini leo marafiki zangu ndio wanaulizia ile biashara maana ninayofanya saivi ni tofauti na matarajio yao. Thanks god kwa kidogo ninachopata.
Nilivyo soma jina tu SANGA nikapita kushoto chap, mkinga si mtu wa kushindana nae.
 
Kwenye hiz Moshe kikubwa ni kuwa na wazo qonk ......na kufanya investigation ya kutosha kuhusu kitu unachotaka kukifanya

Then kumpata mtu sahihi wa kusimamia project zako
Mfano mm npo chuo mwaka wa kwanza hapa Mbeya town. Baada ya kumaliza form six nlifanya kautafiti kidogo niliona hapa town nyama inatumika kwa kiasi kikubwa so na broo angu tuli plan kuanza ufugaji wa nguruwe ambapo tulichanga pesa tukanunua mkubwa then. Navoingia first year nguruwe alizaa vitoto 11 ..mwez wa tatu ..na tuliamua kufuga vyote then mwez wa saba huu tumepiga pesa heavy kila mtu kashika zake mfukoni

But from mwakan nta expand naanza kufuga vidume vya ng'ombe wa kisasa ....

Pumba + plus mashudu ndan ya miez minne. Unapga pesa ndefu

Kikubwa ......Fanya research na umpate mtu wa kusimamia .....lkn pia uwe karibu na project zako. Thats y chuo nlichagua karibu ili kuendleza projects. Zangu
NGURUWE MLINUNUA BEI GANI MKUU?

vp kuhusu gharama za kuwatunza mpaka kuja kuwauza?
 
Kupitia Uzi huu Kama Kuna mtu yupo dar na anataka tushirikiane kwenye biashara ya ujasiriamali ikiwemo :

Kuuza maziwa fresh /mtindi

Kuuza chakula

Chips..

Nipo tayari zama dm nikupe contact zangu
Uko pande za wapi mdau mi Niko toangoma
 
Mkinga bwana anaweza kuanza kuuza maji ya kandoro baada ya mwaka tu unakuta anamiliki duka la jumla kariakoo wanamiujiza yao hawa watu
Hivi inakuwaga discipline yao au wanstumia zaidi mafusho ya kiganga kutoboa?
 
Hivi inakuwaga discipline yao au wanstumia zaidi mafusho ya kiganga kutoboa?
Kabla ya mganga kwanza inabidi vitu vyote muhimu kwa ustawi wa biashara viwepo.
Mganga hawezi kufanya maajabu kama huna mtaji

Mganga hawez kufanya maajabu kama upo location mbaya.

Mganga hawezi kufanya maajabu kama unafungua dukani saa 4 na sa 12 umeshafunga.

Kazi ya mganga ni kulainisha tu mambo.
 
Back
Top Bottom