Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
2,345
4,168
Ndugu zanguni mawazo ndio benki kuu kabisa ya kila wazo unalotaka kufanya, basi kwa uzoefu wa waliopitia changamoto fulani za kiuchumi na kijasiriamali ni vyema mngetushirikisha biashara ndogo ambazo mlizibuni na maeneo mlikofanyia hizo shughuli zenu hadi mkafikia hatua ya mafanikio mliyo nayo sasa.

Tunatarajia ushuhuda, miongozo na shauri zenu zitusaidie nasi kujikwamua hapa tulipo ili nasi tusogee mahali fulani.

1619511108732.png
 
Nimeuza viazi vya mafungu na kwenye sado pale Temeke sterio sokoni hapo nipo chuo UDSM mwaka wa pili dah halafu najishangaa hata nilikuwa sioni aibu.. lakini leo marafiki zangu ndio wanaulizia ile biashara maana ninayofanya saivi ni tofauti na matarajio yao. Thanks god kwa kidogo ninachopata.
 
Biashara ya chakula...sembe kilo 1 linatoa plate 9_10... Dona linatoa plate 7

Sasa ukatafuta kijiwe ukaspeciliaze kwenye uchomaji nyama mzuri plus mapande...ukatengeneza formula nzuri ya pilipili..yaan ni ugali na nyama na mboga majani na maharage...kwasiku unalaza 20 faida...ila wateja wa dona bei sio ya buku...maana dona halivimbi ni hasara kibiashara...
 
Watu wengi wanaamini wakiwa na pesa nyingi mtaji ndo watafanikiwa kibiashara, kitu ambacho Ni tofauti, unatakiwa upate wazo la biashara ambalo ndio utajiri wengi wasiojua, mfano unatakiwa kuwaza ni biashara ipi mfano naweza nikawekeza mtaji wa 200,000 na kwenye hii laki 2, kila siku faida yangu ianzie 30,000 tu kwa siku Kama starting point, ukiwa hujawahi au si mbobezi wa biashara usijaribu weka fedha nyingi kwenye trial never.
 
"Mtaji wake ni mdogo" ni kama kiasi gani mkuu?,
Walau milioni 3 kwa kiwango cha chini. Photocopy machine, printer, lamination machine, stapler kubwa/ndogo, desktop iliyo kamilika/laptop, nk.

Baada ya hapo ndiyo uje sasa kwenye vitu vidogo vidogo! Na hapo ni nje ya kabati na shelf! Kudadeki hata hizo milioni 3 zenyewe hazitoshi.

Ila ukishakamilisha kuianzisha na kumpata kijana mzuri wa kuisimamia! Hakika utakua unakula tu mafao. Ni biashara moja nzuri sana.
 
Walau milioni 3 kwa kiwango cha chini. Photocopy machine, printer, lamination machine, stapler kubwa/ndogo, desktop iliyo kamilika/laptop, nk.

Baada ya hapo ndiyo uje sasa kwenye vitu vidogo vidogo! Na hapo ni nje ya kabati na shelf! Kudadeki hata hizo milioni 3 zenyewe hazitoshi.

Ila ukisha kamilisha kuianzisha na kumpata kijana mzuri wa kuisimamia! Hakika utakua unakula tu mafao. Ni biashara moja nzuri sana.
Ni ukweli mkuu million 3 haziwezi kutosha kwa biashara ya stationery. Ukianzia kwenye photocopy Machine hadi kwenye vitendea kazi vingine inakuja pesa nyingi tu, labda ujibane utafute vitu used/ second hand.

Na kama unataka kupanga kwenye mzunguko mkubwa wa watu, kodi ya fremu nayo huwa kubwa.

Yawezekana mtu akaanza kwa hiyo 3 mil lakini si kwakutoa huduma zote zinazopatikana stationery.
 
mkuu hebu nipe madini kidogo hapa, ukiwa Wakala wa premierbet na kampuni zingine commission zao zikoje.
Premier bet buku saba unapata ukiuza laki moja.....sasa hivi raia hawana hela mie nilikuwa nauza laki nne per day mpaka tano wikiend sasa ndio balaa nagonga laki nane mpaka 1M.......nilikuwa na mashine mbili moja ya vibosile kuanzia mkeka wa buku kumi na kuendelea hawa walikuwa balaa mtu anakuja na laki tatu anatoa mkeka mmoja tu mashine nyingine ya hawa wenzangu na mie mikeka ya jero buku mpaka buku tisa.....

Nilikuwa nafunga kijiji balaa pale mtaani nikikosekana masaa tu natafutwa kwenye simu na wafanya biashara wa lile eneo huwa wananiambia nasie tunauza vinywaji na vyakula sana kupitia wewe mimi mwenyewe sikuwahi kuwaza kabisa kama kuwa kwangu pale ni faida kwa wengine......

Nilisoma chuo miaka mitatu kupitia ile biashara nilimaliza 2015 kizaazaa alipoingia huyu bwana, wateja wakaanza kupungua mdogo mdogo mwishowe hakuna kabisa umeuza sana laki tena wikiendi kufika 2017 mwishoni nikafunga rasmi biashara........
 
Kuna jamaa Kariakoo Agrey mitaa ya wauza simu. Wasambaa wale dadeki ugali pande buku 2, wanaweka na vikabichi na pilipili. Mnagombania yaani foleni unakula Hadi umesimama. Siku hizi sina mishe kule Ila najua watakuwa mbali sana.
Biashara ya chakula...sembe kilo 1 linatoa plate 9_10...
Dona linatoa plate 7
Sasa ukatafuta kijiwe ukaspeciliaze kwenye uchomaji nyama mzuri plus mapande...ukatengeneza formula nzuri ya pilipili..yaan ni ugali na nyama na mboga majani na maharage...kwasiku unalaza 20faida...ila wateja wa dona bei sio ya buku...maana dona halivimbi ni hasara kibiashara...
 
Kuna jamaa kariakoo agrey mitaa ya wauza simu.wasambaa wale dadeki ugali pande buku 2,wanaweka na vikabichi na pilipili.mnahombania yaani foleni unakula Hadi umesimama. Siku hizi sina mishe kule Ila najua watakuwa mbali sana
Sure..wengine walikuwa hapa nyuma ya ghorofa ya China town sijui. Uwii wanauza mnoo. Hata ukitaka kwa 1500 bado inalipa..mradi uhakikishe unauza zaidi ya plate 50...
 
Premier bet buku saba unapata ukiuza laki moja.....sasa ivi raia hawana ela mie nilikua nauza laki nne per day mpaka tano wikiend sasa ndio balaa nagonga laki nane mpaka 1M.......nilikua na mashine mbili moja ya vibosile kuanzia mkeka wa buku kumi na kuendelea hawa walikua balaa mtu anakuja na laki tatu anatoa mkeka mmoja tu mashine nyingine ya hawa wenzangu na mie mikeka ya jero buku mpaka buku tisa.....nilikua nafunga kijiji balaa pale mtaani nikikosekana masaa tu natafutwa kwenye simu na wafanya biashara wa lile eneo huwa wananiambia nasie tunauza vinywaji na vyakula sana kupitia wewe mimi mwenyewe sikuwahi kuwaza kabisa kama kuwa kwangu pale ni faida kwa wengine......
Nilisoma chuo miaka mitatu kupitia ile biashara nilimaliza 2015 kizaazaa alipoingia huyu bwana wateja wakaanza kupungua mdogo mdogo mwishowe hakuna kabisa umeuza sana laki tena wikiendi kufika 2017 mwishoni nikafunga rasmi biashara........
Kama hivyo commission ni ndogo mno.

Hili African Bonanza/ dubu katika kila 60,000 ya kwako 9000 na bado mi nikaona ni hela ndogo nikatemana nalo.
 
Kuna jamaa kariakoo agrey mitaa ya wauza simu.wasambaa wale dadeki ugali pande buku 2,wanaweka na vikabichi na pilipili.mnahombania yaani foleni unakula Hadi umesimama. Siku hizi sina mishe kule Ila najua watakuwa mbali sana
Umesema Wasambaa? Oohh hao watakuwa mbali.
 
Premier bet buku saba unapata ukiuza laki moja.....sasa ivi raia hawana ela mie nilikua nauza laki nne per day mpaka tano wikiend sasa ndio balaa nagonga laki nane mpaka 1M.......nilikua na mashine mbili moja ya vibosile kuanzia mkeka wa buku kumi na kuendelea hawa walikua balaa mtu anakuja na laki tatu anatoa mkeka mmoja tu mashine nyingine ya hawa wenzangu na mie mikeka ya jero buku mpaka buku tisa.....nilikua nafunga kijiji balaa pale mtaani nikikosekana masaa tu natafutwa kwenye simu na wafanya biashara wa lile eneo huwa wananiambia nasie tunauza vinywaji na vyakula sana kupitia wewe mimi mwenyewe sikuwahi kuwaza kabisa kama kuwa kwangu pale ni faida kwa wengine......
Nilisoma chuo miaka mitatu kupitia ile biashara nilimaliza 2015 kizaazaa alipoingia huyu bwana wateja wakaanza kupungua mdogo mdogo mwishowe hakuna kabisa umeuza sana laki tena wikiendi kufika 2017 mwishoni nikafunga rasmi biashara........
Hata mimi nilikuwa nayo nikairudisha...tech ilivyokua watu wengi walihamia online, mambo ya kutembea na makaratasi wakaachana nayo.
 
Back
Top Bottom