Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

LaRosa

JF-Expert Member
Jul 3, 2020
679
1,000
Kuna biashara uchwara nimeifugua Zanzibar mtaji laki 2 na nusu, lakini hadi sasa Nimetengeneza zaidi ya milion tatu kwa siku kadhaa tu na kila siku nalaza faida ya laki Kama net profit.

Hela hata sipeleki benki natunza chini ya kapeti tu. Leo ndo napeleka benki milion 2.

I'm happy

DSC_0703.JPG
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,336
2,000
Biashara ya chakula...sembe kilo 1 linatoa plate 9_10.
Dona linatoa plate 7
Sasa ukatafuta kijiwe ukaspeciliaze kwenye uchomaji nyama mzuri plus mapande...ukatengeneza formula nzuri ya pilipili..yaan ni ugali na nyama na mboga majani na maharage...kwasiku unalaza 20faida...ila wateja wa dona bei sio ya buku...maana dona halivimbi ni hasara kibiashara.
Hii idea nilikuwa nayo jana tu hapa. Nilitaka kuweka laki 6 kwenye kakibanda ka chips baada ya kufatilia nikaona miyeyusho kwanza vibanda vingi na chips zina usumbufu. Nikafikiri nikiweka pungufu ya hiyo kwenye kibanda cha mamantilie si napata hela ingawa siwezi kamwe kufanya hiyo kazi mpaka niweke wadada.

Bado niko dilemma.
 
Torque vs HP

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
1,774

Biashara yoyote ile nisiyo na ufahamu nayo kimtindo na isio na usimamizi wangu siwezi kuifanya kamwe.
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,336
2,000
Kuna biashara uchwara nimeifugua Zanzibar mtaji laki 2 na nusu, lakini Hadi sasa Nimetengeneza zaidi ya milion tatu kwa siku kadhaa tu na kila siku nalaza faida ya laki Kama net profit.

Hela hata sipeleki benki natunza chini ya kapeti tu. Leo ndo napeleka benki milion 2.

I'm happy View attachment 1722606
Uzi unakuomba utaje jina la biashara. Au unaogopa copyright issues
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,336
2,000
Biashara yoyote ile nisiyo na ufahamu nayo kimtindo na isio na usimamizi wangu siwezi kuifanya kamwe.
Niko chuo sina muda mwingi wa kukaa mtaani. Kila biashara ninayofikiria inataka muda wangu mwingi. Nina options mbili, either nimuamini mtu nimkabidhi biashara badala yangu, au nisimamie kazi ila operations zote ziwe mikononi mwa anayefanya kazi.

Nishapoteza hela nyingi kula bata kwa sababu ya kufeli katika uchaguzi wa options hizi nikapata hasara na kukata tamaa ya kuwekeza.
 
RReigns

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
16,980
2,000
Kuna biashara uchwara nimeifugua Zanzibar mtaji laki 2 na nusu, lakini Hadi sasa Nimetengeneza zaidi ya milion tatu kwa siku kadhaa tu na kila siku nalaza faida ya laki Kama net profit.

Hela hata sipeleki benki natunza chini ya kapeti tu... Leo ndo napeleka benki milion 2.

I'm happy View attachment 1722606
Embu fafanua mkuu biashara gani hiyo.
 
Torque vs HP

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
1,774
2,000
Niko chuo sina muda mwingi wa kukaa mtaani. Kila biashara ninayofikiria inataka muda wangu mwingi. Nina options mbili, either nimuamini mtu nimkabidhi biashara badala yangu, au nisimamie kazi ila operations zote ziwe mikononi mwa anayefanya kazi.

Nishapoteza hela nyingi kula bata kwa sababu ya kufeli katika uchaguzi wa options hizi nikapata hasara na kukata tamaa ya kuwekeza.
Sasa hivi unaenda kubadilisha tu namna hela yako inavyoenda kupoteza badala ya kuipoteza kwny bata unaenda kuipoteza kwny kupeleka pesa kwny kiti usicho na usimamizi nacho.
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
35,048
2,000
Hii idea nilikuwa nayo jana tu hapa. Nilitaka kuweka laki 6 kwenye kakibanda ka chips baada ya kufatilia nikaona miyeyusho kwanza vibanda vingi na chips zina usumbufu. Nikafikiri nikiweka pungufu ya hiyo kwenye kibanda cha mamantilie si napata hela ingawa siwezi kamwe kufanya hiyo kazi mpaka niweke wadada.

Bado niko dilemma.
Hv ujasiri wa kuwekaga wadada mnaupata wapi? Au la awe my wife wako...ww unakaz zingine?..hizi mishe piga mwenyewe saidiana na wenzako muwe 3..kwisha habari..yaan msichana awe wa kuosha vyombo na kupika greens
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
35,048
2,000
Sana.siku moja nimechukua sahani nimepeleka jikoni jamaa anaweke ugali nikakuta sufuria la kg 20 wanapikia ugali.halafu Ile biashara hakuna kuhudumiwa yaani wewe fika chagua pande muoneshe mgosi Yule ,kamata plate nenda jikoni weka ugali wako ,nawa nje pale utasaidiwa Ile nyama ikatwe Tu basi
Chakula cha hvo kinakuaga very tastey
 
Ngosha Mashine

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
534
1,000
Walau milioni 3 kwa kiwango cha chini. Photocopy machine, printer, lamination machine, stapler kubwa/ndogo, desktop iliyo kamilika/laptop, nk.

Baada ya hapo ndiyo uje sasa kwenye vitu vidogo vidogo! Na hapo ni nje ya kabati na shelf! Kudadeki hata hizo milioni 3 zenyewe hazitoshi.

Ila ukisha kamilisha kuianzisha na kumpata kijana mzuri wa kuisimamia! Hakika utakua unakula tu mafao. Ni biashara moja nzuri sana.
Kumbe milioni 3 ni mtaji mdogo? biashara kama ya kuuza mihogo, viazi kwa mafungu haizidi laki 2 au hata kuku wa kienyeji haizidi laki tano,, ww unaleta biashara za mamilion
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,336
2,000
Sasa hivi unaenda kubadilisha tu namna hela yako inavyoenda kupoteza badala ya kuipoteza kwny bata unaenda kuipoteza kwny kupeleka pesa kwny kiti usicho na usimamizi nacho.
Basi bora nile maisha na manzi yangu as long as nakusanya elimu ya mazingira nikiwa free nitafanya. Sio kuwa ndio naenda kupoteza, nishapoteza 1.2M kwa kutosimamia. Niliambulia kuokoa laki 5 kasoro

Kwa kiasi flani nimeibukia kwenye savings, tatizo hela nayoweka ni ndogo naona bora niiwekeze ikue ila ndio vitasa napokea. Nikisema nisikate tamaa nazidi kupoteza hela
 
hnp

JF-Expert Member
Dec 4, 2020
216
500
Biashara yangu ina copyright issues hivyo samahani jamani sitaitaja maana naifanya mwenyewe tu huku Zanzibar watu wengine bado hawajapata mechanism ya kucopy.

Na soon baada ya wao kucopy nahamia kwenye phase 2.

Mtanisamehe!
Najaribu kuitafakari iyo biashara akili inagoma kabisa. Kibaya zaid sijapata biashara nzuri ya mtaji mdogo niifanye toka mwaka uanze,eeh Mungu nisaidie !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,336
2,000
Hv ujasiri wa kuwekaga wadada mnaupata wapi? Au la awe my wife wako...ww unakaz zingine?..hizi mishe piga mwenyewe saidiana na wenzako muwe 3..kwisha habari..yaan msichana awe wa kuosha vyombo na kupika greens
Kuoa mimi sio leo wala kesho. Ndo kwanza niko chuo nina ghetto hasahasa namiliki jeans na raba hakuna kingine. Muda wa kufanya kazi sitopata, kusimamia sawa ila sio kukaa.
Hapa yenyewe nina UE jioni niko nazima moto
322baa103ae747f3951a703fd31a8216.jpg
 
Attachments

  • IMG20210311112410.jpg
    File size
    76.4 KB
    Views
    0

Torque vs HP

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
1,774
2,000
Basi bora nile maisha na manzi yangu as long as nakusanya elimu ya mazingira nikiwa free nitafanya. Sio kuwa ndio naenda kupoteza, nishapoteza 1.2M kwa kutosimamia. Niliambulia kuokoa laki 5 kasoro

Kwa kiasi flani nimeibukia kwenye savings, tatizo hela nayoweka ni ndogo naona bora niiwekeze ikue ila ndio vitasa napokea. Nikisema nisikate tamaa nazidi kupoteza hela
Usimamizi ni kila kitu mkuu, hakuna mtu anae enda kukutengenezea pesa huku wewe ukiwa kwny mishe zako nyingine mzee.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom