Kwa iPhone 4, 4s, 5....
1. Ringtones --- hii app ni maalumu kwa ajili ya kuset customised ringtones. Ila ni lazima uwe na iTunes katika PC yako ili uweze kutumia app hii. Kwa wale wanaopenda kupersonalise ringtones, basi hii app ni bab kubwa.
2. RedLaser --- hii app ni kwa ajili ya kufahamu details za bidhaa mbalimbali zenye barcode. Ni poa kama unataka pia kufahamu kama bidhaa fulani ni genuine ama kanyanga.
3. Camera360 --- kwa wapenzi wa kupiga na kuedit picha, hii app ni bab kubwa. Kuna watu zaidi ya milioni 100 duniani wanatumia app hii! Unaweza ukaedit picha kwa styles mbalimbali. Unaweza kuimport na kuexport picha kutoka kwenye apps nyingine za picha unavyotaka.
4. Units Plus --- hii ni kwa ajili ya kufanya conversions za area, power, currency, length, fuel mileage, pressure, speed, time, weight n.k.
5. PS Express (Adobe photoshop express) --- hii ni kwa ajili ya kuedit picha unavyotaka..
6. Essentials (how to cook everything) --- hii ni kwa wapenzi wa kuandaa mahunjumati. App inatoa maelekezo ya kuandaa na kupika. Kuna recipes za aina ya misosi kama 15 hivi zilizo na vijirecipes vingi tu ndani yake.
7. Home --- hii ni kwa ajili ya kujifunza namna bora ya kuandaa na kupamba ndani mwa nyumba. Ipo poa sana hii app. Inakufanya unakuwa interior designer bila kulipia chochote (zaidi ya pesa ya bundle).
8. RunKeeper --- hii ni kwa wapenda mazoezi ya kukimbia. Itakusaidia kutambua umbali uliokimbia, njia uliyotumia, calories ulizochoma, spidi uliyotumia n.k. Ila inafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya GPS. Unaweza ukapanga na kuweka historia ya ukimbiaji wako na kuwaonyesha marafiki kupitia Facebook na Twitter.
9. DHL ACT --- hii ni kwa ajili ya kutrack/kutrace mzigo wako uliosafirishwa na DHL.