Tanzania Tech
JF-Expert Member
- Dec 8, 2016
- 355
- 276
Habari wana JF, Natumain wote humu mko salama kabisa. Leo tulikuwa tunatafuta app nzuri za kitanzania za kushiriki na wasomaji wetu wa tovuti ya Tanzania Tech, lakini kwa haraka haraka hatujafanikiwa kupata App nyingi kutokana na kuwepo kwa Apps nyingi sana kwenye soko la Play Store.
Sasa basi, tunaomba msaada wenu au kama wewe ni mmiliki wa App yoyote ya android ambayo unahisi inaleta mchango fulani wa maana kwa jamii basi unaweza kushare hapa na sisi tutashiriki app hizo kwenye tovuti yetu na App yetu ya Tanzania Tech.
Natumaini hii itasaidia pia hata kwa hapa JF, kwani wengi wetu tunatumia Apps zinazo tengenezwa na wabunifu kutoka nje ya Tanzania na tunasahau kuwa hata watanzania wanaweza.

- Kifupi App yako inatakiwa iwe ina mchango wa maana kwenye jamii hasa ya Kitanzania na iwe inafanya kazi kikamilifu.
- Kitu kingine unaweza kuweka maelezo kidogo Jinsi App hiyo inavyofanya kazi ikiwa pamoja na link yake kwenye soko la Play Store.
- Kingine kama app yako haiko kwenye soko la Play Store basi unaweza kuweka link ya file la apk lakini hakikisha app yako ni salama na haina malware au virus.
Natumaini hii itasaidia pia hata kwa hapa JF, kwani wengi wetu tunatumia Apps zinazo tengenezwa na wabunifu kutoka nje ya Tanzania na tunasahau kuwa hata watanzania wanaweza.