Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,355
- 2,767
Teknolojia ya Tanzania inazidi kupiga hatua! ๐น๐ฟ๐
Anaitwa Emmanuel Mpyambala, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), amebuni mfumo unaoitwa VexGuard Anti-Theft System, unaolenga kusaidia kufuatilia simu zilizopotea au kuibwa.
๐ Mfumo huu umetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia kutambua eneo la simu kupitia GPS, kufunga kifaa kwa mbali na kuweka taarifa za mawasiliano ya mmiliki ili kurahisisha kurejeshwa kwa kifaa.
Mfumo huu unafanya kazi vipi?
๐ฑ Simu ikipotea au kuibwa Unaweza kutumia simu ya ndugu au rafiki kujaribu kufikia taarifa za kifaa chako.
๐ Kuingia kwenye akaunti kupitia kupakua app husika kupitia Google Play Store na kuingia kwa akaunti iliyokuwa ikitumika kwenye simu iliyopotea.
๐ Kutambua vifaa kwa kuonyesha vifaa vilivyowahi kuunganishwa na akaunti hiyo, kulingana na maelezo yaliyotolewa kuhusu uvumbuzi huo.
Vijana wa Tanzania wanaibadilisha dunia kwa teknolojia! ๐น๐ฟ๐ ๐ Je, ungeitumia teknolojia hii?
#bongotech255