Ni akina nani wenye haki ya kupishwa barabarani?

IGADESA

JF-Expert Member
Jan 15, 2021
295
721
Habari wadau!

Kuna wimbi la madereva wa magari aina ya Land Cruiser kutanua barabarani huku wakiwasha vitaa vya vimwelu mwelu kuashiria wapishwe. Je, huu ni utemi? Na je, kina nani kwa miaka ya sasa wanaoruhusiwa kupishwa bila kuwekwa pembeni na trafiki polisi?

Au ndio " unanijua mimi nani" wameanza kurudi?
 
Wameanza kurudi lini?

Hii kitu ilikomaa wakati wa JPM ndo kila gari DFP,SU,SM,STK zote waliweka vimulimuli wanataka hiyo privilege.

Hadi Land Cruiser za katibu wa CCM wilaya(Mkonge zile) zinatanua siku hizi.

Nilimsikia Muroto RPC Dom alianza kuwakamata madereva wa serikali wanaoweka vimulimuli kinyume na utaratibu.

Wengine walikua wanapita hadi njia ya mwendokasi wakikamatwa wanampigia simu Mambosasa akawaruka kuwa hata yeye hatumii hiyo njia

Hii nchi ubabe tu
 
Jana tumepishana nazo ikatubidi mda wote tutoke nje ya barabara maana isije kujirudia zama za Dito mtu akapigwa cha moto kisa kupishana.
 
A motorcade (or convoy, carcade, autocade) is a number of vehicles driving in the same direction on official business.

Hii kisheria na Protocol inahusisha watu wafuatao
1. Rais
2. Makamu wa Rais
3. Waziri Mkuu
4. CDF

Wengine kama IGP, SPIKA, CIG, CS, CGP ni mbwembwe tu PLUS wakuu wa taasisi za Umma, hawa wanaponzwa na madereva wao wanaojifanya wanaharaka.
 
Jana tumepishana nazo ikatubidi mda wote tutoke nje ya barabara maana isije kujirudia zama za Dito mtu akapigwa cha moto kisa kupishana...
Na ili mtu apishwe(msafara) kiutaratibu ni lazima kuwe na kimulimuli(flashlights) na king'ora(siren) ili kutaarifu madereva wengine toka mbali kwa sauti kabla hata hajaona mwanga

Sasa hawa wa naweka vimulimuli vidogo pale wanawasha na taa tu basi unashitukia huyu hapa katanua hovyo. Ni kutafutana ubaya tu

Na watu wengi sana wameumizwa kwa huo ujinga
 
Back
Top Bottom