awamu3imetulimaza
New Member
- Jul 2, 2006
- 1
- 1
Mkono awashushua wenyeviti halmashauri
na Charles Mullinda
MBUNGE wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, amewashushia tuhuma nzito wenyeviti wa halmashauri za wilaya ilimo migodi ya dhahabu inayoendeshwa na Kampuni ya Barrick Gold Tanzania kwa kukubali kupokea kodi ya sh milioni 240 kwa mwaka.
Amesema kitendo walichokifanya kimewadhalilisha na kuonyesha jinsi walivyo waroho na wasivyofikiria juu ya athari zinazosababishwa na wawekezaji hao wanapochimba madini.
Ni ujinga mtupu uliofanyika; yaani walipoona pesa, bila kufikiri wakakubali kuzichukua, alisema.
Mkono aliyasema hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima kwa simu kuhusu hatua ya Kampuni ya Barrick Gold Tanzania kuanza kulipa kodi ya dola za Kimarekani 200,000 sawa na sh milioni 240 kila mwaka kwa halmashauri hizo za wilaya.
Alisema kabla ya kuamua kuzichukua fedha hizo, kulikuwa na ulazima wa kukaa chini na kuangalia uharibifu wa mazingira unaosababishwa na kampuni hiyo, sambamba na kuangalia faida wanayoipata wawekezaji hao kama inalingana na kodi wanayotoa.
Kulikuwa na ulazima wa kukaa chini na kuangalia jinsi mazingira yanavyoharibiwa, mashimo yanayoachwa baada ya kuchimba, pale kwangu katika mgodi wa Buhemba kuna vifusi vinalingana na mlima. Je, hiyo pesa wanayotoa kwa halmashauri itatosha kufukia kifusi hicho?
Katika kazi zao, wanatumia vijana wetu ambao wamesoma, hakuna mtu ambaye hana elimu pale. Je, wanachangia nini katika elimu? Hizo fedha wanazotoa zitasaidia katika elimu? Na si elimu tu, barabara, maji na mambo mengi ya maendeleo, alisema Mkono.
Mbunge huyo alisema kampuni hiyo inatumia vijana wa Kitanzania ambao wamesomeshwa na Watanzania bila kuchangia chochote katika elimu; wanatumia barabara na huduma nyingine za muhimu zilizotokana na jasho la wananchi wa kawaida, huku wakivuna faida kubwa.
Alisisitiza kwamba sh milioni 240 kwa mwaka zilizoanza kutolewa na Kampuni ya Barrick hazitoshi kwa sababu kazi ya kufukia mashimo yaliyotokana na uchimbaji wa dhahabu itahitaji mabilioni ya fedha.
Nasisitiza ni lazima tuelewe ni kiasi gani cha madini wanachimba na kuchukua kuondoka nayo ili tupime na sisi kiasi kinachostahili watupatie.
Kuweka wastani wa sh milioni 240 kwa migodi yote, ni upuuzi kwa sababu kuna sehemu ipo dhahabu nyingi kuliko kwingine, sasa kwanini iwe kiasi hicho hicho? alihoji Mkono.
Alisema kama hoja hizo zingezingatiwa, hata Rais Jakaya Kikwete asingekuwa na sababu ya kwenda kuomba ufadhili kwa ajili ya kujenga chuo kikuu hapa nchini.
Dhahabu ilikuwepo siku nyingi, lakini ilitunzwa na kuwekewa ulinzi kwa makusudi ili ije isaidie ujenzi wa nchi yetu na maendeleo kwa ujumla, hivi hata wewe unaona ni jambo zuri kwa rais wetu kwenda kuomba ufadhili wa kujengewa chuo kikuu wakati kuna dhahabu lukuki hapa nchini? alihoji Mkono.
Alitahadharisha viongozi kuwa makini katika kutetea maslahi ya wananchi ili kujiepusha na migogoro ambayo inazikumba nchi nyingine zenye utajiri wa asili kama uliopo Tanzania.
Alitoa mfano wa nchi za Nigeria na Afrika Kusini, ambako kuna machafuko ya kila mara katika maeneo yenye migodi, kwamba yanasababishwa na uonevu wa wawekezaji kwa wananchi ambao ndio wenye mali.
Aidha, Mkono alisema Kampuni ya Barrick inapaswa kushitakiwa kwa kukiuka mkabata wake wa uchimbaji madini ilioingia na serikali.
Alisema Barrick haipaswi kusamehewa kwa kuwadhulumu Watanzania iliotakiwa kuwalipa mrahaba kupitia halmashauri zao za wilaya kwa mujibu wa mkataba, na pia inapaswa ieleze waziwazi imekuwa ikikiuka mkataba wake kwa miaka mingapi.
Mkono alisema mtu yeyote anayevunja sheria ni budi afikishwe mbele ya sheria, jambo ambalo linapaswa kufanyika kwa Kampuni ya Barrick ambayo imedhihirisha kuwa ilikuwa ikivunja mkataba wake kwa kutolipa kodi ambayo iko kwenye mkataba wake tangu ilipoanza shughuli za kuchimba madini hapa nchini.
Kulingana na mikataba ya wawekezaji hao, kodi ya dola 200,000 ilitakiwa kulipwa kwa halmashauri za wilaya husika baada ya kutunga sheria ndogo kuhusu suala hilo, lakini kutokana na usiri uliokuwapo katika mikataba hiyo, hazikuweza kutambua suala hilo.
Hivi karibuni, Kampuni ya Barrick Gold Tanzania ilitoa sh milioni 240 kwa kila halmashauri, ambako imewekeza migodi yake. Fedha hizo zilikabidhiwa kwa wenyeviti wa halmashuri husika katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma Juni 14.
Mkono alionyesha kutokubaliana waziwazi na hatua hiyo baada ya kususia hafla ya kukabidhiwa fedha hizo na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa hili lilikuwa tukio chafu ambalo hakuwa tayari kulishuhudia likifanyika mbele ya macho yake.
Mkono alikaririwa na waandishi wa habari akieleza kwamba kiwango hicho ni kidogo na kukubali kukipokea, ni kujitia kitanzi kwa sababu kisheria ukipokea hicho kidogo unakuwa umekikubali moja kwa moja.
Swali ni kwanini tumeamua kukaa kimya huku mali yetu ikiedelea kuibwa bila huruma na sisi kugeuzwa kuwa omba omba> Je hizo halmashauri ni nani aliezipa huo uwezo wa kufanya maamuzi ya utumbo kama haya???
kwa madiwani wengi ni darasa la saba huko mara! huo ni ukweli mtupu!