Ni 2019,hivi Hamisa bado ana miaka 24?

Dec 9, 2018
66
52
2018 ndo imeisha hivyo,tupo 2019 tunaelekea 2020,sasa wewe 'sista duu' endelea kumsubiri mwanaume mrefu ,handsome,mwenye gari ,msomi,mwenye pesa,mweupe,supasataa n.k.Nasema endelea kusubiri.

Mademu wa mjini wana vituko sana.Akigundua mwenzake kamzidi hata wiki moja ni kosa ,utasikia Da Nuru,Da Jeska,Da Eliza,,,wanapenda utoto kuliko ndoa.Ukiwaambia chagua kati ya pesa ,ndoa au umri mdogo,90%watachagua utoto.Hawataki kuzeeka.

Ndio maana wanasherehekea birthday bila kutaja umri wao.Wanaotaja wanapunguza miaka utadhani wanataka kusajiliwa na Man United.
Atakwambia ana miaka 24 na ameanza kutoka na Diamond Platnumz miaka 9 iliyopita.Ina maana kaanza ngono akiwa na miaka 14 ,,Hamisa Mungu anakuona .

Wengi wakifanya birthday wanacheza kwenye miaka 21-29 yan 30 inawakera sana mastaa wengi.Tunasaidia wanaofanya upuuzi wakijiona watoto,,au kutokujipanga kimaisha wakiamini muda bado.

Wema Sepetu alishiriki na kubeba taji LA Miss Tanzania 2006.Hapo changanya Uwoya ,Jokate,Aunt Ezekiel na wenzao .Hiki ni kizazi cha Miss Tanzania kilichoivamia Bongo muvi na kuiteka.

Kuanzia 2006 hadi sasa ni miaka 13,na Miss Tanzania mshiriki lazima awe na miaka 18-22.Kwa hiyo hapa tuwape wote miaka 19 waliposhiriki 2006.Tupige hesabu rahisi (19+13=32)Huo ndio umri wa Wema na wenzake labda upungue au kuongezeka mwaka mmoja .
Kama walidanganya ili washiriki,wanastahili kushitakiwa pamoja na Basata yao wore sukumia ndani kwa kuacha watoto washiriki.

Malkia wa kaskazini ,Jacqueline Wolper haeleweki.Kafanya umachinga wa sufuria ,alitoka kimapenzi na King wa Kariakoo.Piga hesabu ya kumaliza shule ,umachinga ,na King wa Kariakoakiwa undergroundutagundua kala chumvi.

Elizabeth Michael 'Lulu' mwaka 2011 aliwahi kufanya birthday ya kutimiza miaka 18 ,,mwaka 2012 alipopata kesi ya kifo cha Marehemu Kanumba umri ukapungua.Huenda ni kwa sababu ya matatizo.

Wacha tusimaamie miaka take 18 mwaka 2012.Kale katoto kalifanya birthday ya miaka 18 mwaka 2011 ili kaanze kuruhusiwa kuingia klabu na kupiga ulabu.Mwaka 2012 hadi sasa ni miaka 7 .Kwa hiyo (18+7=25) Lulu ana miaka 25.

Acheni kina Samatta na Msuva wadanganye umri kwa sababau mpira ni ajira yao na ni ya muda mfupi .Ukizingatia miili ya kiafrika haikongoroki ovyo kama ya wazungu.

Mwanasanaa ni ama mvinyo ,anavyozeeka ndivyo anavyoZidi kuwa bora zaidi kisanaa.
 
Hao ni wa kuzowea tu Mkuu sababu mwisho wa siku kama kuna faida au hasara inakuwa kwao.
 
mbona Museveni kabadilisha mpk cheti itakuwa hawa??
wakati ni ukuta siku zote
 
Sielewi ujue!

Watu wanajua kujihangaisha aisee!

Umri wa mtu mimi sijui hata unanihusu nini????
Mi sijawah hata kujiuliza mtu flani ana miaka mingapi, labda partner wangu ili nijue birthday lini, maisha ya mastaa ni entertainment tunatakiwa tufurahie kile kinachooneshwa tu sasa haya mambo ya huyu ana miaka 43 huyu 25 naona km tunatumia ubongo vibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom