NHIF ni taasisi ya ovyo haijawaitokea duniani!!

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,439
859
Habarini wadau,
Katika taasisi mbovu hii imepindukia kiasi cha kuhatarisha maisha ya wananchi.

Wamefuta baadhi ya makundi yaliyokuwa wanachama wao pasipokutoa taarifa yoyote kitu ambacho ni usumbufu sana kwa madai kuwa wangeanzisha huduma nyingine mubadala kuanzia tarehe 1/9/2019 lakini hawajafanya hivyo na hakuna dalili wala majibu ya kuridhisha.

Sasa kwanini wasiruhusu watu warenew kadi/uanachama wao kwa makundi ya zamani hadi watakapokuwa tayari ndiyo wafute au watajiondoa automatically wenyewe

Rais saidia hili jambo siyo taasisi zinakuwa zinajiamulia maamuzi yao tu bila kujali adhali zitakazojitokeza wananchi hawapati matibabu wakati kadi wanazo na majibu mazuri hamna
 
NHIF nadhani pesa nyingi inaenda kwenye "Branding" mishahara minono, Makongamano, semina (posho) na V8/VXs. Wanachama wanadhalilika utadhani wanatibiwa bure?
Pili, sijajua uharaka (idadi ya siku toka kuwasilisha madai mpaka kulipwa) wa ulipaji wa madai yakifishwa kwao.
NB: endapo mwanachama atahitaji Miwani ya kusomea basi mfuko huchangia 18,000/= Tshs. Sasa sijajua kama ni miwani gani ya kiasi hicho.
 
Ni ushenzi wanafanya
Mkuu pole,kwa maoni yangu NHIF,ni taasisi ambayo tangu kuanzishwa kwake imejotahidi Sana...Changamoto zipo ,lakini sidhani Kama wanastahili matusi.badala ya kutukana tuwasilishe hoja na mapendekezo ilo NUIF
 
Hoja ipi unadhani wanawezaifanyiakazi nje ya hoja zao wenyewe?

Kila leo wanabadili masharti halafu wanasema mwanachama mpya hasitahili baadhi ya huduma sasa kama kila siku wanabadilibadili aina ya uanachama ni wazi wanachama watakuwa wapya kila siku
 
Umoja/vyama vya wafanyabiashara wanadai wamebaki na AMCOS/SACCOSS tu
SACCOS wanadanganya hata hao SACCOS wameondolewa bila taarifa Mimi nipo kwenye Saccos lakini wanachama wetu Sasa hivi hawapati matibabu wakienda hospital wanarudishwa NHIF ovyo kabisa
 
Back
Top Bottom