NHC Kijichi hizi bei

Ila iyo bei na location ndio utata pia nyumba zingewekwa moja moja inapendeza zaidi kuriko kushea ghorofa kwa iyo price
 

Yaani nilipie hela zote hizo nikaishi kwenye hosteli au kwenye squatters.

Poleni NHC, hamna wataalamu Wazuri wa Real Estate Investments and Projects.

Poleni Sana
 
Bado monthly home association payment.

Hapo unaweza ambiwa uchangie 300,000 kila mwezi for security, takataka, lift, usafi wa mazingira n.k
Service charge hio. Nyumba yako ila kila mwezi unaweza kujikuta unalipa kodi ya pango ya Goba.
 
Mkuu huku ulaya ndo zetu walala hoi hizo terrace, semi terraced, detached na semi detached na town house ni za matajiri.

RRONDO mrangi
Hawawezi kukuelewa. Mtu kazoea aishi na bata mbuzi kuku apartments ataziweza wapi? Halafu asilimia kubwa wanaonunuq hizo sio first time home owners.
Wengi wananua kama investments, short term rental kama Airbnb
 
Ukishakabidhiwa jiandae na maboresho kibao pia. Mafundi Juma na Fundi Michael wanakuwa washafanya yao.
 
Viongozi wa hii nchi kwa ujumla hawapo in contact na reality, yani kwa kuwa wanapiga na kujipakulia tu pesa za umma muda wote huwa wanasahau maisha ya mtu wa kawaida yanafananaje. Hizi bei wanajiundia mezani tu hadi unajiuliza wao hivi vifaa vya ujenzi huwa wanafitoa Mars au kwa hawahawa akina mangi kariakoo na China. Source kubwa sana ya inflation wakishapiga wanamwaga mamia ya mamilioni mtaani kwa vitu vya hovyo na kuvipandisha bei including bei ya uchi kule rivasaidi na mitaa ya sinza
 
Yaani nitoe milioni 112 kwenye makazi kama mabweni ya wanafunzi wakati nikienda hao kibaha napata kiwanja kikubwa MIta 100 Kwa 100 Kwa shilingi milioni20-30.ukiishi kwenye apartment ni matumizi mabaya pa pesa
Kwa sisi tunaopenda kuishi kwenye nafasi natoa million 20 namiliki ekari mia Moja hapa pwani pembeni kabisa ya dar iliyobaki nashusha mjengo Wa maana nikipata na usafiri wangu safi kabisa halafu mtu ananiambia nitoe zaidi ya million mia kununua kile chumba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…