NHC: Hatuuzi nyumba, tutajenga mpya 15,000

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,972
3,830
Na John Ngunge

14th June 2011
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limesema kwa sasa halitauza nyumba zake kwa wananchi,badala yake linaelekeza juhudi zake katika ujenzi wa nyumba mpya 15,000.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC, Kesogulewele Msita, alisema hayo jijini hapa jana wakati akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu maombi ya wapangaji kuuziwa nyumba.
"Nyumba za NHC zilizopo sasa hazitauzwa…na Bodi imeuagiza uongozi wa shirika kuelekeza juhudi zote katika ujenzi wa nyumba mpya 15,000 ambazo asilimia 70 zitauzwa kwa Watanzania wengi na asilimia 30 zitapangishwa," alisema. Alisema mpango huo utafanyika ndani ya miaka mitano ijayo na ujenzi wa nyumba 2,500 utaanza mwaka huu sehemu mbalimbali nchini.
"Hii ni idadi kubwa zaidi ya nyumba kuliko nyumba zinazomilikiwa na shirika kwa sasa, na pia ujenzi huu ni mkubwa sana kuliko ujenzi wo wote uliowahi kufanywa na shirika katika mipango mikakati yake," alisema.
Alisema ujenzi huo utawapa Watanzania wengi fursa ya kutimiza ndoto zao za kumiliki nyumba kwa kuuziwa na pia kupangishwa kuliko hali iliyopo sasa ambapo ni Watanzania wachache wanaofaidi matunda ya shirika.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu, alisema shirika litatoa utaratibu wa wazi wa kuuza nyumba hizo utakaowawezesha watu wa makundi yote na bila ubaguzi kupata nafasi ya kununua nyumba.
Alisema shirika lake limewekeza shilingi trilioni 1.5 kwa ujenzi wa nyumba hizo ambazo zitaanza kuuzwa baada ya nyumba kukamilika.
Alisema baadhi ya nyumba ambazo zimechakaa na kupitwa na wakati zitabomolewa na kujengwa nyumba za kisasa zaidi na kwamba ujenzi huo kwa kila mkoa utategemea na uhitaji, uwezo wa wananchi wa mkoa husika wa kununua na ushiriki wa viongozi wa mkoa husika katika kutoa viwanja.
Alifafanua shirika lake kwa sasa lina nyumba za kibiashara zipatazo 6,840 na za kuishi 9600 ambazo zimepangishwa kwa watu mbalimbali.



CHANZO: NIPASHE
 
Hii habari faida yake nini wakati Mawaziri, Majaji, Makatibu wa Wizara wanakaa hoteli. nyumba walizokuwa wanakaa zamani wameuziana watawala wetu bei rahisi kabisa
 
kwenye itv mdahalo alisema msimamo wa kuuza nyumba kwa 70% upo pale pale na 30% ndio zitzkazopangishwa
 
hao wahindi waende wakanunue nyumba huko kwao india, hizo za upanga ni za watanzania nawachukia wahindi sana
 
Back
Top Bottom