Red Cross kuwajengea nyumba waathirika Hanang'

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

Red Cross Kuwajengea Nyumba Waathirika Hanang'

Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania linaendelea na ujenzi wa in nyumba 35 kwa waathirika wa maporomoko ya udongo wilayani Hanang ikiwa ni hatua ya shirika hilo kusaidia jamii.

Rais wa Red Cross Tanzania, David Kihenzile amesema kati ya nyumba 101 zinazojengwa kwa waathirika hao nyumba 35 zinajengwa na shirika hilo ikiwa ni sehemu ya majukumu yake pale yanapotokea maafa.

Kihenzile ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi amesema, pamoja na kazi kubwa iliyofanywa wakati wa maafa hayo, shirika hilo pia limeona lijenge nyumba 35 ikiwa ni sehemu ya kuisaidia Serikali kuhudumia waathirika hao.

Ameongeza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan ameandika barua ya kuishukuru Red Cross kwa namna walivyoshiriki katika kutoa huduma mbalimbali wakati wa maafa hayo.

WhatsApp Image 2024-02-19 at 14.49.47(1).jpeg
 
Back
Top Bottom