NHC: Hatujamuonea Mbowe

Hata NHC imeamua kufanya siasa! pathetic
 
Nonsense Mwasenga, anadhani wote ni wapumbavu/ majuha kama yeye! Why start with Mbowe?
 
Tunaishi katika jamii ambayo bado ni duni kivitendo na kifikra. Kwa vitendo kama hivi ni vigumu sana nchi hii kupata maendeleo. Tunaongelea nchi ya viwanda, hivyo viwanda vitajengwa na wanachama wa CCM pekee yao? Maana siamini kwa mtu ambaye siyo mfuasi wa CCM kama anaweza kufanya uwekezaji mkubwa usiohamishika kwa kipindi hiki kutokana na hofu inayojengwa.

Ni mjinga pekee yake atakayeamini kuwa limefanyika hili bila ya sababu za kisiasa maana hata maelezo yenyewe yapo wazi kuwa, 'tumeanzia na Mbowe ....', sababu za kuanzia na Mbowe hazikuelezwa.
 
Hiyo kauli ya " pamoja na wadaiwa kuwa wengi tumeamua kuanza na Mbowe " tu ni ushahidi wa wazi kwamba tukio hili limefanyika kisiasa!
 
Suala la Mbowe ni la kibiashara zaidi. Hakufuata masharti ya kupanga. Msichanganye masuala ya biashara na siasa
Hii ni full politics usidanganye watu hapa. Na kumbuka kipindi nccr iliposhika kasi miaka ya 1999 wafanyabiashara wengi walifanyiwa figisu kama hizi za Mbowe hadi baadhi kubambikiwa bili kubwa na madeni ya tanesco na tra kule iringa. Ushahidi upo kwani yule mzee hoteli na biashara zake zilifungwa hadi alipokubaki kuwa kada wa ccm. Siishangai nhc kutumikia ccm badala ya watanzania wote kwa haki.
Ccm isisahau kuwa hati miliki ya kuiongoza nchi hii wanayoforce kuirenew ipo jirani kukoma kama kuwadhoofisha wale wenye mawazo mbadala kupitia riziki zao ndio dawa basi watafute mbinu nyingine. Wasisahau wenye mawazo mbadala wengi wao hawana biashara. Na kwa maana nyingine ccm msijisumbue kumfilisi maskini kwani hana cha kupoteza!
 
Lipeni kodi acheni kulialia
 
Sentensi yenye ukakasi wa kisiasa ni

"Wadaiwa wapo wengi, ila tumeamua kuanza na Mbowe"
 
Kwasababu ni mdaiwa sugu na deni lake ni kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…