Nguvu ya uumbaji ilishafanya kazi yake nzuri ya uumbaji, ni binadamu ndiye aliye uwanjani sasa

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,542
3,451
Binadamu ni kiumbe aliyejaliwa uwezo mkubwa sana kuliko viumbe wengine wengi Duniani.

Binadamu leo anaweza kuumba ayatakayo ikiwa tu atauelewa ilimwengu wa ndani unavyofanya kazi yake. Kwanza kabisa tunapaswa kujua hakuna kitu chochote alichokiumba mwanadamu ambacho hakijaanzia ndani yake.

Leo ukiona mambo mengi yawe mazuri au mabaya elewa kuwa yalianzia kwenye ulimwengu wa ndani wa binadamu na kinachoonekana nje ni zao la mvuto "impression wa kilichokuwa ndani.

Uwezo wa kuamua inatokana na uthati "commitment" katika kupangilia mawazo yetu, hisia zetu miili yetu na nguvu za uhai kwa kuzielekeza kwenye upande mmoja ambao ndiyo tunaoutamani bila kubadilishabadilisha.

Leo tunaona kama uumbaji ni suala li aloshondikana kwa sababu ya kutokujua hasa nini hasa tunakihitaji ili tukiumbe na pia kubadilishabadilisha uelekeo wa mawazo yetu na nguvu za uumbaji. Tunapaswa kujua ni nini hasa tinakihitaji ili tukivute.

Hatupaswi kuafiki kuwa uzoefu uliopita kuwa ndiyo kigezo cha uumbaji wetu.Kwa sababu kilichoshindikana jana haimaainshi kitashindikana leo.

Suala la kuwezekana au kutokuwezekana siyo la kwako ila ni suala la asili "nature"unachopaswa kufanya wewe ni kujiumbia mile unachotaka na kuelezea mawazo yako nguvu na mwili kwenye uelekeo mmoja bila kuumbayumba.

Usijitengenezee mawazo hasi juu ya kile aunachokitamani,endekea kukiumba na kuelekeza mawazo yako ili kukiumba na kukivuta kwako badala ya kukikwamisha kuja kwako. Baadhi ya watu hufundisha juu ya kuwa na imani ili kusaidia kutunza mawazo chanya kwa lengo la kuwafanya watu kutobadilibadili uelekeo wa natamani yao.

Uliopo uwanjani leo ni sisi wanadamu yaani Mimi na Wewe, tulishaumbiwa Ulimwengu mzuri na Muumbaji Mkuu, ni jukumu letu sasa kuumba yale tunayoyahitaji na siyo kusubiri tuumbiwe tena.
 
Mkuu uliyeniambia nikaumbe dawa ya kuondoa Corona jibu lako lipo ndani ya andiko nililolitoa.
Nafahamu unataka kuzungumzia kushindikana au kwa maana ya karibu unalenga kusema " Siwezi" kutenda nilichokiandika.

Unapaswa kuelewa kuwa suala la kuwezekana au kutokuwezekana siyo langu ila suala langu ni kuumba yale ninayoyataka take kwangu kwa dhati.

Na uumbaji huo inatokana na uelekeo wa mawazo yangu nguvu, hisia na mwili wangu bila kubadilikabadilika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom